Natamani News presenters wa Kenya wangekuja Tanzania

Samahani kwenye hoja yangu hapo juu nimeanza na jina LA shabani kissu kimakosa, naomba samahani kama nitaleta usumbifu wowote Kwa mhusika, kwani jina tajwa halihusiani na mchango wangu ktk mada.
unaweza kuedit na kufuta jina
 
Jeff Koinange, July Gichuru ni noma....

Leo kuna mahojiano ya RAO na Hussein Mohamed. Usikose kumwangia Babaa
 
Tuko pamoja mkuu hawa jamaa wapo vzuri sana, kuna mmoja anaitwa hussein mohamed kesho anamhoji raila odinga saa tatu usiku, sikiliza maswali ya jamaa. Hvi wandishi wetu si wajifunze namna ya kuhoji na kuliza maswali.

Waandishi wetu ni kama viongozi wa TFF.. Wao siku zote wanawaza kuteuliwa viti maalum..!
 
Waandishi wetu huhoji kwa unyenyekevu na nidhamu ili waingie kwenye droo ya uteuzi wa Ma-DC na Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya.
 
Ili mwandishi awe mzuri kwenye interview inabidi producer na team nzima iwe nzuri nyuma ya camera.

Mfumo wetu wa elimu na watu wetu hawapendi kusoma kujielimisha nje ya mfumo. Binti anasomea Journalism utoto mpaka ujana yeye hajawahi kutazama taarifa za habari,akisoma gazeti anasoma la udaku,muziki,insta za wasanii,vipodozi,ngono,kudanga.

Shule anafaulu kwa kudesa,ngono kwa mwalimu akijakuajiliwa kwenye media house anakuwa hana additional value yoyote.

Content yake kichwani inakuwa ya kitaarab taarabu tu. Huyu hawezi kufanya interview ya maana. Hata wanaume wako hivyohivyo. Juzi kuna news presenter wa channel ten dada alipata shida kutamka mji mkuu wa venezuela Caracas.
 
Shabani kissu,

Samahani kwenye hoja yangu hapo juu nimeanza na jina LA shabani kissu kimakosa, naomba samahani kama nitaleta usumbifu wowote Kwa mhusika, kwani jina tajwa halihusiani na mchango wangu ktk mada.

sasa kama hukuwa na nia ya kumtaja Shaban Kisu kwa nini usiedit comment yako? si kuna sehemu ya ku click edit unapata nafasi ya kufuta hayo maneno?!
 
Tuko pamoja mkuu hawa jamaa wapo vzuri sana, kuna mmoja anaitwa hussein mohamed kesho anamhoji raila odinga saa tatu usiku, sikiliza maswali ya jamaa. Hvi wandishi wetu si wajifunze namna ya kuhoji na kuliza maswali.

Kituo gani mkuu?
 
Wamiliki wa vyombo vya habari waweke exchange programme/ mikakati ya ushirikiano,

Mikakati hii itafanya waandishi wa bongo wawe wanaenda japo kwa miezi mitatu kenya,uganda,China,south Africa,ulaya au marekani,kutegemea na chombo kilipopata partner na ajenda ya chombo kwa kipindi hicho,may be kuongeza ujuzi kwa journalist wa uchumi,au siasa au michezo.

Nadhani pia vyombo hivi "havija-exploit" vya kutosha mashirikiano ya kikanda.

Kuna radio hurusha matangazo ya BBC,Sauti ya Ujerumani,Radio Japan,Radio France international,nadhani zinapaswa kuongeza kipengele cha mashirikiano kimafunzo.

Pia nadhani uandishi pia inahitaji kautundu kidogo,utafiti,kujisomea,kujua mazingira yanayokuzunguka ili unayemuhoji asije "kuku-trick" na facts
Issue hapa ni kuwa na waandishi habari ambao wamepata mafunzo sahihi na wanaopata mafunzo kazini mara kwa mara ya ubobezi katika maeneo yao wanayofanyia kazi, mfano habari za uchunguzi,afya,michezo,Jinai na nyinginezo. Lakini huwezi kumleta mtangazaji wa kenya hapa, je ni kwa ajili ya nini?sauti yake,msamihati wa kikenya ambao wengi hatupendi kutokana na lafudhi zao,au unapenda kiingereza chao au unataka nini maalumu kwa ubadilishanaji huo waandishi?Vyombo vingi vya habari Tanzania vinakabiliwa na uwezo duni wa kulipa waandishi hivyo kuandika habari za uchunguzi inakuwa tatizo sana. Hata hivyo kuna taasisi kama TMF(Tanzania Media Foundation) na Nyingine za kimataifa zimekuwa zikitoa Ruzuku kwa waandishi wa vyombo hivyo au Vyombo vyenyewe, kwa ajili ya kusaidia maeneo hayo. Kupata uzoefu wa vyombo vya habari vya kimataifa kupitia "Exchange programme"imekuwa ikifanyika hasa kwa vyombo kama DW na BBC. Kwa hiyo sioni mantiki ya watangazaji wa Kenya kuja hapa ambapo wataexperience same problems wanazopata waandishi wetu, kwa hiyo uwekezaji katika training za mara kwa mara na malipo mazuri ndiyo tatizo kubwa hapa ukiacha tatizo la baadhi ya wamiliki wa vyombo vya habari kuwa kikwazo katika Uhuru wa waandishi habari
 
Waandishi wa kibongo wengi shida sana,Leo clouds

TV wamemuhoji Prof Lipumba,maswali yanaulizwa bila mpangilio,kipanya hajamaliza kuuliza,Hassani kaingilia,kipindi kinaenda bila mpangilio,jaribuni kuiga kwa wenzetu,kuna kipindi kama Chechen luninga ya citizen Kenya,igeni kinavyoendeshwa,
Sasa Leo,mpaka muda unaisha,Prof hajaongelea mustakabali was CUF
 
Back
Top Bottom