Soko la ajira limekuwa gumu kweli. Kuna vijana wengi tu kwa sasa wana digrii za pili ila bado hawana ajira. Hii ni changamoto kubwa sana na inaweza katisha tamaa hata wengine kusoma. Hata hivyo bado elimu ni muhimu sana sema tu tukubali kuwa dunia ya leo inataka kuwa na vitu vya ziada sana
1: Ufaulu mzuri sana. Ushindani leo hii ni mkubwa sana. Kabla ya kuitwa kwenye usaili mchojo wa awali unaangalia papmoja na mabo mengine ufaulu. Ile dhana ya kwamba GPA sio ishu ni ya upotoshaji. Kampuni kama big four za auditing zinangalia sana vyeti. Ni muhimu sana watu wakiwa shule wakubali kutengeneza vyeti vyao hasa kuanzia form 1V hadi chuo. Ukiwa chuo na hutaki kufaulu vizuri basi tengeneza pesa vizuri. Sasa ufaulu unakuta hatupo, pesa pia hatupo,hili ni tatizo.
2: Uwezo,ni muhimu kuhakikisha kuwa mtu anaelewa mambo mengi kadiri iwezekanavyo hasa alosomea.Baada ya vyeti kukubaliwa ishu ni je vinaendana na mtu mwenyewe. Elimu za kukariri kariri hazina tena tija leo hii. Lazima ukipata A uhakikishe wewe ni A material na sio vinginevyo.
3: Vitu vya ziada. Hii ni muhimu kuliko neno muhimu. Tujifunze kutengeneza CVs ambazo ni za ukweli. Ni muhimu tukiwa shule tufanye field/practicals zakutosha. Kama ni ishu ya accnts kwa mfano ni muhimu kuangalia wapi mtu unaweza ajiriwa ukimaliza kisha kajitolee huko kwa miezi ya kutosha. Na ukipata nafasi hata ya field mahali tupige mzigo. Tushiriki katika kubuni njia bora za kuleta ufanisi. Leo hii mtu anamakiza digrii ya sociology lakini hajawahi hata kubuni au shiriki kwenye ishu ya kijamii. Kwenye interview mtu anakosa hata mifano ya kusema vitu alivotenda. Dunia imebadilika tubadilike.
4: Connections. Wengi wetu ni watoto wa maskini kabisa. Ila bado tunawajibu wa kuangalia wapi ni tegemeo la sisi kufanya kazi. Kama ni marketing kwanini tusishiki kuandaa workshop/presentations/exhibitions nk kutoka kwa wadau mabalimbali. Najua hapa vvyuo vinahusika lakini kama wahusika tunaweza kuufanya uongozi wetu ukafanya hivyo. Vyuoni kuna career days lakini mara nyingi unakauta wanafunzi wanakacha na kwenda kwenye ishu zisizo na tija. Huku ndiko network zinapopatikana.
5: Focus ya kujiajiri. Huu ni wakati wa kusoma kwa malengo. Tujiulize nikisoma digrii au masters ya .....ninauwezo wakujiajiri katika nyanja gani. Ni muhimu ubunifu ukahusika hapa. Mtu wa accnts anaweza angalia namana anavoweza kuwanzisha simple consulting firm ikawalenga watu wa kawida sana. Mfano wenye maduka, sokoni, mama lishe, bodaboda. Huku kunafursa zakutosha tu. Wengi wa hao hawajui namna ya kuweka rekodi,kutunza fedha,kukupa ndio maana wanaishia kuingizwa mkenge. Huu ni mfano tu lakini kuna namna nyingi za kujiajiri haswa kwakuungana na wengine.
Niishie hapo ntarudi baadae kumshauri dada yangu,hii ilikuwa kwwa upana tu