Natabiri Paul Makonda atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 2030

mchawi wa kusini

JF-Expert Member
Apr 18, 2018
830
897
Habari Wana JF

Nisipende kuzunguka Sana Ni Kwamba PAUL MAKONDA anaenda Kuwa Raisi Wa Jamuhuri Ya Muungano wa Tanzania mwaka 2030 tuombeni uhai

Ukweli Ni kwamba Paul makonda anapitia wakati mgumu sana ila huwa anakuwa na uvumilivu wa Kuyabeba wengi Wenu Mnamchukia sana Huyu Mwamba naamini Mungu atamsimamia kwa kila Hatua anayopita na kila baya mnalomfanyia.

Ukweli ni Kwamba naumia sana kumuona mh. Paul Makonda kila analofanya nyinyi mnaliona baya.

Hivi kwanini huwa mnamchukia huyu mwamba,hivi kwa nini huwa hampendi huyu mwamba?

Je, kitu gani kinawafanya nyinyi mum mumuone tofauti wakati makonda ni mtete wa wanyonge?

Kikubwa na kwamba binadamu wengi wa Tanzania mmejaa chuki nyingi sana juu ya huyu mwamba.

Naumia sana kumuona mtu mwenye kipawa cha uongozi mnakichukia.

Ombi langu hii hazina ya mtu kama makonda anatakiwa atunzwe sehemu ili mwisho wa siku aje kuikomboa hii Tanzania.

Poul Makonda mheshimiwa wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ajaye sina cha kuongea zaidi ila naamini kila baya litapita na utakuja kushinda hii vita.

Hapa nipo mbioni kuhama mkoa kumfuata mh.poul makonda huko ARUSHA popote atapo hama mimi nitamfuata .

Moyo wangu unafarijika kumuona makonda ananyazifa katika serikali hii.

Mungu naomba huyu mtu umtie nguvu kwa kila jambo.

Nina mengi sana juu ya makonda lakini huko ulipo nakuombea dua njema na nipo mbioni hadi mwezi wa Tano panapo majaliwa nitakuwa Arusha najisikia raha sana unapokuwa na uongozi sehemu mojawapo ya serikali ya Tanzania.

Mungu akulinde na mabaya, akuepushie wabaya wote wanaokuombea dua mbaya mh.Paul Makonda.

Nahakikisha nitakuwa mwananchi wako mwema juu yako kwa kila jambo

Ahsante.
 
Naunga mkono hoja.

Pamoja na kuwa na roho mbaya kama Waafrika na mwingine ukimuuliza why unamchukia huyu, hajui au anakopi ubaya aliosikia au kusoma ndiyo anakwambia huyo fascist, killer nk.

Uzuri hata wkt Bimkubwa anaingia wengi walishangilia sana, nilisema simpi siku 100 wala miaka yake bali hadi akitoka ndipo nitatoa "shukurani kwa mheshimiwa Rais"

Mara chache hutokea na binadamu hapangi ila Maulana.
 
Back
Top Bottom