Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 19,857
- 21,860
Katika ajali niliyoipata mchana wa leo Jumamosi May 11, 2024..
Mwenyezi Mungu ameninusuru, na amenijalia ahuweni ya mapema kwenye majeraha mabaya niliopata kwenye mguu wangu wa kulia na kwenye michubuko michache maeneo mbalimbali ya mwili.
Nashukuru Mungu pia wahusika wengine wa ajali hiyo, ikiwa ni pamoja na dereva wangu, ambao vilevile wanaendelea vizuri. Hakuna alie lazwa hospitalini miongoni mwa wahusika wa gari tatu waliohusika kwenye ajali hiyo....
Nisingependa kumlaumu yeyote kwamba ndie sababu ya ajali ile. Sifa na Utukufu ni kwa Mungu sote tuko hai, athari za kwenye magari zinarekebishika.
Rai na wito wangu kwa watumiaji barabara wote.....
Ni vema kuzingatia sheria za barabarani, kuepuka kilevi na mwendo kasi kiholela, na daima kua waangalifu na makini barabarani, na kuhakikisha vyombo vitumikavyo barabarani ni salama, havina hitilafu zenye uwezo wa kusababisha ajali au uharibifu usio wa lazima, licha ya kwamba ajali haitabiriki na wala haitarajiwi na yeyote miongoni mwetu.....
Nawatakia safari njema watumia barabara wote humu nchi. Safiri Salama 🐒