Nashauri TANESCO iwapunguzie Deni Wadaiwa wake kwa nusu ili walipe

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
58,910
69,628
Deni la zaidi ya Bil.244 ni Pesa kubwa sana ili kuwahamasisha kulipa deni na kuleta mapata Tanesco ni vyema wawapunguzie.

=======

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawadai shilingi Bilioni 244 wateja wake mbalimbali, wakiwemo wateja wa umma na wateja binafsi.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Nishati Stephen Byabato wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Tawhida Galos aliyehoji kuna mpango gani wa kukusanya madeni ya TANESCO katika taasisi kubwa ili shirika hilo liweze kujiendesha.

Byabato ameongeza kuwa ili kuzuia ukuaji na kuwezesha ukusanyaji wa madeni, TANESCO wameweka mita za LUKU kuhamasisha na kufuatilia madeni na inapobidi kukata huduma ya umeme kwa wateja wenye deni kubwa na sugu ili liweze kulipwa.

Chanzo: TBC
 
Habari ndugu mteja asante kwa kuwasiliana nasi kupitia ukurasa huu, tumepokea taarifa na maoni yako juu ya swala hili tutalifikisha idara husika kwa utekelezaji.^OK
 
@TANESCO hiyo ok mnayoweka mwisho Ni ya Nini?
 
Back
Top Bottom