Nashauri serikali ipunguze masharti kwenye vyuo vya ufundi (VETA)

MUME MASKINI

JF-Expert Member
Jun 11, 2019
203
282
Wasalaam,kama kichwa kinavyojieleza hapo juu.

Nashauri serikali ipunguze masharti kwenye vyuo vya ufundi(VETA) ili vijana ambao hawakupata nafasi ya kufika form 4 waweze kupata elimu ya VETA bila mahitaji ya cheti cha form 4.

Kuna vijana ambao waliharibikiwa utotoni kwa njia moja au nyingne lakini wanahitaji kujifunza kwa vitendo ili wapate taaluma za kazi mbalimbali za mikono lakini hawana vigezo ktk vyuo vyetu vya kiserikali au binafsi. Mfano:

  • Udereva
  • Ubaharia
  • Ufundi mbalimbali(VETA)

Wote hawa wanahitajika vyeti vya form 4 ili kupata mafunzo (VETA)
Ni vyema serikali ikatoa katazo la cheti cha form 4 ili vijana waweze kupata mafunzo na kuweza kujiajiri au kuajiriwa.

Leo mtu anataka ajifunze kuendesha fork lift anaambiwa awe na cheti cha form 4.

Anataka ajifunze kuendesha crane awe crane operator anaambiwa cheti cha form 4.

Anataka ajifunze kuendesha skaveta anaambiwa cheti

Anataka asome ubaharia kuna sehem mwisho anakwama anaambiwa cheti cha form 4.

Wakati huko melini wala huulizwi hiko cheti cha shule Zaidi ya kuulizwa vyeti vya meli (STCW.)

Sasa najiuliza hivi cheti kinasaidia nn ktk kujifunza kazi za ufundi stadi?

Kwann huwezi kujiunga VETA bila cheti cha form 4?mbona wazee wetu walihitajika cheti cha darasa la saba pekee kusoma VETA?

Halafu haya mambo yapo hapa Tanzania tu.

Ukienda Sout Africa na kwenginepo ulaya / USA hakuna upuuzi huo.

Serikali ondoeni katazo la cheti ili vijana walioharibikiwa utotoni waweze kusomea fani za ufundi stadi VETA..
Hilo litaondoa ukakasi wa vijana kupata ajira.

Zamani ilikuwa ukifeli darasa la saba unapelekwa VETA. Ukasome ufundi stadi au udereva au ubaharia..nk.

Lakini sasa hawa wasomi wetu sekta zote wanataka wao.

Hilo ndy tatizo. Vijana wanazidi kuharibikiwa mitaani. Hawajuwi pakuanzia wala pakushika.

Lakini wakitoa katazo la cheti litakuwa mkombozi kwa vijana wengi mitaani..

Cheti kibaki kwa vyuo vingne lakini sio VETA. Cheti kisiwe kikwazo cha kumkataa kijana mwenye ari na moyo wa kujifunza ufundi.

Ndy maana unakuta vijana wanajifunza magari au taaluma mbali mbali mitaani bila kupitia shule, baadae wanaleta changamoto kubwa kwenye kujuwa sheria za kazi husika.

Mfano mtu anayejifunza gari mtaani atajuwaje sheria za barabarani bila kupitia shule?

Ajali nyingi zinasababishwa na madereva bila kupitia shule ya udereva.

Serikali iangalie hilo ili vijana wapite shule za ufundi stadi VETA Ili kuepusha ajali ambazo zingeweza kuepukika.

Nawasilisha
 
Daah, jamani, hata cheti cha form four nacho mtu hana?

Hata DIVISHENI FOO mtu kashindwa kupata? KWELI?

Mtu kama huyo anataka kuendesha TINGATINGA? Ataweza kusukuma gia? Utaweza kuelewa matumizi ya barabara? Maana ni ZUZU KWELI KWELI!!!

Wengine bakini kuchanganya zege na kuuza mitumba!!! Ni kazi nzuri piaa??

Mtatusaidia sana kujenga majumba na kuchimba mitaro na barabara.
 
Naungana na mleta uzi
Kigezo Cha cheti Cha form four ili kuniunga veta kitolewe kigezo kiwe nikujua kusoma na kuandika ili tutoe fursa sawa kwa vijana kupata ujuzi.
Wengine sio kuharibikiwa utotoni hawakupata fursa ya kusoma elimu ya sekondari
 
Na ada wapunguze pia, nasikia mwaka huu wamepandisha ada zao, kutoka laki tano na sitini, na laki sita na ishirini elf, mpaka lakini nane na tisa,

Sasa ukichanganya na hostel laki tatu, kwa wanafunzi wa mbali ni zaidi ya million na upuuzi,

Sasa hapo sijui Serikali inamsaidia mtoto wa masikini au inafanya biashara?!
 
Unahisi wakifanya hivyo kuna kijana atakaetaka asome hadi form 4 kwa hali ilivyo sasa km wote hawajaishia la 6 na kuelekea VETA
kama ndio amechagua hiyo njia acha aende,hao waliofika vyuo na mavyeti wanayafanyia nini?

Mtu kama kafika la 6 kaona anataka kwenda veta aachwe aende,kote kunatoa elimu tuache kubagua watoto kwa kigezo cha cheti.

Mtu anaweza kuwa hana cheti lakini ana Utayari, hicho ni cheti tosha chakuweza kumfanya aingie darasani.
 
Una hoja,
Sema nini, hii kidogo inafanya madogo wawe serious kidogo shuleni, madogo wa sikuhizi hawapendi kusoma, na wakiwa huko shuleni ni usumbufu na utukutu, inatakiwa Ajue kabisa akitoka na mzunguko, hakuna atakapoenda kiprofessional zaidi ya Mishe zake Binafsi(biashara n.k)

Hii itawafanya angalau wajitahidi, watulie, wasitoke kapa, hii itawasaidia pia kupata chochote kitakachowasaidia...
 
Back
Top Bottom