Wanabodi wanajamii na watanzania kwa ujumla, nawasihi kila Siku kwamba namuona Magufuli kwenye sura za akina sokoine, Nyerere, Mkapa, Tumain el Kihwelu, na saa Nyingine ni kama Mrema Wa enzi zile,
Kwanza tumjue Magufuli ni nani,
Magufuli ni rais Wa jamhuri ya muungano Wa Tanzania,
Mambo yapi yanayoonesha magufuli hana utani kazini wala hataki kukwamishwa,
1. Wakati huu mamlaka zimekuwa active zaid kushughulikia wale wakosaji hata kabla ya yeye kutamka lolote maana wanajua akitamka ni mbaya zaid, bora watende kabla hajatamka
2. Magufuli hataki kutoa ahadi za kuridhisha tu , kama haiwezekan ni haiwezekan, fuatilia hotuba zake nyingi,
3. Magufuli ni mtu asiyependa kukwamishwa wala kubishiwa au kumtoa kwenye misingi anayoamini yeye,
4. Hacheki na MTU na hapendi kujaribiwa na hajaribiwagi
5. Upinzani na watu kwa ujumla wapo.kimya na wanachunguza maneno kabla hawajasema, imekuwa kama mwalimu nyerere vile, ukisema vibaya au kukashfu uko mikononi
6. Wala rushwa na wabadhirifu wanahaha wanashindwa wafanye nini kila kukicha maana njia zote kazibana
7. Magufuli ameweza kuelekeza hela za rambirambi bukoba zifanye mambo ya jamii ya bukoba na hakuna Wa kuhoji wanahoji chini chini,
8. Magufuli anania njema na Tanzania hivyo ukitaka kuleta ujinga tutakutunza sehem Salama kwanaza
9. Magufuli ndo kafanya Maalim seifu kukaa kimya na kuishia kujifariji kuwa kesi iko ICC, na kakataza fyokofyoko.
10. Magufuli ndo kafanya mnyika, mdee na wengine kukaa kimya maana utawala huu hauhitaji ujinga,
11. Magufuli ndo amesababisha Tanzania kujulikana upya uku Nje tulipo na kutambulika sana kama nchi yenye heshima,
12. Kama humjuhi magufuli hebu jaribu kumjaribu maana hata thread nyingi zinafutwa na mods kwa kuogopa,
13. Magufuli kafanya shilling ithaminiwe tena hakuna tip tena kwenya hoteli na bar
14. Mi namuona Magufuli kama MTU sahihi kuongoza nchi ambayo ilikuwa imepinda ,
Dah Magufuli!!!!!!!!!!!