Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,042
- 10,787
Nape Nnauye amemweleza Rais Samia kwamba watu wengi wanaopiga kelele mitandaoni wengi wao hawako Nchini Tanzania na hawapigi kura hivyo asiwe na wasiwasi maana wapiga kura wengi hawako mitandaoni "achana na kelele za mitandaoni"
Nape amesema kwenye mitandao ya kijamii kuna watanzania asilimia 16, wengi hawako kule. Zile kelele zote unazozisikia ni 16%, na katika hao asilimia 40 wako nje ya nchi na hawana mpango wa kurudi nchi hivyo kelele zote unazosikia ni za nje ya nchi, wapiga kura wako hapa unawaona.
Ameendelea kusema kuwa wale wanaotegemea kura za mtandaoni wacha wagawane hizo asilimia 16, CCM isonge mbele kuletea watanzania maendeleo.