Mbunge wa jimbo la Mtama mkoani Lindi kupitia tiketi ya CCM, Mhe. Nape Moses Nnauye ametoa duku duku lake la moyoni kwa kusema kila anapokumbuka shida wanazozipata wananchi humfanya aonekane mkorofi kwa kuwa anasema ukweli.
Nape amebainisha hayo, kupitia ukurasa wake wa kijamii wa twitter huku akiwa ameambatanisha na picha ambayo inaonesha wananchi jinsi wanavyopata tabu kuvuka upande mmoja wa mto kwenda upande wa pili kwa kupita ndani ya maji hayo.
“Niliyashuhudia maisha haya mikoani kwa miezi 38, nadhani ndiyo nikiyakumbuka naonekana mkorofi !! iko haja kama Taifa kuangalia vipaumbele vyetu”. Ameandika Nape