Nape Nnauye awekwe anapopataka, 'anaidhalilisha' serikali ya JPM

Watanzania tuko zaidi 45 millions,
Inakuwaje MTU mmoja anakuwa vyeo vingi, unakuta MTU mkuu wa wilaya hapo hapo mbunge bado haitoshi anaongezewa Na uwaziri hii imekaaje jamani ina maana yeye ni bora kuliko engine
 
Kwani waziri lazima uwe mtoa tamko?
Yeah ndo style za serikali ya CCM, rais anatoa tamko, Katibu mkuu anapinga tamko, waziri naye anatoa tamko, mwenye kiti wa chama anatoa tamko, Chama Na serikali inaendeshwa kwa matamko Na kushtukiza, sasa Nape lini ameshtukiza Na kutoa tamko km waziri naona tangu awe waziri anatamka kichotara chotara tu
 
Magufuli alifanya makosa mawili kwa nape.
1.kumpa uwaziri kisa alimsaidia kutukana wapinzani wakati wa kampeni amempa mzigo mzito.
2.Kufuta semina elekezi kwa kuwa nape hajawai kuwa serikalini hivyo hajui majukumu ya serikali, huyo semina ingemfundisha kujua majukumu yake kama waziri, kwa sababu hadi sasa hajui hata majukumu yake.
 
Bahati nzuri wamemuweka wizara inayomfaa. Habari za wenzie "Lukuvi avamia ofisi ya ardhi", yeye zake zitakuwa "Nape avamia Twanga", "Nape amtumbua petimani", "Ujio wa Nape LeMutuz akimbia ofisi" :D
 
Bahati nzuri wamemuweka wizara inayomfaa. Habari za wenzie "Lukuvi avamia ofisi ya ardhi", yeye zake zitakuwa "Nape avamia Twanga", "Nape amtumbua petimani", "Ujio wa Nape LeMutuz akimbia ofisi" :D
teh teh teh kwa mipasho hata hadija kopa haoni ndani..nape atakuwa na matatizo sio bure
 
Mzee wangu huyo naona REMOTE imeelekeza kwamba ndiyo Channel ya kubofya huko.Vinginevyo hakustahili kuwa waziri wala naibu waziri kuna maeneo Mheshimiwa amepitiwa lakini hapo amechapia kabisa tena kwa udongo kwenye nyumba ya block
 
Last edited by a moderator:
Nilikwambia achana na nape lakini bado unamfuatafuata. na katika kumfuatafuata hutaji kakosea wapi, kachanganya wapi, hili la chama na hili lilipaswa liwe la serikali n.k huko si kumsaidia nape.

Unakuja hapa unaanza lisakata rhumba kwa ustadi mkubwa wakati hatusikii huo muziki
unaocheza.

Unapomkosoa mtu, taja na yale anayokosea ili ajirekebishe, atakushukuru. lakini ukija kimipasho kama mwimba taarabu unaleta wingu zito kati ya nape, mashabiki wake na wewe. haifai kuwa hivyo.
 
Last edited by a moderator:
Mzee TupaTupa umejitahidi kuibeba UKAWA lakini umeshindwa. Upo peke yako. Huna anayekussuport. Umepwelepweta. Ungeeleza wapi Nape kachanganya mambo tungekuelewa. Akiwa Waziri anatekeleza vema majukumu yake. Na Jana kaongea kama msemaji wa chama bado umechanganyikiwa. Najua kilichokuchanganya ni pale alipomjibu Tundu Lissu kuwa kama CHADEMA wanataka kuendelwza vita dhidi ya Ufisadi, basi watangaze kumuunga mkono Rais Magufuli na wawafukuze waruhumiwa wote wa Ufisadi wakianza na Edward Lowasa. Basi. Ni hapo tu alipokuchanganya Nape kwa vile wewe TupaTupa ni uzao wa mafisadi
CCM imemtimua nani kwenye chama kwa tuhuma za ufisadi labda tuanzie hapo, na Magufuli kamtimua nani kwenye chama kwa ufisadi hebu tuangalie na hapo pia.
 
Mzee TupaTupa umejitahidi kuibeba UKAWA lakini umeshindwa. Upo peke yako. Huna anayekussuport. Umepwelepweta. Ungeeleza wapi Nape kachanganya mambo tungekuelewa. Akiwa Waziri anatekeleza vema majukumu yake. Na Jana kaongea kama msemaji wa chama bado umechanganyikiwa. Najua kilichokuchanganya ni pale alipomjibu Tundu Lissu kuwa kama CHADEMA wanataka kuendelwza vita dhidi ya Ufisadi, basi watangaze kumuunga mkono Rais Magufuli na wawafukuze waruhumiwa wote wa Ufisadi wakianza na Edward Lowasa. Basi. Ni hapo tu alipokuchanganya Nape kwa vile wewe TupaTupa ni uzao wa mafisadi

Uko CCM wameshafukuza wangapi?Akina vijisenti mnawaogopa hata kuwataja mpaka kampeni mlienda kumpigia.

Jitahidi kusema hii ni blue na siyo inafanana na Blue.Na ukitaka kuona KIBANZI kwenye jicho la mwenzako TOA BORITI lililopo kwenye jicho lako.
 
Nape kiboko upinzani lazima mumchukie hamung'unyi maneno
Nchi hii haina wapinzani. Sote ni watanzania. Mtu akileta maada changia kwa uwezo wako na sio mihemko ya kisiasa. Nape ameteuliwa kuwa waziri lengo likiwa ni kulijenga taifa na sio chama. Funguka
 
Kwa upande wangu simulaumu mh. Najua alimteua kama kumpa pongezi tu. Maana ndo watu waliomsaidia kwenye kampeni. Ila hakufaa kuingia kwenye baraza la mawaziri
 
Angejifunza kutoka kwa Waziri Simbachawene alipoamua kutolea maamuzi suala la Uchaguzi wa Ma-meya wa manispaa za dar es salaam kwa kuangalia maslahi ya wananchi zaidi nadala ya maslahi ya kichama
 
Back
Top Bottom