Nape Moses Nnauye; Shujaa wa awamu kandamizi

Tunataka nchi yenye sauti moja ifuwatwe na watanzania wote, tv moja, radio moja, chama kimoja, jeshi la mtu mmoja!
 
Hongera sana Nape, binafsi sijawahi kukupenda ila kwa hili nimekupenda sana na umejiwekea heshima ya hali ya juu. Maisha sio uwaziri. Maisha popote tu, wao wako wawili, sisi tuko wengi na tupo nyuma yako.

Tangu Juzi watu walikua wanakushauri ujiuzulu ili kulinda heshima yako ila nadhani wewe ulikua unaamini Magufuli ni yule yule ulimuhangaikia na kumpigania mpaka akafika hapo alipo. Ila sasa nadhani umeona rangi yake.

Sasa kabla hawajakuletea zengwe lingine fanya hivi, jitoe huko CCM, njoo CDM, trust me Ubunge unaupata tena asubuhi tu.

You did that for us.. yes sisi wanyonge.

Mungu akubariki na kukuinua zaidi.
Amen.
 
watanzania sisi niwanafiki sana leo hii NAPE ageuka shujaa wa chadema wanamsifia kila kona hahahahahahah
 
Asiache Siasa. NAPE ni Bonge la Kiongozi, JPM kakosea sana, halafu anajua siri zote za CCM ni rahisi sana kupambana nao.

Akiacha Siasa atakua hajawatendea haki wanamtama na sisi wengine.

Kabisa....

Wache watumbuliwe na wao walikuwa wanafurahia wapinzani kuonewa wajifunze sasa
 
Nape kwa sasa kuna ngumi mfululizo za kisiasa zinakuja na inabidi uzikwepe. Usizikinge utavunjika mikono, wanaokupiga wamevaa vyuma. Mimi kama ninja halisi na sio kwa jina tu nakushauri ufanye yafuatayo ( nakushauri kwa kutumia ujuzi wangu wa ninjutsu);

1. Relax, fanya kama hakuna chochote kimetokea
2. Usihame CCM
3. Endelea kushirikiana na serikali
4. Samehe yote, maana hata wanaomsifia Kinana wanasahau Kinana alikua na mkono unaitwa Nape Nnauye, ni kama tu wanavyomsahau mzee Mang'ula.
5. Usikubali kuongelea chochote kwa sasa mahala popote pale, wala kuhojiwa, hisia zinaweza kukufanya uropoke, ukilazimika 'just be absolutely positive'.
6. Potea, kapumzike mahala fulani kimyaa, soma vitabu ujaze ufahamu wako mambo mazuri
7. Mkaribie mwenyezi Mungu sana kwa sala na maombi, ukishirikiana na familia.

Hapo ndipo ngumi zote za chuma zitapita. 'That's how a ninja wins the obvious perilous attack'.

Mods muwe mnajiongeza, hii ni 'message' kwa Nape. Sasa kwa njia hii ataionaje? Sio kila uzi mnaunganisha tu. Mimi niko porini Kakurezato, hadi nimfikie Nape kwa wakati sahihi na kumpa huu ujumbe itakua 'too late'. Au mmetumwa?
 
Mara hii watu wamesahau aliyoyasema kuhusu Bunge Mubashara !!!
Amechokankutumiwa wakati ana akilu zake
Bunge mubashara alitumiwa na akaona malalamaiko ya wananchi kibao yakamgusa sana
This time ameamua kusimamia nafasi yake kama waziri at any cost
Mawaziri wengine wanajifunza usidhani kwa hili watabaki kama walivyo
By the way uwaziri awamu hii ni kazi moja ngumu na risk
Inaweza kukuharibia status yako forever.
Kwavile mawaziri wengi wana umri mdogo
Kwa kuburuzwa huku wanaweza kuonekana hawajui kazi kabisa.
 
Basi kwa maneno hayo hata Lowasa alikuwa anatumiwa, sijui ni kwa nini watu wameendelea kumwanadama baada ya kutoka Kundini.
 
Hongera sana Nape, binafsi sijawahi kukupenda ila kwa hili nimekupenda sana na umejiwekea heshima ya hali ya juu. Maisha sio uwaziri. Maisha popote tu, wao wako wawili, sisi tuko wengi na tupo nyuma yako.

Tangu Juzi watu walikua wanakushauri ujiuzulu ili kulinda heshima yako ila nadhani wewe ulikua unaamini Magufuli ni yule yule ulimuhangaikia na kumpigania mpaka akafika hapo alipo. Ila sasa nadhani umeona rangi yake.

Sasa kabla hawajakuletea zengwe lingine fanya hivi, jitoe huko CCM, njoo CDM, trust me Ubunge unaupata tena asubuhi tu.

You did that for us.. yes sisi wanyonge.

Mungu akubariki na kukuinua zaidi.
Hata mimi sijawahi kumpenda hata jinsi alivyopata ubunge lakini kwahili nampongeza. sishauri aondoke ccm kwasasa bali aunganishe nguvu na wengine wenye mitazamo kama yake wafanye mabadiliko- ipelekwe hoja bungeni ya kutokuwa na imani na 'mungu mtu' ili turudi kwenye uchaguzi. Inawezekana kabisa. Tumechoka kubezwa na kutukanwa kama watoto. Hii ni nchi yetu sote. Hongera sana Nape. Umepata mtaji mkubwa wa kisiasa.
 
Siasa haina rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu,pale mtu anapofanya maamuzi yenye manufaa kwa taifa ikiwemo kutetea democracy anastahili pongezi
 
Daaaaa.... Hakuna fadhila dunia hii...... Katika uchaguzi alifanya mangap uyu bab jaman..... Atumbuliwe penye kosa basi sasa hata ili kweli... Halafu jumapili watu wataenda kupiga magoti kanisan wakisali. Unafki wa hali ya juu. Ila Mungu ni wetu sote
Usiku wanapiga magoti kwa Mashetani.
 
Ninakupongeza sana Waziri Nape kwa kusimamia ukweli ingawa unaweza/umekugharimu. Hili laweza kukuvunja moyo au kujisikia vibaya, ila nakutia moyo kwamba Nyota yako na heshima yako imepanda. Nikizingatia umri wako, msimamo wako, na Jinsi CCM ilivyo haina watu waadilifu na umri wao umeenda, umeianza Safari nzuri sana ambayo ukiwa mvumilivu, mtiifu na ukaendelea kusimamia ukweli itakupeleka Mahali.

Mungu na akubariki sana, regardless the cost you might pay, you will be rewarded.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom