Nape: Kasi ya CCM na Serikali yake, vyama vya upinzani vipo hatarini kufa

Nape anaongea pumba.

Hivi kweli kama anachoongea Nape kinatoka ndani ya moyo wake kuwa wao CCM wasingependa kuona vyama vya upinzani vinakufa, na badala yake wangetamani vishamiri.

Sasa naomba anijibie maswali yafuatayo:

1. Kama CCM wanatamani demokrasia ishamiri, ilikuwaje katika uchaguzi wa Umeya hivi majuzi jijini Dar, waka-import madiwani wa viti maalum kutoka Zanzibar ili mradi tu watake kulazimisha ushindi huo wa Mameya wa Halmashauri za Ilala na Kinondoni?

2. Inajulikana wazi kuwa huko Zanzibar mkwamo wa kisiasa uliopo huko unatokana na wananchi kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 25/10/2015 kumchagua kwa kura nyingi Maalim Seif na hivyo kumshinda Dr Shein. Sasa kama CCM wanatamani demokrasia iendelee kushamiri nchini, ni kwanini basi wamefanya figisu figisu hadi uchaguzi huo ukafutwa?

Kwa hiyo kinachoongelewa na Nape ni vice versa, kwa kuwa wao CCM ndani ya nafsi zao wanatamani sana vyama vya upinzani makini vife ili nchi hii irejee kwenye mfumo wa chama kimoja!
Kaka usipoteze muda wako kumbe aliyesema hayo ni Nape!
 
t
nape anaota. ni ndoto kwa upinzani kufa...
TENA nape AKIENDELEA KUOTA HIVI HATAAMKA MILELE. VIVA UKAWA, VIVA LOWASSA , VIVA MAALIM, VIVA MAKAMANDA 26JANUARI ANZENI MAMBO YENU YALE, MSIPEPESE MACHO NA KUMWONEA AIBU YOYOTE ASIYEPENDA MABADILIKO YA KWELI.
 
Akamuulize yule "binadamu wa kale" aliyesema CDM itakufa kabla ya 2015 yuko wapi sasa hivi!!!
 
Naamini hizo ni kejeli tu na vijembe kwa upinzani. Nchi yetu iko 1000000miles away kutoka kwa wenzetu wa nchi zilizoendelea. Mambo tunayoyafanya sasa wenzetu walishatoka huko siku nyingi lakini bado upinzani upo. Serikali yake Nape bado inasafari ndeeefu sana ya kuzitimiza ahadi walizoahidi wananchi. Kwanza ndio panakucha.
Kufa kwa upinzani sio kupiga hatua kimaendeleo. Maendeleo ni pamoja na kuimarika kwa upinzani no matter how existing goverment inaperfom.
Tutafikia hatua tutatoka kwenye mabarabara, mahospitali, maji , elimu na nk. Lakini bado upinzani utakuwepo tu hata kwenye sera zingine kama za mambo ya nje, mahusiano, uhamiaji na mengine. Kama mataifa makubwa kama Marekani yanavyofanya. Mfano mzuri ni sera za mgombea wa Repulican alivyosema kuhusu kuingia marekani kwa watu flan flan hivi.
 
Back
Top Bottom