Nape: CCM ikiendelea hivi wananchi hawatairudisha madarakani

Maneno ya majukwaani yanayotolewa na waandaa sera,watunga ilani,watunga sheria,wasimamizi wa sera na sheria hizo na maisha ya mtanzania wa kawaida kabisa kwa uhalisia wake ni ardhi na mbingu!Mtanzania wa kawida jitambue,jipangie mikakati yako kulingana na vipaumbele vyako kuanzia ngazi ya nafsi yako hadi familia yako!Kama ishu ni umeme kanunue sola siku hizi bei ziko chini-usisubiri rea,kama ni maji yavune-saruji imeshuka bei!Fuga,lima,au jambo lolote kulingana na mazingira yako lkn ukiwaamini wanasiasa ukakaa barazani unasubiri ahadi zao 'umeliwa'.Ajira yao ni vinywa vyao na siasa kwa mbali naanza kuona inapotoshwa,inageuzwa kuwa kama ugomvi na uhasama,Ukiwasikiliza sana kauli zao Mara kadhaa huwezi kujifunza la maana.
Ndio tutafuga tutalima ila ni nani anapaswa kututengenezea mazingira ya kufanya hayo katika ubora?tunahaki na ni wajibu wetu kuwasema na kuwaeleza aijarishi wamefanya awajafanya sisi wajibu wetu ni kuwa ambia kutekeleza ni wajibu wao viongozi,natunasema kwasababu tunaona inawezekana kufanyika isipokuwa ni mfumo wa kijinga ndo unawamaliza na kuwafanya walaumiwe,na kama wameshindwa waseme tumeshindwa watu wawasaidie mawazo na lakufanya,kujifanya unajua aitabadili kutojua kwako utabaki ujui tu.
CCM HAMTARUDI MADARAKANI KWA KURA ZA WANANCHI BALI KWA KUPITIA TUME(BAO LA MKONO II)
 
Nape bhana.... Angekuwa waziri angeyaongea haya au unafiki..... Huyu akipewa tena uwaziri haya aliyo yasema atakuja kuyakana....
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Nape amesema ukweli ambao wenzake huko kwenye chama hawapendi kusikia
Alivyokuwa na cheo alikuwa na dharau na haya anayoyasema sasa aliyaweka tumboni

Mwerevu hawezi kumtilia maanani nape

Siasa hizi bora akina Bashe ila sio wachumia tumbo kama Nape
 
Ukiisha dungwa /chomwa sindano akili ni lazima zirudi.

Eeeh, Rais wetu endelea kuwachoma sindano ili wote waendelee kujitambua. Maana wamekuwa kama "tiger paper"
 
Nape amesema ukweli ulio wazi tu.

Lakini hapa Mh Nape pia anaonyesha ukubwa wa tatizo la uongozi wetu. Akiwa Waziri anatetea kila kitu. Mbunge wa CCM hata akilia na kulalamika vipi lakini ataunga hoja mkono 100% kwa bashasha na sifa kemkem kwa Serikali sikivu na Chama. Lakini sasa Waziri wa CCM akitoka/akipumzishwa kwenye Uwaziri anaikosoa Serikali vilivyo kuliko Mbunge wa kawaida wa CCM (mfano Nape na Kitwanga wiki hii) why???
 
  • Thanks
Reactions: SDG
2015 walichaguliwa kwa kutekeleza ilani ya CCM au walichaguliwa na wananchi kwakuwa maisha ya Watanzania waliyaboresha vilivyo miaka ya nyuma?
Aliyoyafanya huyu Nape kwa kinywa chake ni mabaya sana, akitimuliwa CCM sijui chama gani kitampokea, au aanzishe chama chake.
Uwaziri mtamu, kafukuzwa sasa anaweweseka tu. Alizoea
-kutembea kwa msafara
-ving'ora
-Ukifika mkoa wowote kupokelewa na wakuu wa mkoa.
-Kutoa kauli
-Posho za safari
-Kula kwa tenda ya serikali pamoja na familia yake.
-Matibabu ya bure tena VIP pamoja na familia yake.
-Ofisi 2, jimboni na wizarani.
Haya na mengine mengi aliyoyakosa ndiyo yanamfanya kuweweseka huyu kijana.
Uchafu wa CCM haukuanza leo, huyu kashika nyazifa kubwa ndani ya CCM na hajawahi kuwaonya.
Huyu ndiye aliyetamka maneno machafu kwa vyama pinzani ili kuisafisha CCM.
Akiwa waziri wa habari , michezo na sanaa kaharibu mengi tu ,leo anakuja juujuu.
Washamwandalia dawa yake
 
Mwisho wa siku ulitaka akae kimya?
 
Uwaziri mtamu alipokuwa na wadhifa hakutoa povu wamemtoa povu la nini watajuana wenyewe
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Nape amesema ukweli ulio wazi tu.

Lakini hapa Mh Nape pia anaonyesha ukubwa wa tatizo la uongozi wetu. Akiwa Waziri anatetea kila kitu. Mbunge wa CCM hata alie vipi lakini ataunga hoja mkono 100%. Lakini Waziri wa CCM akitoka/akipumzishwa kwenye Uwaziri anaikosoa Serikali vilivyo kuliko Mbunge wa kawaida wa CCM (mfano Nape na Kitwanga wiki hii) why???
Kwanza wanajua mengi ya ndani zaidi pili Unae mtetea anapo kusaliti unarudi kuungana na waliokuwa kinyume nae iko ivyo siku zote
 
Ni kweli mkataba kati ya CCM na wananchi ni Ilani...Hakuna shaka kuwa CCM itapimwa kwa utekelezaji wa Ilani.

Bungeni ndio mahala swadakta pa kuongelea changamoto za utekelezaji wa ilani ya ccm.
Uzuri wa CCM hairukii matukio bali inafanya yale yaliyoko kwenye mpango wa kitaifa wa muda mfupi na mrefu.

Swali Kwa Nape...Je bei ya Korosho ni sh. ngapi pale jimboni mtama?na ilikuwa sh ngapi hapo awali?

TUTAFIKA BILA SHAKA...[HASHTAG]#HAPAKAZITU[/HASHTAG]
Kwani kupanda kwa bei ya korosho pale mtwara kumebadili maisha ya wananchi maeneo yote tanzania, Nape kaongelea kwa ujumla ww unaleta habari ya korosho hapa
 
Alitaka tu kuongelea kulala kila alipopita, alikuwa analipwa mshahara ilikuwa kazi yake.

Ameonyesha bado anaumia sana sana.

Mangapi mengine CCM hawafanyi na wanarudishwa madarakani kwa miaka sasa.

Huyu mwanaume ana lake.

Nape hatutaki kusikia juu yako, ongelea wananchi... kazi uliimaliza unatukumbushia nini
 
Imekuuma kukumbushwa eeh
Timiza wajibu ukachukue posho lumumba mama sawa
 
Kumkosoa Nape kwa mwanaccm haipendezi kwani ndani ya chama ktk nafasi ya unaibu Katibu ni yupi mngine atakaye wavusha ktk uchaguzi ujao kijana alifanyakazi kubwa ambaye hakuona hilo basi tutazidi kuyaona mengi sana kipindi hiki
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Back
Top Bottom