Napata hedhi mara mbili kwa mwezi mmoja, je inaweza kusababisha mayai yaishe?

Traviana Tray

JF-Expert Member
Jul 8, 2017
546
457
Habari zenu waungwana? Mimi ni mschana wa miaka 23. huwa napata hedhi mara mbili ndani ya mwezi mmoja yaani ni hivi mwezi huu wa kwanza nilipata hedhi tarehe 4 ikaisha Siku 5.

Sasa hivi tena huu huu mwezi wa kwanza nimeingia hedhi tarehe 28 hadi sasa hivi inatoka yaani huwa naingia tarehe za mwanzo na ikifika tarehe za mwisho kuanzia 28 au 29 au 30 au 31 ya mwezi huo huo ndiyo inaanza.

Sasa jamani waungwana nishaurini, je inaweza kufanya mayai yaishe au inabid nizae tu mapema?
 
Kuna mizunguko tofauti ya hedhi kwa wanawake, wapo wenye mifupi ( wewe), wastani (siku 28) na mirefu (30+)

Hauna mayai mengi ila una mzunguko mfupi (siku 24) hivyo kwa mwezi mmoja unajirudia mara 2 ni kawaida ilo kutokea.

hata uzae utaendelea pata hedhi mara 2 kwa mwezi maana kuzaa haipunguzi mzunguko wako wa siku kwa mwezi.
 
Kwa kawaida mtu anaengia period Mara 2 kwa mwezi huyo anamatatizo kwenye mirija ya uzazi na pia kunauwezekano wa kuto kushika mimba.

Kwa Ushauri mzuri na tiba ya ugonjwa wako, tafadhali wahi Hospital haraka.

Cheza na vitu vyote Dada ila usicheze na Kizazi chako (Papuchi).
 
paulina ray pole sana. Kwanza kabisa hilo sio tatizo kubwa sana na haunalo peke yako. Wanawake wengi wana hilo tatizo. Wengi huambiwa ni homon au vichocheo kutokuwiana, nenda hospitali kwa wataalam watakushauri cha kufanya.

Wataalam watakupa ushauri unaofaa, hapa nakutoa hofu tu kwamba sio ugonjwa au tatizo kubwa sana la kukufanya ujione una mikosi na laana.

Kila la kheri
 
Kuna mizunguko tofauti ya hedhi kwa wanawake, wapo wenye mifupi ( wewe), wastani (siku 28) na mirefu (30+)

Hauna mayai mengi ila una mzunguko mfupi (siku 24) hivyo kwa mwezi mmoja unajirudia mara 2 ni kawaida ilo kutokea.

hata uzae utaendelea pata hedhi mara 2 kwa mwezi maana kuzaa haipunguzi mzunguko wako wa siku kwa mwezi.
Asante
 
paulina ray pole sana. Kwanza kabisa hilo sio tatizo kubwa sana na haunalo peke yako. Wanawake wengi wana hilo tatizo. Wengi huambiwa ni homon au vichocheo kutokuwiana, nenda hospitali kwa wataalam watakushauri cha kufanya.

Wataalam watakupa ushauri unaofaa, hapa nakutoa hofu tu kwamba sio ugonjwa au tatizo kubwa sana la kukufanya ujione una mikosi na laana.

Kila la kheri
Asante nashukuru
 
Kubleed mara mbili kwa miezi hii ya kawaida (jan,feb,march, etc)inategemea na mzunguko wako wa hedhi ukoje. Unatakiwa ujue mzunguko wako wa hedhi kwa kuhesabu siku ya kwanza damu inapotoka mpaka siku moja kabla mzunguko mwingine haujaanza. Hesabu kuanzia tarehe 4 mpaka 27 utapata 24days. Hio ndio sababu unapata period mara mbili kwa mwezi January.

Suala la mayai kuisha kwa umri wako si kweli kama unavyohisi.Bado unanafasi ya kupata mtoto hata baadae endapo vipimo vya hospital vitathibitisha unauwezo wa kushika ujauzito.
 
pole dada pau

not a serious problem, nishawah date na mdada wa dizain yako. yani alikuwa anaenda mara tano au nne, mwanzon na mwisho wa mwezi.

hakuwahi nambia, sasa ikawa kipindi nmemtembelea nikitaka mambo mara anasema yupo mp, ikawa inajirudia hadi nikahisi ananidanganya, ile hali ikanifanya niwaze huyu ananibania au vp, mbona karibu kila nikitaka sipewi ? au kwa nn napewa kwa nadra sana ? siku akija kwangu ni ivo ivo, ile hali nikawa nimeizoea, simuombi tena mpaka yy anzishe.

siku nkamtolea uvivu why most of the time nikikuomba unasingizia upo MP ? Au mpaka ujisikie wewe ndio unipe ? aisee alilia kwa uchungu sana, akaanza kunielezea a-z, jinsi ambavyo mzunguko wake haupo regular, sio kwamba anapenda iwe ivyo, nilijikuta namuomba msamaha.... nilimshauri akaenda hosp, doct akamwambia yupo tu hivo no way, wapo wengi tu wa aina hiyo.

recently tushaachana, bt sababu ya kuachana sio hiyo
 
Kubleed mara mbili kwa miezi hii ya kawaida (jan,feb,march, etc)inategemea na mzunguko wako wa hedhi ukoje. Unatakiwa ujue mzunguko wako wa hedhi kwa kuhesabu siku ya kwanza damu inapotoka mpaka siku moja kabla mzunguko mwingine haujaanza..
Asante nimefarijika kiasi
 
Habari,

Pole kwa wasiwasi ulionao juu ya mzunguuko wako wa hedhi. Kwa kawaida mzunguuko uliozoeleka zaidi (ambao wanawake wengi wanao) ni wa siku 28. Lakini bado kuna mizunguko ya siku 20, 36 na 54 ambayo ni nadra.

Kwanza unapaswa kuangalia kama kuingia mara mbili kwa mwezi (yaani mzunguko wa siku 24) umeanza mwaka huu au ulianza toka lipovunja ungo (kuanza hedhi kwa mara ya kwanza).

Kama ilianza toka zamani ni jambo la kawaida na ndio mzunguuko wako ulivyo. Mzunguuko hauna mahusiano ya moja kwa moja na kuishiwa kwa mayai (kuingia mapema menopause).

Hivyo bado una nafasi kama mwanamke wa kawaida katika chances za kupata ujauzito. Cha muhimu zingatia lishe na tabia za kukufanya uwe na afya njema muda wote
 
Mi naona uvivu kutoa maelezo mengi ila kiufupi hauna tatizo sema una mzunguko mfupi. Kuna mzunguko wa siku 15, 24, 28, 30, 35 mpk 45. Kwhy wote walio na mizunguko mifupi huingia hedhi mara mbili kwa mwezi.

Kiufupi ndio hivyo tu dada, somo la hedhi ni refu sana jaribu kugoogle utapata materials tofauti tofauti na utelewa vzizuri
Lakini pia usiache kwenda hosp kwa maelezo zaidi.

Hili somo nakumbuka wakati sie tunafundishwa kazini ilituchukua siku tatu nzima.
 
Habari zenu waungwana? Mimi ni mschana wa miaka 23. huwa napata hedhi mara mbili ndani ya mwezi mmoja yaani ni hivi mwezi huu wa kwanza nilipata hedhi tarehe 4 ikaisha Siku 5...
usijali ata mie nna mzunguko kama wako haina shida huo ni mzunguko mfupi wengine wana mzunguko mrefu,na mimba inapatikana vizur tu
 
Back
Top Bottom