bo adams
JF-Expert Member
- Apr 11, 2016
- 213
- 351
Kwanza nikushauri mnapokuwa mmezaliwa wengi katika familia usijiweke mbele mbele kwa kila jambo linalohusu familia kwani mzigo wote utakuelemea wewe japo una malengo na mipango mizuri katika familia, mfano michango ya harusi, vikao vya usuluhishi, kusomesha wana ndugu, gharama za vyakula, malazi na matibabu hospitalini kila jambo litakuelemea wewe na hata mzigo wa lawama pia utakuangukia mara kwa mara kuonekana wewe ndio chanzo japo ulikuwa na lengo zuri na moyo wa dhati kuikwamua familia yako ktk matatizo/majanga.
Tunatambua kwamba unawapenda sana wazazi wako na ni baraka kwako kwani Mungu anatambua kuumia kwako na malengo ya kuwasaidia wazazi wako wawili. Maamuzi hayo yarudishe kwenye familia ili mpate kujadili pamoja na ndugu huenda kukapatikana wepesi zaidi (Mfano kuna watakao jitolea kuchangia pesa, ushirikiano wa nguvu, mawazo kwenye kiwanja cha fidia cha wazazi au hata mmoja katika ndugu akajitolea kukaa nao wazazi nyumba moja), huenda baadhi ya ndugu zako wanaumia zaidi kuliko wewe ila bado hamjakaa pamoja kujua mnalitatua vp tatizo hilo kwa mapana.
Inabidi uwe na longterm plan, kutokana na wewe shughuli zako na maisha yako sasa hivi yapo dar basi kwa baadae utakapokuwa na nafasi nzuri ya kuwasaidia wazazi wako hata katika uzee/maradhi au utulivu.
Jenga huku huku dar na uvumilie kwa muda kukaa kwao kwenye nyumba ya kupanga (nyumba ya kupanga na kulipa kodi sio aibu),watu wengi na hata matajiri walikaa nyumba za kupanga kabla hawajajenga nyumba zao.
Ukijenga mkoani utawasaidia wazazi pekee, ukijenga dar utajisaidia wewe, familia yako na wazazi wako kwa pamoja na shughuli zako zitaendelea bila kuathirika kiuchumi wala kisaikolojia