Nani zaidi kati ya Hamie Rajab, Eddie Ganzel, Elvis Musiba, Ben Mtobwa?

Posta maeneo gani mkuu...? Nielekeze kama inawezekana

0404
Nenda posta,shuka usawa wa sanamu ya askari acha hiyo njia ielekeayo NBC headquarter wewe panda njia kama unaenda LAPF ila usifike huko.utapita kwa wachonga mihuri na watengeneza picha za marais na vinyago mkono wa kulia.hapo hapo utakuwa umefika.Duka linaitwa TPH Bookshop mkono wa kulia.Ukiona mbali sana huko,hapo hapo posta kuna duka lingine linaitwa Dar es salaam bookshop nadhani utapata.Mimi si mwenyeji sana ningekutajia jina la barabara ila nimenunua sana vitabu vyangu hapo kama kuna mwenye kunisaidia kunyosha Maelezo anaweza kufanya hivo.
 
Kikomo,Elungata,Musiba katika ubora wake!Ni kweli kuna vitabu vingi vizuri ambavyo sikumbuki watunzi,vutabu kama kaburi bila msalaba,operesheni vipusa,nteko vano maputo,rosa mistika,nk,ila musiba nimemvulia kofia
 
Kama kuna kitu kinakosekana katika taasisi zote za kiswahili ni kushindwa kuwaenzi waandishi mahiri kabisa waliotikisa viunga vya Afrika Mashariki kwa masimulizi yenye kuchetua nyoyo za wasomaji.

Hebu tukumbushane ni nani zaidi kwako, kati ya waandishi uliowahi kusoma vitabu vyao, ambao masimulizi yao yameacha athari ktk kumbukumbu zako.

Je, ni Shabani Robert? Marehem Bawji? JoHn Kaduma? Taja mwandishi yoyote na na kitabu chake au hadith yake, maana kuna baadhi ya waandishi walikuwa wanatoa hadithi zao ktk magazeti.

MKUU
UNAPOTAJA WAANDISHI NGULI KATIKA FASIHI NCHI HII
NI LAZIMA UANZE NA #MAN_FONGO.
 
Ki ukweli kama kuna mtu aliyewahi kusoma vitabu vya hadithi/riwaya za kibongo mimi ni mkali. Nakumbuka miaka ile ya 80 tulikuwa tunaenda pole moshi library tukiwa vijana wadogo tunasoma vitabu. Nimesoma vitabu vingi jamani. Ingekuwa kusoma riwaya ndio unapata cheti basi sijui ningepewa cheti cha aina gani.!
 
Ki ukweli kama kuna mtu aliyewahi kusoma vitabu vya hadithi/riwaya za kibongo mimi ni mkali. Nakumbuka miaka ile ya 80 tulikuwa tunaenda pole moshi library tukiwa vijana wadogo tunasoma vitabu. Nimesoma vitabu vingi jamani. Ingekuwa kusoma riwaya ndio unapata cheti basi sijui ningepewa cheti cha aina gani.!
mkuu huna mabaki ya vitabu huko nyumbani?
 
Mwacheni alie'. Bibi Kizee mmoja alishauri 'Machozi ndio njia pekee imalizayo huzuni ya mwanamke'.... Namsoma Ben R Mtobwa katika ubora wake. Kitabu cha PESA ZAKO ZINANUKA. Rest in peace my role model.
Pesa zako zinanuka hatari mkuu,waandishi hakuna siku hizi
 
Dar es salaam usiku among the books I always like red more
Mara chache kukuta tunazungumzia vitabu vya waandishi wa siku hizi hii inadhiirisha tuna tatizo ktk sanaa hii kwa kizazi hiki,waandishi ni wachache na kazi hazieleweki
 
Back
Top Bottom