Nape si mwanaCCM tena (amekuwa) almost four years ago, kipindi kile cha CCJ na CCK. RIP Mzee Sitta.
Hata ndani ya CCM ilijulikana hivyo ila busara na hekima za Kikwete zilimbakisha chamani. By then alikuwa ndio mmojawapo wa vijana waliokuwa wanategemewa sana ndani ya chama.
Wakati si milele, enzi ya Kikwete ikapita Salama. Uchapakazi wa Nape kama Katibu mwenezi Kitengo cha propaganda unaonekana wazi, akalipwa fadhila ya ubunge na hatimaye uwaziri.
Huyu ni Nape katika ulimwengu wa siasa za chama tawala! Lakini Kiuhalisia na kutoka rohoni mwake kama ikitokea nafasi nyingine huru Nape Nnauye is no longer CCM. Na kwa taarifa yako hayuko peke yake. Mwigulu, Makamba Jr, Kigwangala (wenye tuhuma za kughushi majina), Bashe na vijana wengi ndani ya CCM hawako happy na utawala wa sasa.
Kuna kitu hawakubaliani nacho asilani hata kama hawaongei kwa sauti kwa kuhofia kutumbuliwa, lakini iko hivi "Hawapendezwi na SPECIAL CARE anayopewa RC wa Dar mwenye tuhuma nyingi ikiwemo za kupora mali Kisha kusingizia madawa, kughushi cheti na matumizi mabaya ya madaraka.
Wanajiuliza kwani yeye ni nani hadi abwebwe na mbeleko kubwa kiasi hiki wakati wao ndio walifanikisha kwa sehemu kubwa mkulu Bob kuwa madarakani? Kama ni ishu ya Ben mbona hata wao wangeweza kuifanya? Wanajiuliza What is so special wit dis guy kwa mkulu?
Kwahiyo inapotokea nafasi kama hii ya kuongea, hawa waliotengwa wanajaribu kuonyesha hisia zao japo kwa woga mkubwa. Between they have already a plan B or I can say back up If ever things fall apart...
.
Just thinking aloud... But namuona Nape Nnauye and the rest kwenye gwanda ......!!!!the soonest....!!!!!!!!!!!