Namshangaa mwanasiasa/Kaisari anayesema atagawa chakula leo

Viongozi wa dini nawaelewa maana hata Yesu aliposema "naona kiu" hakuwa amemaanisha kiu ya maji.Sasa nyie wapinzani mnazungumzia "njaa" gani ambayo ninyi mnaiona lakini wenzenu wa CCM hawaioni?!
 
Sakata la njaa linaloikumba baadhi ya maeneo nchini linaendelea kuonesha taswira halisi ya maigizo yanayoendelea kufanywa na Lowassa na chama chake, Chadema. Mbali na wao(chadema) kuzusha,kukuza pamoja na kuilazimisha Agenda ya njaa kuwa ya kitaifa na janga la nchi nzima pamoja na kwenda mbali zaidi kumlazimisha Rais kutangaza njaa kama janga la kitaifa kinyume na hali halisi ilivyo nchini kwani katika maghala ya taifa kuna zaidi ya tani milioni 20 nchi nzima, katika maghala ya wakulima nchi nzima kuna zaidi ya tani milioni 8 nchi nzima, pia wakulima wengi wamehifadhi vyakula vya kula zaid ya miezi 8 ijayo.

SARAKASI ZA LOWASSA NA CHADEMA

Jana Lowassa amesema kuwa yeye na chama chake(chadema) wamejipanga kuwaletea watanzania chakula hata kwa kuomba nje ya nchi maana wanaamin mataifa yatawasikia, hakika haya ni maajabu ya Abunuasi. Kwa mujibu wa sheria za nchi mtu pekee anaweza kutangaza njaa nchini ni Rais wa nchi na ndiye mwenye jukumu la kuomba chakula kwa mataifa mengine kwa mujibu wa sheria za kimataifa. Anyway nikikumbuka mwaka 2006 Lowassa jinsi alivyoomba mabilioni ya fedha ili akanunue mvua Malaysia, huwaga sipendagi ujinga na huyu mzee.

MAMBO YA KUZINGATIA.

• Hakuna serikali yoyote katika nchi za kidemokrasia dunian inayoweza kuwaacha watu wake wafe kwa njaa.
• Serikali ya JPM haijakataa kugawa chakula kwa wenye mahitaji ila alisitisha kugawa chakula meneo ambayo hali ya hewa ni shwari.
• Wakulima wengi huweka akiba ya chakula toka katika mavuno yao kwa ajili ya kula kipini cha kulima,kupanda na kuvuna yaani kuanzia septemba mpaka April, je hii njaa ya katika kipindi hiki cha kupalilia mazao inatoka wapi??,,
• Chombo pekee chenye mamlaka ya kutangaza ukame nchini ni Mamlaka ya hali ya hewa (TMA) kazi ya taasisi za dini kama BAKWATA na TEC ni kuliombea taifa liepukane na majanga ila sio kutangaza ukame.
• Chadema,Act waache tabia za uzushi na uongo bali wajikite katika kuwahamasisha wananchi kupiga kazi kwa maslahi mapana ya taifa letu.
• Uongo na Uzushi wa vyama vya upinzani umeviweka taifa katika hali ya taharuki na kusabibisha kupanda kwa bei ya vyakula nchini

Vyama vya siasa hasa vya upinzani viaache kujijenga kwa misingi ya propaganda, huu ni wakati wa kujenga nchi yetu pamoja, vyama vya siasa vifanyekazi ya kuwahamasisha wananchi kufanya kazi ikiwa pamoja na kuwapa mafunzo mahsusi ya kujiinua kiuchumi. Uongo na uzushi hautufai
[HASHTAG]#lowassakatununuliemvua[/HASHTAG]
 
Yusufu(Mtu wa Mungu) alitoa maono ya njaa. Kaisali/Mwanasiasa(Farao enzi hizo) akaagiza kujengwa maghala yenye uwezo wa kutunza chakula miaka saba wakati Misri nzima itakapokumbwa na njaa.

Binafsi sijaiona njaa Tanzania ila nikipita mabarabarani ninaiona ardhi sehemu kubwa ikiwa na Mazao Dhaifu.Upungufu wa chakula baadhi ya maeneo sio habari maana ni toka uhuru na Yawezekana tukaja na njia mpya sio ileile ya kila siku kugawa chakula.

Kazi ya Kaisali sio Kugawa Chakula wakati njaa halisi haijafika au Kumuomba Mungu Mvua Inyeshe, Bali ni kuleta mipango yenye uhalisia jinsi ya kukabiliana na Njaa ijayo kama kweli ipo.

Ninawashangaa wote wanaoshabikia kauli ya kugawa chakula kama kilele cha ubunifu wa Mwanasiasa.
Watanzania wakifa Kwa njaa Dhambi hii mtatubu wapi au ndio sikio la kufa. Hadi mkuu wa Wilaya analia bado kuamini tu?
 
Naunga mkono hoja. Ukigawa chakula akienda chooni kimekwisha atataka kupewa kingine.
We need longterm plan & permanently solution. Tupunguze mihemko na Mahaba Niue.
Unapoambiwa lisha masikini na wasiojiweza,kwani mungu hakujua kuwa "wanakunya",mwenye roho mbaya hawezi kuwa muumini wa dini yeyote ya mungu.,wewe na mtoa mada ni wauaji kwa kauli zenu tu.
 
Hawa wanaolilia kutoa leo walikuwa wakitoa pesa makanisani na misikitini kwa watu walioshiba. Kaisali kumtumia raia kama ngazi ya mafanikio ya kisiasa ndio dharau ya kukemewa.
Mwanasiasa wa Kweli anapaswa kuona mbali zaidi ya Kugawa chakula. Matatizo ya taifa hili hayatatatuliwa kwa kuwapa watu SAMAKI bali NDOANO. Maoni yangu
Mtu ana njaa Kwa kukosa mavuno. Unataka ugawe mbegu( ndoano) apande Kwa mvua ipi? Na hata akipanda atavuna baada ya miezi 3. Hata wiki haitafika huyo mtu anakufa. Chakula ndiyo njia ya haraka ya kumsaidia aliyepata janga la njaa ili azidi kuishi. Chakula hakitolewi kum sustain mhitaji ila kumtoa ktk kipindi kigumu hadi hali ya hewa itakapo kuwa nzuri
 
Naunga mkono hoja. Ukigawa chakula akienda chooni kimekwisha atataka kupewa kingine.
We need longterm plan & permanently solution. Tupunguze mihemko na Mahaba Niue.
Kwanza unaitwa CANNIBAL-MTU MLA WATU.
STPD.
 
Kama unaamini naishi kwa dada, sikushangai kukusikia ukisema tanzania kuna njaa kwa kutumia picha ya shamba la eka mbili tatu au kutupia picha mbili tatu za mizoga ya ng'ombe. Lakini tuushahidi mnatotupia hatujathibitika kama ni currently au ni past.
Punguzeni MAHABA NIUE NA KUSHADADIA KILA KITU. REALLY MNABOA KWA KUENDEKEZA UZALENDO KIBARAKA.
Wewe ni mtoto wa nyoka na tunajua pia ni nyoka
 
Mtu ana njaa Kwa kukosa mavuno. Unataka ugawe mbegu( ndoano) apande Kwa mvua ipi? Na hata akipanda atavuna baada ya miezi 3. Hata wiki haitafika huyo mtu anakufa. Chakula ndiyo njia ya haraka ya kumsaidia aliyepata janga la njaa ili azidi kuishi. Chakula hakitolewi kum sustain mhitaji ila kumtoa ktk kipindi kigumu hadi hali ya hewa itakapo kuwa nzuri
Shinyanga mfano ndio mkoa pekee ambao hata inyeshe mvua nchi nzima wao wataomba chakula. Lkn katika lisala yao kwa Rais waliomba mbegu za mtama washushiwe bei ili wapande waje wale baadae njaa halisi ikifika sio hii ambayo vyanzo halisi havijatueleza kama ni janga la Kitaifa.
Mkuu tofautisha janga la njaa na tishio la njaa
 
Yusufu(Mtu wa Mungu) alitoa maono ya njaa. Kaisali/Mwanasiasa(Farao enzi hizo) akaagiza kujengwa maghala yenye uwezo wa kutunza chakula miaka saba wakati Misri nzima itakapokumbwa na njaa.

Binafsi sijaiona njaa Tanzania ila nikipita mabarabarani ninaiona ardhi sehemu kubwa ikiwa na Mazao Dhaifu.Upungufu wa chakula baadhi ya maeneo sio habari maana ni toka uhuru na Yawezekana tukaja na njia mpya sio ileile ya kila siku kugawa chakula.

Kazi ya Kaisali sio Kugawa Chakula wakati njaa halisi haijafika au Kumuomba Mungu Mvua Inyeshe, Bali ni kuleta mipango yenye uhalisia jinsi ya kukabiliana na Njaa ijayo kama kweli ipo.

Ninawashangaa wote wanaoshabikia kauli ya kugawa chakula kama kilele cha ubunifu wa Mwanasiasa.

Huo ni utoto, hivi huamini kwamba kuna watu hawana chakula kabisa? acha kushabikia siasa za kitoto. kukosa chakula unakotaka ni pale ikula watakapoanza kulala njaa? hiyo haitatokea kamwe
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom