Namna ya Kupinga Hukumu Iliyotokana na Makubaliano yenu wenyewe (Proper Procedure to Set Aside a Consent Judgment)

Apr 26, 2022
82
121
Procedures, how to challenge consent judgment (namna ya kupinga hukumu iliyotokana na makubaliano yenu wenyewe)

Kama ilivyofafanuliwa na Mahakama kwenye kesi ya “Arusha Planters & Traders Ltd and two others v Euro African Bank (T) Ltd”.

Ikiwa mnadaiana, mkaenda mpaka Mahakamani, mkaomba kesi isimame ili mkakubaliane jinsi ya kulipana nje ya Mahakama, na Mahakama ikaandika hukumu kutokana na makubaliano yenu wenyewe. (CONSENT JUDGEMENT)

Je, baadaye unaweza ukaruka na ku challenge (kupinga) hiyo hukumu (consent judgement)? Utapinga kwa njia ipi na utatoa sababu gani?

Kwenye hii kesi kulikua na marumbano (issues) kadhaa:

{i} Wengine wanasema, utaiomba Mahakama ile ile kutengua hiyo hukumu mliyokubaliana (ku set aside consent judgement)

{ii} Wengine wanasema utakata rufaa Mahakama ya Rufaa kwa ruhusa ya Mahakama Kuu (you lodge an appeal with leave of the High Court).

{iii} Wengine, kuomba marejeo kwenye Mahakama ile ile (to apply for a review) na

{iv} Au Kufungua kesi nyingine upya (by instituting another suit).

-Hii Kesi inakujibu. Ni kesi ya Arusha Planters and Traders Ltd and two others v Euro African Bank (T) Ltd, Civil Appeal no. 78 iliyoamuliwa na Mahakama ya Rufaa Tanzania mwaka 2001.

FACTS (STORI YA KESI)

-Mwaka 1998, Benki (Euro African Bank) iliwashtaki, Arusha Planters and Traders Ltd, Jayant Narshbhai Patel na Rozina Jayant Patel katika Mahakama Kuu, ikidai walipe deni la mkopo waliopewa.

-Wakati wanaendelea na kesi, wakakubaliana kesi iahirishwe ili wakaandae makubaliano (consent judgement) ya jinsi ya kulipana nje ya Mahakama.*

-Baadae, mwaka 2001 Benki ikafungua tena kesi kwenye Mahakama Kuu kitengo cha Biashara, ikidai mambo yafuatayo.

-Tamko la Mahakama kwamba hayo makubaliano ni batili (deed of settlement is null and void) kwa hiyo yafutwe. kwa sababu kwamba, Benki walishawishiwa kuingia hayo makubaliano kwa lazima (by coercion), ushawishi wa mazingira (duress) na kupitia matumizi mabaya ya nafasi au cheo (undue influence), na

-Pia wakaomba Mahakama ikubali ile kesi ya mwanzo ya mwaka 1998 iendelee pale ilipoishia.

-Washtakiwa wakaweka pingamizi kwamba:

-Benki imekosea kufungua kesi nyingine na inatumia vibaya mfumo wa Mahakama.

-Kwamba Mahakama haina mamlaka ya kutathmini upya makubaliano ambayo yalishapitishwa na Mahakama kwa ridhaa ya walioshtakiana wenyewe.

-Na kwamba, Mahakama haiwezi kukaa kusikiliza tena, kufuta au kubadilisha kwa vyovyote vile, maamuzi yake yenyewe kupitia kesi nyingine.

UAMUZI

-Mheshimiwa Jaji akasema, Mlalamikaji (Bank), alitakiwa aombe marejeo (review) kwenye Mahakama ile ile na mbele ya Jaji yule aliyerekodi makubaliano yao (consent settlement). Akarejea Order XLII rule 1(a)(b) ya Sheria ya Mwenendo wa Madai (Civil Procedure Code kwa kifupi CPC)

-Pia Mheshimiwa Jaji (Bwana J), akasema, kama akiamuru ile kesi nyingine iendelee kuanzia ilipoishia, atakuwa anamwamuru Jaji mwenzake (Katiti J), ambapo kwa mtazamo wake itakuwa sio sawa, kwa sababu wote ni Majaji wa Mahakama Kuu wenye mamlaka sawa.

-Mheshimiwa Jaji akaendelea kusema kwamba, kwa kuwa ile kesi nyingine iliahirishwa tu baada ya wanaoshtakiana kuomba wakapange namna ya kulipana, hivyo basi kesi hiyo bado ilikuwa iko pending (haijaisha), na katika mazingira hayo haikuwa sahihi kufungua kesi nyingine kwenye Kitengo kingine cha Mahakama ile ile Kuu.

-Pingamizi likapita.
-Kesi ikapigwa chini.

Mlalamikaji ambaye ni Benki, hakuridhika. Akakata rufaa kwenda Mahakama ya Rufaa akiwa na sababu zifuatazo;

1: Kwamba, Mheshimiwa Jaji alikosea kusema kwamba, consent judgement (hukumu inayotokana na makubaliano ya wanaoshtakiana wenyewe) ambayo ilifikiwa kwa udanganyifu (fraud), matumizi mabaya ya nafasi aliyo nayo mtu (undue influence) au kulazimishwa (coercion) inaweza kupingwa Mahakamani kwa kuomba marejeo tu (review) na sio kufungua kesi nyingine upya.

2: Kwamba, Mheshimiwa Jaji alikosea alipoamua kuwa, hukumu ikitolewa kulingana na makubaliano yenu, alafu baadae hao watu wakarudi Mahakamani ili kurekebisha namna ya kulipana, kwamba ile kesi nyingine inakuwa bado inasubiri (pending) au haijaisha kwa mujibu wa Order IV rule 3 ya CPC.

UAMUZI WA MAHAKAMA YA RUFAA

Kwanza, Mahakama ya Rufaa ikaona ni kweli, wanaoshtakiana kwenye hii kesi walisaini makubaliano (Deed of Settlement) ya kulipana deni.

-Na Mahakama Kuu ikawapa hukumu ikiwa imebeba walichokubaliana wenyewe. Kwa lugha nyingine hukumu ya maridhiano (consent judgement).

-Pia Mahakama ya Rufaa ikasema ni kweli, huwezi kukata rufaa kwenda Mahakama ya Rufaa kutokana na uamuzi uliotolewa na Mahakama Kuu kwa ridhaa yenu wenyewe (consent of the parties), isipokuwa tu kama una ruhusa (leave) ya Mahakama Kuu. Rejea section 5 (2)(a)(i) of the Appellate Jurisdiction Act, 1979.

-Lakini pia, ni sahihi kwamba hukumu ya maridhiano (a consent judgment) inaweza kupingwa Mahakamani kupitia review (marejeo).

-Swali linalobaki (issue) ni je, hukumu ya maridhiano inaweza pia kupingwa kwa kufungua kesi nyingine upya? (whether a consent judgment may also be challenged by way of instituting a separate suit)?

-Mahakama ya Rufaa ikasema, haijaona kifungu kwenye Sheria ya Mwenendo wa Madai (CPC) kinachoeleza wazi kwamba hukumu itokanayo na maridhiano ya watu wenyewe (a consent judgment) inaweza kupingwa (kuwa challenged) kwa kufungua kesi nyingine (by way of instituting a separate suit).

-Kwa India Sheria imesema inawezekana. Ukisoma Kitabu cha Mulla, mwandishi nguli wa sheria za madai kutoka India. (Mahakama ikamnukuu).

-Kenya pia inawezekana. Ukisoma kesi ya Wasike v Wamboko (1976-1985) EA 625.

-Lakini kwa Tanzania Sheria iko kimya. Hakuna kifungu cha CPC kinachoruhusu kupinga hukumu ya maridhiano (consent judgment) kwa kufungua kesi nyingine (by way of instituting a separate suit).

Sheria inachosema (CPC na the Appellate Jurisdiction Act 1979), ni kwamba hiyo hukumu ya makubaliano inaweza kupingwa kupitia kuomba marejeo (by way of a review) au kukata rufaa (or appeal) kwa ruhusa ya Mahakama Kuu (with leave of the High Court).

-Mwisho, baada ya kurejea vyanzo kutoka nchi zingine, Mahakama ya Rufaa ya Tanzania ikakubali kwamba, inawezekana kabisa kuipinga hukumu mliyokubaliana wenyewe (consent judgment) kwa kufungua kesi nyingine (by instituting a separate suit).

-Swali sasa ikawa je, kwa mazingira ya hii kesi, ilikuwa ni sahihi kufungua kesi nyingine?

-Kwenye hii kesi, mlalamikaji aliomba Mahakama ikubali ile kesi ya kwanza iliyofunguliwa mwaka 1998 iendelee kuanzia pale ilipoishia, kabla wanaoshtakiana walipokuwa hawajafikia makubaliano.

-Majaji wote wawili, Mheshimwa Dr. Bwana, J. (aliyesikiliza kesi ya pili) na Mheshimiwa Katiti, J. (aliyesikiliza ile kesi ya kwanza) walikuwa ni Majaji wa Mahakama Kuu, wenye mamlaka inayofanana.

-Mahakama ikasema kukubali hicho kitu haitakuwa ni utoaji haki mzuri.

-Hali kadhalika, kama Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara ingetengua hukumu ya maridhiano (consent settlement) iliyotolewa na Mahakama Kuu ya Kawaida kwa kusema ni batili, haitakuwa utoaji haki mzuri, kwa sababu itaonesha picha isiyo ya kweli kwamba Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara ina mamlaka ya kutengua maamuzi ya Mahakama Kuu ya Kawaida.

-Mahakama ya Rufaa ikasema kwamba, katika mazingira ya hii kesi, haikuwa sahihi kupinga hukumu inayotokana na makubaliano kwa kufungua kesi nyingine “(in the circumstances of the instant case, it was not proper to challenge the consent judgment by way of instituting a separate suit.”)

-Rufaa ikakataliwa. (Hiyo ilikuwa tarehe 21/12/2007)

------MWISHO------

Angalizo: Position au maelezo haya ni kwa mujibu wa kesi zilizokuwa zimeamuliwa mpaka siku ya kupost hili andiko. Hivyo unaposoma leo hii kesi soma na kesi zingine zilizopo sasa hivi, ili ujue utaratibu bado ni ule ule au la! Mimi sifahamu umesoma lini haya maelezo, lakini Sheria zinarekebishwa na mpya zinatungwa kila siku.

Disclaimer: Lengo la hii makala ni kutoa elimu kwa jamii. Huu sio ushauri wa kisheria kwa mtu yeyote. Ikiwa utaamua kufungua kesi kwa kufata haya maelezo na ukapata hasara, mwandishi wa maelezo haya hatawajibika kwa vyovyote vile. Kama unahitaji ushauri wa kisheria wasiliana na Mawakili.

Pia natoa angalizo, wale wazee wa kukopi machapisho ya watu na kuweka majina yenu. Ni kosa kisheria. Hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayejimilikisha andiko hili. Unaruhusiwa tu kushare lakini usibadili yaliyomo. Ni heri uanze kuandika ya kwako mpya.

Tafsiri hii ya Kesi imeandaliwa na kuletwa kwako nami Zakaria
(0754575246 WhatsApp).
zakariamaseke@gmail.com
 
Back
Top Bottom