Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,500
- 3,698
Waziri kiongozi mstaafu wa Zanzibar ambaye alihudumu kuanzia mwaka 2000 – 2010, Shamsi Vuai Nahodha amechukua fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea urais Zanzibar kwa tiketi ya CCM mapema leo asubuhi katika ofisi kuu ya CCM Zanzibar Kisiwandui.
WASIFU
Shamsi Vuai Nahodha alizaliwa 20/11/1962 na kupata elimu yake katika Skuli ya Msingi Kiongoni huko Makunduchi na kuendelea Sekondari katika Skuli ya Benbella na kisha kufanikiwa kujiunga katika Taasisi ya Kiswahili na Lugha za Kigeni. Ana Shahada ya kwanza aliyoipata Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika fani ya elimu na pia stashahada aliyoipata katika Chuo cha Diplomasia hapo Dar.
Huko mitaani hujulikana kama mtoto wa mkulima na mkwezi alizaliwa shamba Makunduchi Wilaya ya Kusini, Mkoa wa Kusini Unguja.
Nahodha ni msomi wa Chuo Kikuu mwenye shahada, mtaalamu wa lugha, mwanadiplomasia, mwandishi, mwenye kipaji na mwerevu. Historia yake haioneshi kuwa na dhamana yoyote kubwa kabla ya kujitosa katika siasa na kugombania uwakilishi katika jimbo lake na kuibuka mshindi. Kilichobakia baada ya hapo ni historia kwani nyota yake ghafla ilipaa kutoka Ofisa Habari katika Wizara ya Habari mpaka Waziri kiongozi
Katika mwaka 2000 akiwa na umri wa miaka 38 tu, alikabidhiwa moja ya vyeo vya juu kabisa katika nchi ya Zanzibar kwa kuteuliwa na Rais wa wakati huo Aman Abeid Karume kuwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.