Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,679
- 149,866
Kama kweli serikali itaamua kufuta posho za watumishi wa umaa na kudhibiti baadhi ya Taasisi za serikali zilizokuwa na mamlaka ya kujipangia mishahara na posho kupitia bodi za mashirika hayo,eneo mojawapo litakaloathirika sana na uamuzi huu ni uuzaji wa bia na aina nyingine ya vilevi katika mabaa,grocery,n.k pamoja na kampuni zinazojihusisha na utengenezaji na usambazaji wa vinywaji hivi.
Baada ya serikali kuzuia safari za watumishi,semina,washa,mikutano na makongamano,watu wengi uwezo wao kununua vinywaji(pombe) ulipungua na uhudhuriaji katika mabaa mbalimbali ulishuka na wengi walimudu kwenda bar tarehe za mwisho wa mwezi tofauti na walivyokuwa wamezoea hapo awali.
Ni ukweli kuwa baada ya vikao vya kuhudhuria semina,washa,makongamano,mikutano,n.k mida ya jioni watumishi hawa huhamia kwenye mabaa kunywa wakitumia posho za vikao na perdiem zao.
Kwa wale wanaopata posho za kila mwezi nao hali ni hivyo hivyo kwani kila wakipata posho yao baadhi huenda bar na ku-spend maisha yaende ila na hawa sasa posho yao ndio hiyo hatujui kama itaendelea kutolewa au laa kwa mujibu wa marekebisho ambayo serikali inakusudia kuyafanya.
Hivyo basi,kama posho katika hizi Taasisi ambazo watumishi wake bado wanapokea zitasitishwa, Mashirika na Taasi ambazo zilizokuwa na mamlaka ya kujipangia bajeti zake na kujiendesha zenyewe bila kuingiliwa na serikali nazo zitanyang'anywa mamlaka hayo na hivyo kulazimika kupunguza safari na posho za watumishi wake,n.k,sioni ni wangapi watakaomudu kuendelea kwenda bar na kuagiza vinywaji zaidi ya kusubiri mwisho wa mwezi na hapa itategemea na madeni aliyonayo mtaani na kwenye salary slip yake(kama alikopa benki,n.k).
Posho hizi ndio zilikuwa zinasaidia watumishi kufukia mashimo(madeni ya mabenki,saccos,n.k)na kuwawezesha watumishi hawa kuhudhuria bar ila sasa ndio hizo nazo taratibu zinaota mbawa.
Uamuzi wa serikali wa kutoongeza mishahara,kuzuia safari ,mikutano, washa,makongamano,n.k na sasa kutaka kufuta hata baadhi ya posho zilizopo kisheria katika baadhi ya mashirika na Taasisi za umma, utakwenda kuathiri mapato ya makampuni ya bia na mwisho wa siku serikali nayo itaathirika kwa kukosa mapato yatakonayo na kodi ya kuuza vinywaji hivi.
Kama kweli sekta binafsi zinayumba kama tunavyosikia,serikalini nako tight,wafanyabiashara nao lazima wayumbe kwasababu watumishi hawa ndio wataje wao.
Sasa kama mtumishi wa umaa amebanwa,wa sekta binafsi nae hana kitu au amekuwa jobless na mfanyabiashara nae kipato chake kimeshuka,sioni uwezekano wa biashara ya vinywaji kuongezeka zaidi ya kupungua na kupelekea serikali kukosa mapato.
Aliezoea kunywa bia 5 sasa atalazimika kunywa bia 2 ama kuacha kabisa tofauti na mahitaji mengine ya nyumbani ambayo ni ya lazima(sio anasa).
Hii itakuwa ni moja ya athari ya kubana watumishi ambayo kwa sasa inaweza isionekane ila ni swala la muda tu kabla madhara yake hayajaanza kuonekana.
Pamoja na yote hayo,msisahau na sheria ya kuzuia watu kunywa pombe kabla ya saa 10 jioni, sheria ambayo imeanza kutekelezwa katika awamu hii ili watu wafanye kazi.
Lingine la kuzingati ni ukweli kuwa watu wengi huwa hawaendi baa peke yao bali hufuatana na ama mke,mchumba,kimada,rafiki,ndugu,jamaa n.k, hivyo kipato cha mtu mmoja tu kina mchango mkubwa sana katika biashara hii ya vilevi kuliko tunavyofikiri.