Nakoshwa na uongozi uliotukuku wa awamu hii, naiona nuru ya Mungu kwenye nchi yetu. Asante Mungu, asante Rais wetu Samia

Frustration

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
3,123
4,113
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungana wa Tanzania, Kwanza napenda kumshukuru mwenyeezi Mungu ambaye ni mwingi wa Rehema(kiimani itifaki imezingatiwa). Pia napenda binafsi kumshuru Mungu kwa kuuona mwaka wa 2022 kwani kiimani sio kwa uwezo wangu bali ni kwa rehema zake.

Hili ni bandiko langu mahsusi la kuguswa na uongozi wa awamu ya 6 kama vile wengi tunavyoita. Najua sio dhambi kupandisha mada za kukosoa na kupondea utawala huu wa mama Samia, ila sio vizuri pia kutosema yale mazuri au zuri likifanywa na rais wetu.

Wembe uleule unaotumiwa kunyolea kwa kuonyesha kasoro na tena hadi chuki kwa baadhi nautumia hapa leo kunyolea kwa kuonyesha namna nilivyoguswa au kukoshwa na style ya Rais Samia Saluhu Hasani.

Baada ya kusema hayo naomba ku-declare my interest ya kuwa mimi ni CCM na kwa kweli nakipenda sana chama changu hadi mda huu.

Napenda kuwakumbusha watu wote humu juu ya utwala uliopita namna mambo yalivyokuwa ilifikia mahala watu waliamini Jamiiforums ni jukwaa la CHADEMA kwa kuwa serikali ile ilikuwa haiishiwi na maovu. Uchafu uliokuwa ukitendwa ulikuwa unaanikwa humu jf kwa kuwa vyombo vya habari kama radio na tv ilikuwa marufuku kuchapisha uchafu wa serikali.

Nayasema haya sio kwa ubaya au kutoipenda awamu ya tano na kiongozi wake,la hashaa! Nayasema haya ili kuwakumbusha tunakotoka,tuliko na hata tunakoenda.

Wizara zote zilikuwa simesimama kusubili rais atasema nini, kiongozi anasimama mbele ya wana nchi na kuwauliza kwa mihemko na kwa sifa "Nimtumbueee au nisimtumbueeeeee!" Watulizikwa kwa pressure kwa kuachishwa kazi bila ya kufuata masharti na kanunu za ajira na kazi.

Kwenye elimu usipime wakurugenzi na maafisa elimu wanajua hali ilikuwaje, yani Afisa elimu wilaya anaita TAHOSA wilay na kuwaambia. Tunaelekea kwenye mtihani tuhakikishe wilaya yetu haiwi ya mwisho, mm nakipenda kitumbua changu. OCD na afisa elimu wanatembea kwenye gari moja kukagua usimamizi wa mitihani na kuruhusu kuvuja kwa mitihani.

Ninapowaza tuliko toka na tulipo hakika yamkini Mungu ameshusha neema katika nchi yetu. Ni vile tu binadamu hana shukrani au mwepesi sana wa kusahau madhira ya nyuma. Najivunia kuishi katika ukweli.

Japo sio nabii ila kwa kitendo cha rais Samia kudhamilia kukamilisha miradi yote ya awamu ya 5 ni wazi mama ni jibu la maombi ya Watanzania kwa miaka mingi. Hii haijawahi kutokea kwani kila rais alikuja na madudu yake na aliiacha na ikaitwa white elephant projects yaani eti miradi hewa. Nimeita madudu kwa sababu haikukamilika na hela zilienda.

Rais Samia anakamilisha miradi yote kuanzia Nyerere,Mkapa,Kikwete na hadi Magufuri. Badari ya Bagamoyo ilibwagwa,gas ya mtwara ni kama ilitelekezwa,SGR,bwawa la Nyerere na bado anamiladi yake yeye mwenyewe. Narudia tena rais Samia ni mzarendo haswaa na sio porojo she is composed. Huyu ndiye rais wa kuombewa na huyu ndiye rais wa kuongezewa ulinzi sema tu basi hana malingo wala majivuno.

Naendelea kutoa pongezi na sifa kwa rais wetu, kwani kitendo cha kutomfumbia macho aliyekuwa spika wa bunge bwana Ndugai inadhihirisha mama anaenda kukomesha unafiki ndani ya serikali na chama chetu. Ile ni message tosha kuwa yeye ni rais na haogopi,,hatishwi wala halei majambazi hiyo yote inatokana na kujiamini kwake katika utendaji wa kazi. Hii haihawahi kutokea kwa karibuni hii.

Mama amefungua mipaka yote,upinzani upo huru,wakenya wapo Tanzania na watanzania wapo Kenya. Ama sio tu Mzaramo anauza wali Unguja au Mpemba anauza duka kariakoaa bali Mpemba ameoa mngoni na mmasai ameolewa Pemba huku mmang'ati anamifugo Unguja. Muungano umeimalika na dosari zimeondolewa za muungano.

Sijajua sababu ya kutoyaona mazuri haya yote na watu wakakimbilia kwenye Korona na Mbowe tu, yeye ni binadamu hawezi fanya yote kwa mda mmoja. Yeye ndiye atakaeiweka katiba ya wananchi katika nchi yetu na hili halina mda.
OMBI KWA WATU WOTE.

Kwanza naomba mama aheshimiwe lakini pia vilevile athaminiwe kwa kazi ngumu anayopitia ukijumlisha na changamoto ya viongozi wake wengi.. Pia mawazo yake ya kutaka kugombea 2025 isiwe sababu ya kuchukiwa au kupondwa au kumharibia kwa kola anachofanya. Ni mwanamke wa aina yake huyu hakika yeye ni Mpango wa Mungu hao wengine walipita kwa wizi wa kura tu au mmesahau?

Ninaposema Samia ni mpango wa Mungu wa kweli ninamaanisha iliyo kweli. Nitamuunga mkono 2025 na nawaomba wana CCM wenzangu tushikame tuwe letu moja. Kila mtu atakuwa rais hata mm nautaka ila nyakati hizi ni za Samia.
Ahsanteni sana na pole kwa mwandiko mbaya hasa mpangilio lakini pia vilevile mada ndefu.

Alisema nasimama na wananchi na sisi tunasimama na rais wetu.
 
Na sema hivi uchumi bado haujaka sawa na utawala wa sheria bado, ila Mama ni bora kuliko Magu, tuna amani hatuishi kwa hofu.
Umebarikiwa sana kwa kuliona hili, hawa chawa wachache wa kule kwa kasimu hawawezi ona hili. Nimeweka wazi, mm nimeangalia tulikotoka,tulipo na tunakoenda naona mabadiliko makubwa sana kwanza mengi yametokea ya kujifunza. Chuki na wivu walio nao wengi hawawezi ona mwanga aliouleta Samia. Leo na jana ni tofauti sana hivyo kesho tutafurahi wenyewe
 
Uadui huwo mnaouforce kwa Samia hauna faida na hakuna wa kumzuia Samia kwa sababu yeye ni Mamlaka kamili.
Aliyekwambia kuwa Samia anapingwa ni yupi?

Samia mwenyewe kasema adui zake ni ccm wenzake inakuwaje wewe mramba miguu umpangie cha kuongea?
 
Back
Top Bottom