mimiamadiwenani
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 5,637
- 7,575
Anyaashimika!
Kwa kweli acha leo niwe muwazi tu, niwe muwazi tu (katika sauti ya Gwajima).
Zaidi ya 95% za mafanikio niliyopata mpaka muda huu ni kutokana na kuwa karibu na mzee wangu. Kumsikiliza mzee wangu na mawaidha yake kumenifikisha hapa.
Zile "pita huku, usipite kule", "fanya hiki huku ukisubiri kile" nk, zimenipa matunda bora maishani.
Alinichana ukweli siku moja akiniambia nisiwe kama yeye (alijiingiza kwenye masuala ya malezi na familia mapema kabla hajajipanga). Na nilifuata hili, na nitawafunza wanangu pia.
Kwa kweli wazee wetu wana madini mno, tuishi nao vizuri tu. Sasa yale mafanikio aliyoyakosa mzee kwa kosa alilofanya (tajwa hapo juu), nimeyapata mimi mwanawe. Mbuzi wa Bwana Heri, kala mahindi ya Bwana Heri, hakuna kesi.
Ndugu zangu wengi walikuwa wakimbeza na kumuogopa sana kwa ukali wake, mimi kwenye huo ukali niliiona future yangu njema maishani, niling'ang'ana kuwa naye karibu hivyo hivyo ili nimvune mzee wangu. Nilifanikiwa.
Baadhi ya watoto wa ndugu na kaka zangu wakubwa walikuwa wakidharau mausia yake wakisema ni amezeeka hivyo akiongeacho hakitakiwi kutiliwa maanani sana.
Ila mimi sikuachilia hata neno lake moja lianguke pasipo kulitimiza kwa wakati, niliheshimu kila alichonieleza. Sikuangalia ni mzee sana au la. Nimepata faida na naiona sasa.
Shout out kwa mzee wangu sana. Naona ule ukali wake umeniletea faida. Ukali wa mzee wangu haukunifanya nisitake kuwa naye karibu.
NB, namu appreciate mama yangu pia, ana mchango mkubwa maishani mwangu.
Tuishi vema na wazee wetu, tusiwe wakaidi wa mawaidha yao, tutajua mengi.