chinchilla coat
JF-Expert Member
- May 16, 2016
- 5,107
- 10,968
Naibu spika wa Tanzania amelifanyia kazi malalamiko ya mbunge wa Ulanga Goodluck Mlinga wa CCM kuvuliwa balaghashia na mbunge Anatropia Theonest wa CHADEMA na kumsababishia mfadhaiko na mtikisiko wa mawazo mbunge huyo.
Tukio hilo limeangaiwa kwenye kamera za bunge na kuonekana kweli mbunge huyo alimvua kofia.
Naibu spika amesema ni kweli tukio hilo halikubaliki na mbunge huyo wa CHADEMA alifanya kosa kubwa kikanuni kwa kusababisha fujo na dharau kwa bunge lakini kwa kuwa sheria za bunge hazijaweka adhabu kwa matendo kama hayo, ametoa onyo kali kwa mbunge huyo na akirudia basi adhabu kali zaidi itatolewa.
hapa mbunge mlinga akiwakilisha malalamiko yake