Nahisi ugonjwa wa moyo unaniwinda baada ya kuachwa na mwanaume aliyenizalisha

odamae

Senior Member
Nov 5, 2020
163
291
Nimekuwa na mawazo yasiyokoma tangu mwaka Jana 2020, furaha imepotea nimekuwa ni mtu wa kuwaza kukosa amani na huzuni moyoni mwangu. Ninasoma chuo fulani lakini maisha yangu ni stress na kutofurahia maisha.

Chanzo kuna mwanaume alinitolea barua aliahidi kunioa nitakapomaliza chuo lakini nilivyoanza tu chuo akaanza vituko akaniacha. Nimeathiriwa kisaiklojia sana na kuona kila kitu kigumu na siwezi tena. Nipo chuo mwaka wa pili naenda wa tatu lakini nimekata tamaa ya kusoma.

Huyo mwanaume kanizalisha na mimi malengo yangu niliyojipangiaga ni kuwa na familia moja lakini mambo yameenda tofauti.

Roho inaniuma sana, nasoma kwa kujilazimisha tu sasa hivi sina moyo wa kusoma kabisa.
 
Sasa wewe badala ya ukomae na shule angalau upate cheti unaendekeza mawazo ya uliyopanga kuwa na familia moja, utashangaa unaishia kuwa na familia tatu bila hata cheti. Maisha hayana huruma ni kupambana kila wakati.
Hadi nilipofikia nimekomaa sana kaka ila tu hii roho ya mawazo inanisumbua sana mwili mzito akili nzito kila kitu!! Kwani nilipoanza tu chuo walinivuruga akili nimekaa mwaka ndipo nikapona lakini huku akili haiko sawa huku nasoma fikilia maumiv ya kuachwa + kuchanganywa akili
 
Pole sana. Elewa tu chombo chenye divai haiwezekani kuweka divai mpya

Mwaga kilicho chomboni kwanza ndipo utaweza kupata jibu la maumivu yako.... focus kwenye maswala yako mengine huyo aondoke akilini mwako kwanza maana kuendelea kumwachia chumba ndani ya fahamu yako kutakuletea matatizo tu wala si kingine.
 
Polee Sana chanzo Cha kukuacha Ni kipi?? Maana kuachwa ni matokeo

Yeye ndo analipa ADA?
Hapana halipi ada ndugu, ghafla tu akanambia naona umri unaenda tuachane Mimi siwezi kukufurahisha katika maisha yako kisa tu nilikuwa nikimtumia hajibu, nikimpigia tunaongea anakata simu ghafla tu bila kuniambia chochote au siku akiamua nikimpigia simu tukiongea kidogo tu ataniambia subiri baada ya dk 5 kuna kazi nafanya akisema hivyo ndo basi imetoka labda umtafute wewe tena, wasap unamuona online ukitumia text hajibu!! Badae alipoanzisha ugomvi wa kuachana akanambia Mimi nina mtoto mwingine na mwanamke yani hadi niliumwa.
 
duu!! Je tukikuchangia hela hizo stress stress zitakoma.
Haziwezi kukoma kaka, nina maumivu makali sana maana niliacha kikazi changu cha cert kwaajili yake ili niongeze elimu maana yeye alikuw elimu ya juu mi nikaonekana sina elimu. Watu wakawa wananitamkia live muda mwingine kuwa sina elimu huyo mwanaume wangu ataoa mwanamke msomi mwezie. Nilikuwa naumia sana na kujiona sina thamani katika maisha na sifai kabisa kuwa na huyo mwanaume ambaye alikuwa ni mpenzi wangu.
 
Pole sana mamy kinachokuuma hapo ni kuzalishwa na kuachwa

Inuka jikaze anza upya akili zako elekeza kwenye masomo

Mungu atakusahaulisha kila kitu inauma sana lakini utakuja kusahau kabisa
Kama uliota ndugu, hicho kinanipa stress sana hamna kitu kinauma kama kuzalishwa. Kingine najisikia aibu sana kwa ndugu na marafiki wanaonizunguka ambao walijua mahusiano yetu maana mahusiano yetu yalikuwa ya muda mrefu sana. Sio mkubwa sio mtoto waliyajua ilifika muda wamama waliniita mama Mapunda yaani walikuwa wakipachika ubini wa mwanaume wangu japo sikuwa mke!
 
Haziwezi kukoma kaka Nina maumivu makali sana mana niliacha kikaz changu cha cert kwaajil yake ili niongez elimu mana yeye alikuw elimu ya juu mi nikaonekana sina elimu watu wakawa wananitamkia live mda mwingin kuw sina elimu uyo mwanaume wangu ataoa mwanamke msomi mwezie nilikuwa naumia sana nakujiona sina thamani katika maisha na sifahi kabisa kuwa na uyo mwanaume ambaye alikuwa ni mpenzi wangu
Badala ya kupata hasiraa usomee mwanao asijekutesekaa na maisha haya, unakaa unamuwazaa Malayaa mmoja ambae ukutee hata hakumbuki kama ashawahi kuwa na mtu kama wewe.. The beat revenge is success amini kwamba dada anguu kaa mahalii liaa sanaa jutaa sanaa yaani hata pombe kunywa alafu amka siku Jikung'ute uanzee upyaaa yani upyaaa kweli na namba ya simu badilisha kama una mapicha ya jamaa chomaa any memory yako na yeye tupilia mbali. Alafu anze kusoma ukifanikiwa rudi kazini kwako hapo mshahara utapanda utaheshimiwa na waliokuwa wanakudharau alafu ajabu huyo mwanaume anaweza kuja na Magotiii akiomba msamaha.

Pigana ufanikiwee inatosha kuwa revenge kabisa.
 
Back
Top Bottom