Baada ya kuona tangazo lao kwenye browser ya Opera nikaclick, ile kuingia tu inaniambia nimejiunga na AppStore na nimepata SMS inayosoma:
"Asante kwa kujiunga na huduma ya Tigo AppShop. Usajili wako umekupatia siku 7 za bure kwenye huduma hii. Tembelea Opera kupata game na apps mbalimbali. Kujitoa kwenye huduma hii, tuma ONDOA GAME kwenda 15025"
Kwa hiyo bila idhini yangu wameniunga kwenye hiyo app store yao na baada ta siku saba nisipojitoa wanaanza kukata hela, sidhani kama huu ni utaratibu sahihi.
mkuu ni vyema uwaripoti TCRA hata mimi nina wasi wasi na yale matangazo yao ya trailer za Bongo Movie kama ni halali, kila siku wanasumbua nayo zamani walikuwa wantumia namba inayoanza na 09 ila sasa hivi hadi namba za kawaida zinapiga
Kwa kweli Tigo ni tatizo kwenye huduma zao mfano nilifanya muamala wa malipo ya maji kwa Tigo pesa mwaka jana mwezi wa 9 pesa hiyo haikwenda lakini walikaikata na kunitumia mpaka jina kwamba nimelipa hiyo huduma sasa cha ajabu baada kufatilia hiyo mamlaka ya maji bado wajaanza kufanya miamala na Tigo pesa lakini kwenye menu ya ya Tigo pesa wameiweka na malipo hayaende kwa hiyo mamlaka kwa kuwa haiwasajili kwa huduma za Tigo kwa hiyo Tigo nazani kuna tatizo na sio bure sasa hiyo pesa kutoka mwaka jana mwezi wa 9 ni mwezi huu ndio imerudishwa tena kwa kuifatilia haswa ukiangalia kurudisha tu huo muamala wamechukua miezi 8