Nafasi kumi za wabunge wa kuteuliwa na hesabu kali za kuwapata

Sheria ipo tofauti na maamuzi mengine yoyote yanayopitishwa katika jamii. Sheria hutungwa pale tu panapokua na tatizo. Huu ndo wakati muafaka wa kupitia na kurekebisha madhaifu na walakini katika sheria za nchi yetu.

Badala ya kuwa na thread za kulalama. Sasa ni wakati muafaka wa kuwa na thread maalumu yenye kuchambua vifungu vya katiba vyenye mapungufu na kupendekeza visomekaje ili viwe na tija kwa taifa
 
kwa wale wanaoelewa vizuri katiba ya Tanzania , naomba majibu kwenye hili

Inapotokea suala la mbunge kujiuzulu kama alivofanya Bwana Possi , je zile stahiki anazopaswa kuwepa mbunge mfano kile kiinua mgongo wanachopewa baada ya bunge kuvunjwa pale nchi inapoelekea kwenye uchaguzi mwingine na yeye aliyejiuzulu anastahili kuzipata
Lowasa alijiuzulu kuwa waziri mkuu baada ya kutumikia wadhifa huo kwa mwaka mmoja tu lakini alipatiwa na anaendelea kupata viinua mgongo na stahiki zingine zote za mawaziri wakuu wastaafu sawa na kwa mfano na Sumaye aliyetumikia wadhifa huo kwa miaka 10. Yeye mwaka 1 tu na wala hakustaafu bali alitumbuliwa na bunge la wakati huo. Pia Maalimu Seif anapata licha ya kuwa naye alitumbuliwa kwenye wadhifa huo na Mwl. Nyerere. Sasa cha ajabu ni kipi Posi akipatiwa hizo stahiki za wabunge wastaafu?
 
Lowasa alijiuzulu kuwa waziri mkuu baada ya kutumikia wadhifa huo kwa mwaka mmoja tu lakini lakini alipatiwa viinua mgongo na stahiki zingine zote za mawaziri wakuu wastaafu sawa na kwa mfano na Sumaye aliyetumikia wadhifa huo kwa miaka 10.
shida yangu ni kujua ni kwa namna gan rais anaweza ku fix lile suala la kuvunja katiba kwa kuwateua wananume weng kuliko wanawake

Kama aliyejiuzulu atalipwa sawa na wabunge wengne maana yake rais hana namna ya kurekebisha ile kasoro iliyotokea
otherwise kama akiteuliwa mtu wa 11 atakuwa ameongeza bajeti isiyo rasmi kisheria.
 
kwa wale wanaoelewa vizuri katiba ya Tanzania , naomba majibu kwenye hili

Inapotokea suala la mbunge kujiuzulu kama alivofanya Bwana Possi , je zile stahiki anazopaswa kuwepa mbunge mfano kile kiinua mgongo wanachopewa baada ya bunge kuvunjwa pale nchi inapoelekea kwenye uchaguzi mwingine na yeye aliyejiuzulu anastahili kuzipata
ndio kama anavyopata Luwasa
 
Kwa kifupi jamaa alichemka, hizo naksh naksh mnazoleta hazina tija na wala hazifuti ukweli.
 
Anayeteua anajua ni kifungu gani. Ni suala la hesabu tu. Hawajatimia wabunge kumi, hivyo namba inaweza kuongezeka au kupungua, muda wowote ule.
...Kwa maelezo yako baada ya miaka mitano atakuwa ameteuwa wabunge hata 20 sasa...Mfano mwakani tena Bulembo naye akiteuliwa ubalozi na akajiuzulu ubunge nafasi yake itakuwa replaced...
 
kwa wale wanaoelewa vizuri katiba ya Tanzania , naomba majibu kwenye hili

Inapotokea suala la mbunge kujiuzulu kama alivofanya Bwana Possi , je zile stahiki anazopaswa kuwepa mbunge mfano kile kiinua mgongo wanachopewa baada ya bunge kuvunjwa pale nchi inapoelekea kwenye uchaguzi mwingine na yeye aliyejiuzulu anastahili kuzipata
Mkuu, kiinua mgongo atakacholipwa kitaendana na muda aliotumikia huo ubunge wake. Ikiwa alikuwa mbunge wa kuteuliwa kwa miaka miwili, kiinua mgongo kitakuwa cha miaka miwili. Iwapo aliutumikia ubunge wake kwa miezi nane na kiinua mgongo kitakuwa cha miezi nane.
 
...Kwa maelezo yako baada ya miaka mitano atakuwa ameteuwa wabunge hata 20 sasa...Mfano mwakani tena Bulembo naye akiteuliwa ubalozi na akajiuzulu ubunge nafasi yake itakuwa replaced...
Ili mradi idadi ya wabunge kumi haijatimia, basi hata 50 wanaweza kufika. Ni mchezo wa namba unaendelea, wakati bado hawajafika kumi kwa mujibu wa katiba.
 
Hizo nafasi mbili zilizobaki aangalie upande wa pili wa Muungano au Wazanzibar vilaza hamna mwenye sifa ya kuwa Mbunge au huu Muungano ni wa Tanganyika .Prof Mbarawa ndo Mzanzibari mwenye akili peke yake
Wapo Wazanzibar vichwa, labda mkuu bado anawechekecha vizuri.
 
Mkuu unapokuja na utetezi wa kwamba huwezi kuvunja katiba halafu mtu anakuuliza umetumia kifungu gani cha katiba kusema kwamba katiba haijavunjwa au haiwezi kuvunjwa unapanic na kutukana!

Jifunze kuendesha mijadala bila ku-panic mkuu.
Sijapanic, ni akili ya kawaida tu. Wabunge wanaotakiwa ni kumi, nusu wanawake na nusu wanaume. Hivi sasa wapo nane, watatu wanawake na watano wanaume. Kwa sababu haijatimia idadi ya wabunge kumi, kinachofanyika ni kuangalia mahitaji ya kiuongozi ya muda maalum. Katika hao nane wanaweza kupangiwa kazi nyingine na zile nafasi zinazobaki wanawekwa watu wengine. Mkuu kabisa anakuwa mjanja kutoteuwa wabunge wote kumi kwa muda mmoja ili asibanwe na taratibu za kikatiba.
Haihitaji kujua kifungu cha katiba, kama mtu anaweza kuipata katiba yenyewe kwa ujumla wake, na aende akaisome yote, afanye hivyo kwa muda wake mwenyewe.
 
Wangekuwa wameteuliwa wabunge kumi halafu kati yao wanaume wakawa ni wengi zaidi, ungekuwa ni uvunjwaji wa katiba.

Wapo wabunge nane, kati yao kinamama watatu na kinababa watano. Kumbuka kuwa kati ya hao kinababa watano, wanaweza wakapangiwa kazi nyingine na automatic ubunge wao ukawa hauna tena kazi, na nafasi zao zikachukuliwa na kinamama.

Tunashukuru kwa utetezi hata kama ni utetezi dhaifu. Nikushauri bwana Phillipo huu utetezi wako ambao unadhani ni ufafanuzi umezidisha mshangao.
 
Back
Top Bottom