Nabii wa Mapenzi!! Free style

Ryan The King

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
2,788
2,690
         

Sijui nianze na aya ipi. Subiri! Subiri mpenzi. Embu chukua kwanza hii  . Upendo wangu kwako nimeumimina nao nimeujaza nafsini mwako usikose pa kutokea. Nitakupa mwili na moyo, roho na nafsi.


Mtoto umeumbika haswaa. Umejazia riziki mafungu Saba. Umbo lako si la kubeza. Napenda ukitembea umbo lako likijitingisha. Napenda ukikaa kwenye bodaboda nionapo sehemu ya msambwanda wako ikitokea nyuma ya seat. Upaja laini wa huzurungi ya mtelezo.

Nakaa natafakari ningeishi vipi Kama Mungu asingekuumba. Naiona huzuni kubwa siku nikikukosa.
Nakupenda.
Nakuhitaji.
Najua wewe ndio furaha yangu. Wewe ndio alama halisi ya utamu asali kwangu ya nini. Dalili nzuri ya mafanikio.

Umenimulika na mg'ao wa mapenzi yako. Uzuri wako umenipa nuru nafsini mwangu.

Jina lako ni tamu.
Tamu haswa.
Tamu kuliko Utamu wa Vanila naam umezidi utamu wa asali.

Wee ni katoto kangu.
Kababy gooo!
Kasweet moyo.
Kavitamin kangu.
Ka-star kangu.

We ndio habari ya mjini katika ukumbi wa mtima wangu.

Mwanzo nilihisi marue rue nilipokuona. Nilidhani nageuzwa kuwa nabii. Siku ile Kama unaikumbuka. Nilihisi nimetokewa na Malaika kutoka pepo ya Saba. Moyo ulikimbia, damu iliganda kwa nukta kadhaa. Nilihisi kupagawa.

Mafunuo nilipokea.
Mafunuo ya mapenzi.
Mapenzi matamu kutoka peponi.
Pepo nzuri ya mahaba.

Naomba nirudie mpenzi. Kamwe usichoke kusikia wimbo wangu huu;
Nakupenda nakupenda.
Mpenzi wangu umenishinda.
Hisia zaangu umeziteka,
Umezifunga na lako penzi.
Kwa mwingine sisogei.

Basi nikakuonja. Si unakumbuka siku ile wee katoto. Ilikuwa siku adhimu mpaka leo naiadhimisha Kama sikukuu.
Utamu ulionipa
Daaa sikuona wa kuufananisha.
Nilijihisi naionja kuzimu. Kwani pumzi ilikata.

Naongea lugha ya mapenzi, nakupa maajabu ya mahaba na ishara za kupendeza. Hukukosea kuniita mungu wako wa mapenzi japo aliyenijalia ni Maanani Rabuka. Nitakupa miujiza ya kimahaba,
Ukiwa kipofu uone,
Kiziwi usikie, na kiwete utembee.
Mimi ni nabii wako wa mapenzi.

Basi mapenzi nikayamega kwa kipande cha uma.
Uma wangu uliingia kunako keki yako kuipasua. Taratibu keki yako niliigawanya. Nilikuonea huruma ulipokuwa ukilia nikiimega keki yako tamu. Badae ulicheka na chezo likachezwa.

Macho yako yakuchora huwaga yananimaliza. Najua utanibakiza mkia kwa wewe ni zimwi linijualo ambalo huwezi kunila nikaisha.

Nitakula sitambakizia yoyote kwani huu mchezo hauhitaji kusaza. Hata mabaki yakisalia usiku nitayaamkia.

Swaga zangu ulizipenda. Swaga kutoka pepo za mbali. Pepo zilizopindua mapindo manne ya moyo wako. Nikaubwaga bwaaa!! Moyo wako.
Sasa umegeuka ua la uwandani. Moyo wangu kuupamba.

Najua upo humu. Tafadhali tupi yako ishara. Ishara ileeee!! Ya siku zile. Siku uliponipa ufunuo wa mapenzi. Nikageuka nabii wa karne hii.

UTABIRI KWA MPENZI WANGU.

Ikawa nilipokuwa katika njozi za usiku. Natazama nikaona mji mkubwa tambarare. Nao mji ule ulikuwa umezungukwa na mto katika kingo zake.
Nikiwa katika kustaajabu Mara kwa mbali Kama mtupo wa mkuki akatokea mrembo. Yule mrembo alikuwa anamavazi Kama malikia wa Falme za kifilipino.
Moyo wangu ukajawa hofu. Miguu ikakosa uzima.
Naye akasogea hata kunikaribia akiwa kashika tunda la rangi ya yakuti Kama yalivyo mavazi yake. Kichwani alivaa taji ya dhahabu.
Akanena maneno ambayo si kwa lugha yangu.
Naye alipoona sisikie akaninyooshea mkono kunipa lile tunda alilokuwa amelishika.
Nilipolipokea na kuking'ata natazama mwili wangu ukaanza kusikia vichomi vichomi. Na hapo akaongea tena.
Mara hii nilimsikia kwa lugha yangu.

Nikiwa katika kuogopa. Akanishika mkono wake ambao kwa ulaini nilikosa msamiati wa kueleza.
Akanikumbatia. Mwili wangu ukawa Kama mfu. Akaninong'oneza maneno haya akisema;
"PENZI LA KIFO"
Hapo ndipo nilipojikuta nipo uchi wa Sanamu. Naye akanisihi ni mlale kwani uchi wangu haukuwa na moto.

Nami nikiwa katika hamu nikaupa moto uchi wangu nao ukatoa majira kumi na mbili kwa nyakati za mchana na kumi na mbili kwa nyakati za jioni.

Akapanda juu ya uchi wangu wenye majira naye kwenye shimo lake nilipotazama kulikuwa na maandishi mekundu ambayo yameandikwa kwa herufi kubwa na yenye kung'aa. Yalisomeka;
"KISIMA CHA MAARIFA"

Nikachukua kidole kuyagusa. Naye akaanza kupumua Kwa nguvu. Akatema ukelele akisema;
" SASA IMEKUWA FURAHA DUNIANI"

Sikujua maana yake mambo Yale.
Nilipoteza fahamu Mara baada ya kuingiza mshale wangu wa majira kwenye KISIMA CHA MAARIFA cha binti yule.

Nilizinduka na kumuona akiwa na wana ambao kwa sura nilifanana nao.
Sasa sikushangaa Kama mwanzo nikajikuta namchukua yule mwanamke na wale watoto.

Basi nikazinduka kutoka katika njozi.
Mara sauti kutoka kwenye paa la nyumba ikasikika ikinambia andika.

Nikajibu, nitaandikaje ikiwa simuoni asemaye Nami.

Nayo ikasema, tazama nyota ya mapenzi imekushukia. Andika maneno haya kwa maana hayana budi kutukia katika njia yako.

Basi nikachukua laptop na kuanza kuandika.

Andika;
Wewe ndiye taa ya moyo wangu. Umenimulikia kwenye giza la mauti.
Umenipa faraja moyoni katika maisha yangu.

Uzuri wako umewashinda binti za facebook, naam binti za instagram wamepesushwa na uzuri wako.

Umenipa hisia mpya. Nami nimeduwaa.
We ndiye tumaini langu katika safari yangu.


Ghafla nikashtuka Asubuhi imefika.

Unabii wa mapenzi bado nitakutabiria mpenzi wangu.
Najua unapenda Swaga zangu na mambo yangu ya kipekee ambayo hakuna mwenye nayo. Na Kama yupo basi amekopi kutoka kwangu.


Karibuni.
Free style.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…