Nabii GeorDavie: Yesu akirudi leo atataka kutumia gari yangu na atataka nimfuate Airport

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,661
6,395
Nabii Geordavie amesema kwamba endapo Yesu angerudi leo, angehitaji kutumia gari lake na kumtaka amfuate uwanja wa ndege kwa ajili ya msafara wa hadhi yake. Nabii huyo alieleza kuwa Yesu angekuwa na mtazamo tofauti, akiamua kukaa naye na kuchagua gari miongoni mwa alizonazo ili kuendana na hadhi yake.

"Nadhani atakuwa na mtazamo tofauti, jambo la kwanza ataamua kukaa na mimi na atataka kutumia gari langu, atachagua katika hizi (gari) na ataomba nimfuate airport (uwanja wa ndege) kwasababu ndio hadhi yake na kutakuwa na msafara kabisa."

Yaani Yesu Kristo akija mara ya pili kama Bwana wa mabwana Mfalme wa wafalme atamuomba kiumbe aliyemuumba ampe msaada wa usafiri? Sitasema kuwa ni kufuru! Ila nitasema huyu jamaa hajui analolisema na anahitaji maombi! Huyu ni masikini kuliko masikini wote niliowahi kuwasikia!
 
Huyo atakuwa ni yesu wa mchongo. Huyu jamaa anamfanya Yesu kama msela tu, anaonesha jinsi asivyo na imani. Kumbe huduma yake ni abrakadabra tu anadang'anya wehu waliokusanyika kambini kwake wakimsikiliza na kumuamini kuwa ni nabii na mtume kumbe ni zuga tu
 
images - 2023-11-17T211149.491.jpeg
 
Yaani Yesu Kristo akija mara ya pili kama Bwana wa mabwana Mfalme wa wafalme atamuomba kiumbe aliyemuumba ampe msaada wa usafiri? Sitasema kuwa ni kufuru! Ila nitasema huyu jamaa hajui analolisema na anahitaji maombi! Huyu ni masikini kuliko masikini wote niliowahi kuwasikia!
Kweli. Huyo Yesu atakayepanda gari la mwanadamu atakuwa si yule aliyeumba mbingu na nchi. Huyo akishuka nchi itakumbwa na tetemeko kuu. Kitakachofuata baada ya hapo ni kilio cha kusaga meno
 
Back
Top Bottom