Ni takribani miezi miwili sasa inakatika huku kukiwa na ukimya wa kushangaza kutoka vyombo vya usalama kuhusu kilichowatokea ROMA na wenzie,mimi kama raia wa nchi hii imeumizwa na kusikitishwa sana na ukimya huu kuliko hata tukio lenyewe la utekaji,haiwezekani raia wanatekwa wanaenda kuteswa vibaya halafu tukio hilo lipite kama hakujatokea kitu inasikitisha sana.
Nimesikitishwa pia na kimya cha waziri wa habari kwa jinsi picha yake inavyonijia siku akiwa kwenye press conference ya ROMA akionekana kana kwamba ana uchungu na ameguswa sana na tukio hilo kumbe alikuwa anatuachezea bongo muvi,inasikitisha sana
Hata mkuu wa mkoa aliyehakikisha vyombo vya dola vinafannya juu chini kuhakikisha ndugu zetu watanzania wenzetu wanapatikana wakiwa wazima nae pia hana hata habari kama vile hili jambo halikumgusa,KWELI!?
vyombo vya usalama viko kimya,mwezi wa pili huu unakaribia lakini hakuna findings wala update yoyote mpaka sasa,hii inaleta picha mbaya kwamba raia sasa hatuko salama ndani ya nchi yetu kama ni kweli watu wanaweza wakafanya mambo ya kutisha kiasi hicho halafu wakapotelea GIZANI.huu ni muendelezo wa matukio ambayo serikali haiyapatii ufumbuzi kama matukio yanayotokea huko KIBITI,tukio la kupotea BEN SANANE,matukio haya yanaichafua serikali kwamba imeshindwa kuchukua hatua au serikali inapuuzia UHAI wa RAIA wake na pia inapuuzia haki ya sisi wananchi kujulishwa kuhusu usalama wetu.kwa hali hii halafu anatokea mtu anakuhubiria kuhusu UZALENDO,kweli!?