Mkuu kula like yangu. Inashangaza kuona hawa wa kijani walivyo bendera fuata upepo. Ni mwaka jana tu walikuwa wakitetea uozo wa serikali yao kwa maana ya kwamba hawakuona mapungufu. Leo wanaelekezwa kufuata taratibu katika maamuzi, wanalipuka mara ooh! wewe UKAWA unashabikia mafisadi.Inashangaza sana.Ni vigumu sana kuelewa ukiamua usielewe. Lugumi kapigiwa kelele sana na wapinzani kwa ufisadi wake, ila naamini kwa ushabiki wa wanaccm Magu akisimama jukwaani na kusema Lugumi akamatwe na kunyongwa mtashangilia sana. Na wapinzani haohao wanaomtuhumu watakataa hata hiyo na kusema akanatwe na kushtakiwa kwa mujibu wa sheria za nchi.
Na kwa hilo na kwa akili zenu mtasema wapinzani wanatetea mafisadi..
Ni tofauti tuu ya mfumo wa akili ya ukweli na ya unafiki