N/Waziri Kigwangalla: Kuanzia sasa lazima kila mwananchi awe na Bima ya Afya

Kuweka chakula tu kwenye hospitali moja ya muhimbili wameshindwa ndio wataweza kuhudumu watanzania mil.50 kwenye sector ya afya pekee.......TBCCM waanzishe kipindi kinaitwa political comedy kiwe kinarushwa kila ijumaa jioni wawe wanaweka matukio kama haya.
 
Magufuli ni chaguo la Mungu.

Chadema watanyooka tu
Mnapenda kumsingizia Mungu kwa kila kitu. Mungu hana upendeleo, alituumba wote sawa. Hakuna cha Magufuli kuchaguliwa/kuteuliwa wala cha Israel kuchagulia/kuteuliwa mnaokubaliana na hii mentality/idea ni wajinga na mtazidi kudanganyika.
 
Siyo hivyo mkuu.

Ila watanzania tulisali sana ili tupate kiongozi atakayekomesha ufisadi
 
3aa7a7a2-1c6d-48cc-9cd1-4cfbdc751d4c.jpg
 
Tatizo hawa mabwana maneno mob hakuna lolote. Vipi ameshaanza kumsomesha yule binti toka Mwanza aliyetoa ujumbe UN kuhusu utunzwaji mazingira. Honest is very expensive.....wanasiasa kazi yao ni kudanganya mioyo yao wakidhani ndio fahari....noma sana siasa za bongoland
 
Nchi isiyoweza kutengeneza sewage na water systems zinazofanya kazi itaweza kugharamia afya kwa wananchi wake? Wanatufanya sisi ni wajinga. Poombavu sana.
 
Siyo hivyo mkuu.

Ila watanzania tulisali sana ili tupate kiongozi atakayekomesha ufisadi
Hivi kwa akili yako ya umri wako unaamini ufisadi umekomeshwa? Ufisadi upo na utaendelea kuwepo milele. Utakomeshwa pale tu serikali itakapoweza kuwatia nguvuni viongozi walioitia hasara hii nchi mfano rais aliyetangulia na aliyemtangulia. Katiba ikibadilishwa na kuwezesha viongozi wa serikali kushitakiwa na kutiwa nguvuni ndipo huu mnaosema ni ufisadi utapungua.
 
Uwekwe utaratibu mzuri. Bima kwa wote ni jambo muhimu ila linahitaji approach na mikakati mizuri, matamko hayasaidii kama hayo hayapo.
 
Magufuli ni chaguo la Mungu.

Chadema watanyooka tu
Watanyooshwaje hawa majirani wetu kaka..hebu fafanua kidogo tufahamu kwa afya buree wakati ruzuku mahospitalini hatupeleki?? Lakini tutawanyoosha kwenye mikutano hawatafanya kamweee ..
 
Waziri alipaswa kusema kuwa itakuwa ni Haki Kwa Kila Mtanzania kuwa na bima ya afya sio lazima.
Pili, amefanya jitihada gani kuboresha huduma za bima ya afya Kwa sasa?
Idadi hii ndogo ni mzigo Kwa NHIF, je ikishakuwa Kwa idadi kubwa itakuwaje?
 
Hii siiamini kwa jinsi mazingira yetu yalivyo Na hizo huduma za afya zinavyotolewa.
 
Nishukuru kwa taarifa. Lakini kwa wenye 'alergy' na tarakimu mbovu, taarifa ina mapungufu. Sherehe za miaka 50 kwa kanisa lililo anza kutoa huduma 1935 na leo tupo mwaka 2016, tayari naanza kupiga chafya!
 
Naibu Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Dkt. Khamis Kigwangala amesisitiza kuwa kuanzia sasa itakuwa ni lazima kwa kila Mtanzania kuwa na Bima ya afya,huku akiwatoa hofu wananchi wasio na uwezo kwamba serikali kupitia Sera ya taifa ya afya ya mwaka 2007, itakuwa tayari kugharamia matibabu ya makundi maalumu ya kijamii wakiwemo wazee wenye umri wa zaidi ya miaka 60, watoto chini ya umri wa miaka mitano na watu wenye magonjwa ya kudumu.

Naibu Waziri kigwangala, ameyasema hayo wakati akifunga Maadhimisho ya miaka 50 ya utume wa injili kwa waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato Kirumba Mwanza yaliyofanyikia katika uwanja wa CCM Kirumba, yakiwa yametanguliwa na zoezi la utoaji wa huduma za afya bure kwa wakazi hilo zilizofanywa na madaktari bingwa wa macho,meno,kibofu cha mkojo,tezi dume,kisukari na saratani ya shingo ya kizazi kwa siku saba mfululizo.

Sherehe za miaka 50 tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo la Waadventista wa Sabato katika jiji la Mwanza mnamo mwaka 1935,lililopo chini ya jimbo la Nyanza Kusini,ambalo hadi sasa limefikisha makanisa 84 pia zimehudhuriwa na Naibu Waziri wa ardhi, nyumba na makazi Mh.Angelina Mabula, ambaye amesema kazi kubwa ya kanisa ni kuendelea kuokoa maisha ya waumini wake kiafya na kiroho pamoja na kusimamia maadili mema ndani ya jamii.

Kwa upande wake Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato tanzania Dk.Godwin Lekundayo, ameiomba serikali kuharakisha usajili wa hospitali ya Pasiansi inayojengwa na kanisa hilo ili iweze kuanza kutoa huduma kwa muda uliopangwa, lengo la kanisa la SDA jimbo la Nyanza Kusini ni kuifanya hospitali hiyo kutoa huduma za matibabu ya rufaa ili kuokoa maisha ya watu.

Ninashukuru sana kwa kuangalia umuhimu wa afya za watym ndugu naibu waziri.
Lakin naomba muende hatua mbli zaidi. Angalieni sana hawa wanaokatia watu huduma za afya viwango vya hospitali wanazofanya nazo biashara. Nyingi ni za viwango vya chini ambavyo havina uwezo wa kutoa huduma bora hasa katika magonjwa complicated. Na pia angalieni magonjwa wanayokaweka kwenye orodha ya kutibiwa kwa bima na yale wanayoyaacha. Nilikuwa nasafiiri nikapitia Tabora na kwa bahati mbaya nikakuta jamaa yangu mgonjwa anahitajika kwenda kutibiwa na alikuwa na kadi ya bima.

Dr. Alimwandikia vipimo vyote alivyoona vinahitajika, lakini kwend amaabara akaambiwa mgonjwa apunguze kipimo kimoja kwa kuwa vimezidi. Niliuliza how? Wakasema basi amwambie Dr. apunguze kipimo kimoja kwa sababu wagonjwa wa bima hawapimwi vipimo vyote vile na vingine havimo kabisa kwenye bima.
Nilimwambia maabara wa hosptal ile amshauri mgonjwa ni kipimo gani anachokiona yeye kinatakiwa kupunguzwa. Na bial kujiongeza akaingia kichwa kichwa kutaja kipimo kimoja kiondolewe. Yaliyotokea pale sitaki kuyasema isipokuwa nililmwambia atuambie hicho kipimo kilichozidi ni cha shilingi ngapi. Akasema elfu tatu mia tano. Tulilipia cash mgonjwa akapimwa. Na bahati mbaya, ni kwamb vipimo vyote vilikuwa negative kasoro hicho alichokuwa anakifuta mtu wa maabara ndipo lilipokuw atatizo. Naomba mengine , mjazie wana jamvi.

Ndugu naibu waziri naomba baada ya kuyachunguza makampuni ya bima, angalieni na hosptali zetu. Hakuna dawa, hakuna huduma ni mauti tupu!. Mtu anakwenda na bima yake lakini mwisho wa siku hosptali haina dawa anaambiwa kwenda kununua na lazima anunue ili apone.

Ninaomba sana, kabla hamjaanza kulazimisha watu wakate bima, hakikisheni hospitali zetu hasa zinazoingia mkataba wa bima zina huduma safi na madawa bora ya kutosha. Uhai ndio mtaji wa binadamu. Huduma za Afya ni bure watu wanakufa kama nzige na bima wanazo. Angalieni huduma zinazotolewa, viwango vy awahudumu na upatikaani wa madawa na vitendea kazi. Jambo kubwa jamani angalieni sana usafi. Hospital nyingi ni chafu na zinanuka!. Regulatory and supervisory entities ziko wapi jamani? Acheni kuuza sura na kujitafutia umaarufu. Boresheni huduma sifa zitawafuata kule mliko siyo mzitafute.
 
Serikali hii ina wakurupukaji wengi na wapenda sifa kwa namna ambayo sijawahi kufikiria. Haya ndiyo majembe ya mtukufu Rais anayoyategemea katika kuwashusha wanaoishi kama malaika ili nao waishi kama mashetani.
 
siwezi kulipia bima ya afya wakati sina uhakika wa kupata huduma zinazostahili, naona kila waziri anataka asifike anavyokusanya mapato badala ya kufanya kazi kwa ufanisi
Subiri matokeo ya gizo hilo usiongee kabla halijatokea.Hakuna wa kukufata nyumbani ila utakiona cha mtema kuni. Rwanda hilo lipo, ila bila bima hiyo huwezi pewa huduma ya aina yoyote ile. Labda kama hutaingia kwenye ngazi yoyote ya serikali, hata kwa mwenyekiti lazima uende nayo.Hapo naona ukisema hutoi unajiongelea tu.Utatoa na huduma za matibabu utaenda pharmacy
 
Kuna mijitu Bongo inadhani kukosoa serikali ni kuwa against ccm.Hivi mtu kwa akili zako Unaweza kukubaliana na maamuzi ya hawa viongozi wetu ?Kila siku wanakuja na matamshi yasiyoingia akilini haa kwa mtu mwenye elimu ya darasa la 4 yet utasikia mijitu inaunga mkono just because ni mikereketwa ya chama tawala.Hovyo sana.
 
Naibu Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Dkt. Khamis Kigwangala amesisitiza kuwa kuanzia sasa itakuwa ni lazima kwa kila Mtanzania kuwa na Bima ya afya,huku akiwatoa hofu wananchi wasio na uwezo kwamba serikali kupitia Sera ya taifa ya afya ya mwaka 2007, itakuwa tayari kugharamia matibabu ya makundi maalumu ya kijamii wakiwemo wazee wenye umri wa zaidi ya miaka 60, watoto chini ya umri wa miaka mitano na watu wenye magonjwa ya kudumu.

Naibu Waziri kigwangala, ameyasema hayo wakati akifunga Maadhimisho ya miaka 50 ya utume wa injili kwa waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato Kirumba Mwanza yaliyofanyikia katika uwanja wa CCM Kirumba, yakiwa yametanguliwa na zoezi la utoaji wa huduma za afya bure kwa wakazi hilo zilizofanywa na madaktari bingwa wa macho,meno,kibofu cha mkojo,tezi dume,kisukari na saratani ya shingo ya kizazi kwa siku saba mfululizo.

Sherehe za miaka 50 tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo la Waadventista wa Sabato katika jiji la Mwanza mnamo mwaka 1935,lililopo chini ya jimbo la Nyanza Kusini,ambalo hadi sasa limefikisha makanisa 84 pia zimehudhuriwa na Naibu Waziri wa ardhi, nyumba na makazi Mh.Angelina Mabula, ambaye amesema kazi kubwa ya kanisa ni kuendelea kuokoa maisha ya waumini wake kiafya na kiroho pamoja na kusimamia maadili mema ndani ya jamii.

Kwa upande wake Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato tanzania Dk.Godwin Lekundayo, ameiomba serikali kuharakisha usajili wa hospitali ya Pasiansi inayojengwa na kanisa hilo ili iweze kuanza kutoa huduma kwa muda uliopangwa, lengo la kanisa la SDA jimbo la Nyanza Kusini ni kuifanya hospitali hiyo kutoa huduma za matibabu ya rufaa ili kuokoa maisha ya watu.

Mazungumzo kibao yanazungumzia Kanisa. Mada yote imezungumzia Kanisa, naona aina chembe ya ukweli apo
 
Back
Top Bottom