Mwisho wa kulipia daraja la Nyerere (Kigamboni)

Wadau kuna mambo lazima tuyajadili!!
Nani anayejua ni lini NSSF wataacha kuchaji kwa ajili ya kupita darajani? Kwa malipo ya sasa wamekadiria kwa rate hii ya sasa, itawachukua miaka mingapi kurejesha pesa zao! Na baada ya pesa zao kurejea ndio Utakuwa mwisho wa tozo?

Na tunalipia just kwa kuwa pesa za mkopo au kuna sababu nyingine?
Kuna baadhi ya watu wanahoji mbona mwendo kasi watu hawalipii njia, au pesa za nje ndio wanagharamia hadi walio kijijini Ila mkopo wa ndani ndio wakazi tu?

Vipi kuhusu udom? Nao pia ni mkopo wa taasisi za mifuko ya hifadhi za jamii, kwanini wanaosoma nao wasigharamie mkopo?

Kwanini kigamboni tu?

Kwanini sio mto Rufiji au Malagarasi etc?

Kwanini gharama ziko juu?
Malipo ya mwezi kwa wastaafu wa NSSF siku hizi yanausumbufu mkubwa kwani hayana tarehe ya uhakika, inawezekana mpaka wakusanye ushuru ndopo wawalipe waataafu. Sasa usitegemee kusitishwa.
 
Unatumia zaidi ya 900,000/- kwa mwaka!
Ndio, nipesa ambayo mtuangeweza kumlipia mwanae shule akapata elimu bora.

Serikali lazma ifikirie kumpunguzia mwananchi gharama zisizo za lazima kama hizi.
 
Gharama za mafuta huyu wa Kigamboni nae anazo. Wengi wakazi wapya wanakaa kuanzia Kibada (20km from ferry/bridge) au geza/dege ambapo ni kama 30km.
Gharama zote ambazo mtu wa Kibaha anazo wa Kigamboni pia anazo ila hio 900,000 ni wa Kigamboni tu anakabiliana nazo.
Hili ndilo tatizo la sie Watanzania. Hatutaki kuanza na planning kabla ya kuanza kitu chochote. Business plan ni muhimu kabla ya kujenga au kuanzisha biashara au kitu chochote. Hata wakati watoto wetu wanataka kuanza shule huwa hakuna planning ya kuwa akimaliza chuo na Bachela ya Records Management au Business Administration je ataajiriwa wapi au ana uwezo wa kujiajiri? Mwisho akimaliza Chuo anaanza kulau serikali haitoi ajira blah blah blah. Tuwe tunaplan kwanza na ikibuma unagugumia ndani maana ni hasa yako mwenyewe baadala ya kutoa lawama kwa wengine hata M/Mungu
 
Kama Muhimbili tunalipa kwa nini tusilipe kwenye daraja.
Waanzishe ticketi za mida mahalumu tozo ipungue
 
Gharama za maisha ambazo zinamkabili mkazi wa Kigamboni pekee(mwenye usafiri binafsi)
Saloon car
1500/- gharama za kuvuka darajani au kwa pantoni.(3000/- kwenda na kurudi)
6 siku sita za wiki
52 wiki katika mwaka mmoja
3000*6*52=936,000.

Kwa mkazi wa Kigamboni ambae anamiliki gari ndogo na anafanya kazi upande wa pili maximum siku 6 kwa wiki atatumia 936,000 kwa mwaka. Hii ni gharama ya ziada ambayo ni mkazi wa Kigamboni pekee anaipata.
Ukiona hivi, ujue hujafikia kiwango cha kumiliki gari. Una lazimisha tu
 
606305c6f8832c7f8c9069e4543a3aed.jpg
 
Hili ndilo tatizo la sie Watanzania. Hatutaki kuanza na planning kabla ya kuanza kitu chochote. Business plan ni muhimu kabla ya kujenga au kuanzisha biashara au kitu chochote. Hata wakati watoto wetu wanataka kuanza shule huwa hakuna planning ya kuwa akimaliza chuo na Bachela ya Records Management au Business Administration je ataajiriwa wapi au ana uwezo wa kujiajiri? Mwisho akimaliza Chuo anaanza kulau serikali haitoi ajira blah blah blah. Tuwe tunaplan kwanza na ikibuma unagugumia ndani maana ni hasa yako mwenyewe baadala ya kutoa lawama kwa wengine hata M/Mungu
Hakuna anaekaa Kigamboni ambae hakuwa anajua kuwa kuna kulipia kivuko au daraja. Kuainisha gharama za kuvuka kwa mwaka haina maana mtu hakujua kwamba atalipa. Nilichajaribu kufanya ni kuonesha extra cost kwa mtu kuishi Kigamboni na kufanya kazi upande wa pili, au kuna mahali nimelaumu? Mtu yeyote makini huwa anajua gharama zake za maisha hasa zile za ziada.
 
Kama ningelijua mapema daraja linalojengwa ni la kulipia bora ningetafuta kiwanja kwingine. Najuta
 
Chazo cha mapato kwa serekali. Kwa huyo sina kikomo. Tunahitaji kujenga vitu vingi sana. Madaraja kule lake Victoria nk
 
Back
Top Bottom