Mwandishi aliyeripoti vifo vya ng'ombe 17,000 achukuliwe hatua

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,951
29,532
Mwandishi huyu bila ashaka anastahili kushtakiwa kwa uongo na uchochezi.Kumekuwepo na tabia ya waandishi kuzusha habari kwa lengo la kisiasa na maslahi binafsi,Na wakiachwa waendelee basi tutakuwa tunaendekeza kizazi cha uongo .

Leo hii kuna mwandishi karipoti kuwa mvua iliyonyesha shinyanga imeathiri watu zaid ya 200.

Hapa naweza kujiuliza mwandishi huyu ameitoa wapi hii taarifa na ina ukweli kiasi gani?
 
Raisi kamweka wazi eti ng'ombe 17000 Elfu wamekufa Hata rift valley Isingekuwa hivyo
Kumkemea pekee haitishi ni vyema akakutana na mkonio wa sheria ili liwe somo kwa waandishi wote wa vibahasha
 
Eti Ng'ombe 17,000 na yeye anasubiri akahojiwe na ITV ndio aseme!

Huyu Mfugaji Uchwara na mtangazaji wapelekwe kwny Mikono Salama mpaka wataje Wafadhili wa Mradi wao wa kumtisha Rais ambae kawastukia
 
Mwandishi huyu bila ashaka anastahili kushtakiwa kwa uongio na uchochezi.Kumekuwepo na tabia ya waandishi kuzusha habari kwa lengioo la kisiasa na maslahi binafsui,Na wakiachwa waendelee basi tutakuwa tunaendekeza kizazi cha uongo .
Uzi huu pamoja matatizo ya kiuandishi ingekuwa na mantiki endapo mleta mada angetaja ni mwandishi yupi wa gazeti gani na aliripoti lini.Maana inawezekana habari hii imekuzwa kiasi cha kumkasirisha Rais.Hivi ni kweli hapo Morogoro hasa Mvomero kuna mfugaji anayemiliki ng"ombe zaidi ya elfu 17,000,000 kweli.Idadi hiyo ukigawanya kwa 100 ni sawa na 170,000 idadi ambayo bado ni kubwa kuliko hata idadi ya wafugaji wenyewe.Mleta mada karibu kwa ufafanuzi wa chanzo cha habari tafadhali.
 
Msiongee vitu bila kufanya research mvomero ni kubwa na kuna ng'ombe zaidi ya 100k kuna kijiji kinaitwa mangae ambako ninafika mara kwa mara kuna ng'ombe zaidi ya 10k nilikuwa huko xmas kuna ukame wa ajabu na ng'ombe wanaendelea kufa,waliobaki wamekonda kiasi kwamba huwrzi muuzia mtu,tatizo wamasaai ni wabishi sana kuwa ng'ombe wengi kwao ndio utajiri na hawasomi alama za nyakati kwa hiyo sitashangaa kama kweli wamekufa hao 17k na mvua isipokuja majanga yatakuwa makubwa
 
Mwandishi huyu bila ashaka anastahili kushtakiwa kwa uongio na uchochezi.Kumekuwepo na tabia ya waandishi kuzusha habari kwa lengioo la kisiasa na maslahi binafsui,Na wakiachwa waendelee basi tutakuwa tunaendekeza kizazi cha uongo .
Mbona na wewe mwongo
 
Mkuu hii habari ilitoka kwenye moja ya magazeti ya kila sik u....kama siku tatu au nne hivbi zilizopita.
 
Wafe wengi vita ya wakulima na wafugaji ipungue
 
Hakuna chombo cha habari kilichoripoti idadi hio, wekeni hapa hio taarifa au kaisoma yeye peke yake???
 
Kinachonishangaza ni wananchi wanalalamika na Rais nae analalamika. Kwanini hilo gazeti au mwandishi wa habari ajachukuliwa hatua kwa kudanganya umma?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…