SI KWELI Mwanamuziki Celine Dion alihudhuria harusi ya mwanaye akiwa kwenye 'wheelchair'?

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Siku za karibuni kuliibuka picha mnato na mjongeo zikimuonesha mwanamke anayedaiwa kuwa ni Celine Dion akiwa kwenye kiti cha magurudumu ikiwdaiwa ni siku ya ndoa ya mwanaye wa kiume. Picha zile ziliibua hoja mbalimbali katika namna mbili ambapo kundi moja likidai ni Celine Dion na kundi jingine likidai kuwa siyo yeye.

Ukweli ni upi wadau?

dion.png
 
Tunachokijua
Picha za mwanamke huyo zimekuwa zikisambaa mtandaoni tangu mwanzoni mwa mwaka huu 2023, kwa mujibu wa Google Image Search. Picha hizo zinaonekana kutoka kwenye video inayodaiwa kuwa inamuonesha mwanamuziki Celine Dion.

Mtumiaji mmoja wa Facebook, kwa mfano, aliweka video (hapa) pamoja na maelezo: "Hii ni Celine Dion akihudhuria harusi ya mtoto wake akiwa kwenye kiti cha magurudumu. Anaugua ugonjwa nadra unaojulikana kama Stiff-syndrome person. Oh, Celine Dion na sauti yake nzuri... Tuna somo la kujifunza kutoka kwake."

Posti yenye maudhui kama hayo (yenye picha tu bila video) ilifika pia katika jukwaa la JamiiForums.com ikionesha kumsikitikia mwanamama huyo kwa hali anayoipitia, huku ikisisitiza ukaribu na Mungu ili kuepusha changamoo za kiafya.

Hata hivyo, ni muhimu tukipata muhtasari kuhusu matatizo ya afya yanayomkabili Celine Dion. Nyota huyo wa pop kutoka Canada alitangaza mnamo tarehe 8 Desemba, 2022 kupitia mtandao wa Instagram kuahirisha ziara yake kutokana na ugonjwa wa Stiff Person Syndrome, ugonjwa nadra wa neva ambao huathiri takriban mtu mmoja kati ya milioni moja.

"Nimekuwa nikikabiliana na matatizo ya afya kwa muda mrefu, na imekuwa vigumu sana kwangu kukabiliana na changamoto hizi na kuzungumzia yote ambayo nimekuwa nikipitia," Dion alisema katika video yake. "Ninafanya bidii sana katika maonesho yangu, lakini hali yangu hainiwezeshi kufanya hivyo kwa sasa."

Kwa mujibu wa taasisi ya Stiff Person Syndrome Research Foundation, Stiff Person Syndrome ni ugonjwa unaosababisha misuli kukakamaa, kupata spasms (mshituko/mtetemo wa misuli) katika mwili na miguu, maumivu makali, na kupata wasiwasi (anxiety) wa muda mrefu.

Pamoja na ukweli kuwa Celine anapitia changamoto hiyo, utafiti wa JamiiForums umebaini kuwa si yeye anayeonekana katika video hiyo iliyosambaa mtandaoni.

Ukweli ni kwamba video hiyo inamuonesha mwanamke kutoka Florida, Marekani anayeitwa Kathy Poirier, ambaye ana amyotrophic lateral sclerosis (ALS) – ugonjwa ambao huathiri udhibiti wa hiari wa misuli.

Video hiyo inamuonesha mwanamama huyo akiwa katika harusi ya mwanaye, Zak Poirier, ambaye kwa kushirikiana na ndugu yake mwingine walimnyanyua mama yao ili kucheza muziki. Taarifa yake iliripotiwa na vyombo vingi vya habari duniani huku watu wengi wakielezwa kufurahishwa na kitendo hicho.

Inaelezwa kuwa mama huyo aligunduliwa na ugonjwa huo muda mfupi kabla mwanaye Zak kuhitimu shule ya sheria. Hivyo, ili kukamilisha hatua nyingine muhimu katika maisha yake, aliweka dhamira kwamba ugonjwa huo unaomtesa mama yake hautaathiri furaha yao siku hiyo.

Kwa taarifa hizo, tumejiridhisha kuwa picha hizo ni halisi lakini taarifa zinazoambatana nazo si za kweli kwani hazimuoneshi Celine Dion kama inavyosambazwa.
maisha hubadilikakwa kwa kasi, miaka 30 maisha ya mwanadamu huweza kubadilika kabisa.
Hata Madonna ukimwona leo huwezi kuamani kuwa ndiye yule aliyekuwa moto sana enzi hizo. Nilimwona Madonna kwenye TV siku moja akiwa anahojiwa akawa anaonekana kama kinyago, nadhani ni kwa sababu ya plastic Surgery iliyopitiliza. Ila cha ajabu ni kuwa Kyle Minogue ambaye alikuwa malaya sana enzi zake hizo akawa ananunua wanaume lakini bado mwili wake unaonekana kuwa fit sana hadi leo.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom