Duu labda kY ilihusika, huwezi jua.Next time usiende kwa watu.bila K Y,utaumia zaidi ya unavyopaswa kuumizwa.
JF inakufanya unaelewa yanayoendelea duniani, I m feeling sorry for jamaa though.
Bora ww ulipewa papuchi na mtaji juu, wenzio ata papuchi hatupewi na pesa tunatoa.
Bora ww ulipewa papuchi na mtaji juu, wenzio ata papuchi hatupewi na pesa tunatoa.
Una ID ya ujasiri kumbe hovyo tu. NDIO MKOME.Good thinking bro
Heri ya mwaka mpya wakuu
Huu mwaka umeanza vibaya sana kwa upande kwangu,Jana nimedhalilishwa sana, tena mbele ya mwanamke ambaye nampenda sana, am swimming in a pool of emotions hapa,pombe ndo imekua msaada kwangu! Wakuu nisiwachoshe sana kisa chenyewe kipo hivi
Baada ya kumaliza chuo ni kutafuta ajira bila mafanikio ilibidi nijiongezee, nikatafuta kamtaji tukapiga 'collabo' na mshkaji mmoja tukaenda kulima Morogoro, mambo hayakua poa maana tuliishia kupata hasara, mwenzangu akavunjika moyo akakataa kurudia tena, he pulled out. Nikashindwa kulima mwenyewe kutokana na kimtaji kua kidogo,narudi dar naanzisha kibiashara kidogo cha kupata hata hela ya kula maisha yanasonga!
Kiufupi maisha yalikuwa magumu si utani, chumba kimoja uswahilini, ugali dagaa nini maisha yanasonga! Nina rafiki ambaye ni trainer kwenye gym moja kwa wenzetu 'ushuani' nikawa naenda kila jioni kufanya mazoezi! Huko ndipo nilipokutana na huyu bidada
Ni kama zaidi ya mwaka tangu nikutane na huyu mwanamke gym hapo,ni mwanamke mrembo kwelikweli,tunaanza zoeana taratibu(I was helping her with her trainings). Ikafika mahali akanizoea sana yaani nisipoenda gym na yeye haendi(quite became her 'un official' gym trainer!) Mahusiano yetu yalikuwa 'strictly' zoezi tu hakuna kingine! Sikuwahi kupata hata hisia za kimapenzi na huyu mwanamke maana nilijua fika I had no chance at all, same people different world's, mwanamke wa kishua full kubadili magari na mimi mtoto wa uswahilini wapi na wapi bana.
Kiukweli nikawa nakula kwa macho, nikawa najisemea 'wakubwa wanafaidi', basi maisha yakasonga akazidi kunizoea mpaka akataka kujua ninapoishi, baada ya kuwaza na kuwazua nikaona sina cha kupoteza nikamwambia ukipata nafasi karibu, siku si siku huyu mwanamke akatia maguu uswazi, akapaki mkoko wake mahali tukaanza kupiga one two mdogo mdogo mpaka ghetto, si unajua tena uswazi njia za Magari ni kama bikra wodi wa wazazi, tukafika ghetto akasindikizwa na misonyo ya kina halima(hii ni kikawaida sana huku kwetu)
Alikaa kama lisaa hivi tukaongea mengi sana kuhusu maisha,nika mfowadia CV yangu akaahidi kunitafutia ajira na nini, kiufupi huyu mwanamke akaja kua kama ndugu yangu hapa mjini,kanasaidia mengi sana na nilimuheshimu kupita Maelezo, akaja niletea vitu vingi tu,(TV, fridge ndogo, kabati la nguo n.k) kwa madai kwamba alikua navyo mwake stoo havitumii, kiufupi nilimchukulia kama Dada yangu(she is 28) wa hapa mjini! Akaja kuniambia nitafute project nzuri she will inject some money kwa makubaliano ya kuja kurudisha mambo yakikaa sawa, kweli bana nikampa idea ya kulima mkuranga akanipa 2.6M huku akiniambia take your time mambo yakijipa utanrudishia.
Kiufupi baada ya muda tulianza kufanya mapenzi, yeye ndo alianzisha haya mambo maana kiukweli mimi sikuwa na ujasiri hata wa kumtokea jinsi nilivyokuwa namuheshimu. Mara nyingi tulilala hotel na kuna siku alikuwa anakuja uswazi huku! Baada ya kama miezi mitatu, akanipotezea mazima, hapokei simu yangu wala kujibu text zangu! kabisa! For no reason, nikitumia namba nyingine anapokea anasema nimuache, roho ikaniuma sana baada ya muda nikakubali matokeo
Tar 31 DEC nakumbuka nikapokea hela ya mazao niliyopanda, nikamkumbuka sana huyu Dada, mpaka machozi yakatoka, sielewi nimemkosea wapi! Nikawa zangu ndani tu mpweke napiga mtungi, midaa ya SAA 6 kasoro nikampigia sana simu hapokei, kama Mara 14(was high kiasi), nikamtumia sms ndefu tu mwisho nikamwish new year!
Jana asubuhi kanipigia, tukaongea fresh tu akaniomba niende kwake tukaongee vizuri, nikajua hii siku itakuwa nzuri sana, nikapate majibu kwanini alikuwa kimya, nimpe taarifa nzuri ya mradi alioniwezesha, akanielekeza kwake Kawe(the entire time nilikuwa sipajui kwake japo aliwahi kuniambia anakaa na mdogo wake), nikajikoki nikatia maguu, nyumba geti mbili, gallery ya magari, swimming pool dah kweli watu wanaishi wengine tunasindikiza, kuingia ndani bidada amevaa t shirt ndefu tu, mtako huo(damn i miss the old times).. Akanipa juice, usoni ana ka u serious flani hivi, akili yangu inaniambia something is not right hapa, sijakaa sawa kikatokea kijibaba old school, kitambi kilee, kinene kama mtoto wa tembo, ndani ya pensi na vest, nikakisalimu kikakausha, wakuu yani hapo jasho linanitoka kama nimefanya cardio Masaa ma2 non stop!! Juice haishuki tena, akili INA reflect yule mlinzi pale nje na ile sura yake ya kufa, kibaba kipo busy kinasoma gazeti.
Mdada hapo kaondoka sebuleni,nikasema hili disco kaingia Masai hapa, baada ya kama dakika tano kijibaba kikafoka 'nyi ndo mnasumbua wake za watu?'
Yani hapo nimekua mdogo si utani, nikamwambia hapana, akainuka kunifata,akashika simu yangu akapigiza chini huku anafoka 'pumbavu, mnasumbua watu wamelala na visimu vyenu vya ovyo' bidada akawa kaja sasa. Mi npo bize naokota okota ka 'tecno' kangu.
Kijibaba kikashout 'TOKA HAPA MBWA WEWE' dah, nikasepa zangu mdogo mdogo! Sijawahi jiskia down kiasi kile,sijamtafuta tena huyu mwanamke, Jana nimelala bar,ogopa sana kudhalilishwa mbele ya mwanamke unayempenda! Nina maswali kama mia hapo sipati majibu yake, my heart is still weak, I fell in love, was hoping she'll come back someday!!!
Ngoja nijisogeze bar ya karibu hapo!!