Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Mwanaharakati na kada mpambanaji wa CHADEMA ndugu Steven Moses atoweka katika mazingira ya kutatanisha wilayani mufindi (Mafinga) katika Jimbo la Mafinga lipatikanalo mkoani Iringa.
Siku ya jumatatu wakati anatoka katika zoezi la CHADEMA ni msingi alitekwa na watu ambao hawakujulikana.
Binti mmoja kutoka eneo la bar inayoitwa aliweza kumpigia simu dadaake wa STEVEN majira ya SAA kumi akimweleza kwamba Steven Moses alitoka na mmewe, lakini alipotakiwa kutoa taarifa zaidi binti huyo alisema hawezi toa namba za mmewe ambaye yupo na Steven.
Dadake huyu pamoja na mke wa Steven walifika katika kituo cha Polisi cha Mafinga na kutoa maelezo sambamba na kupewa RB no *MFG/RB/591/2019* ya Tarehe 21/02/2019
Cha kushangaza polisi waliwatuma Dadake na mkewe wa Steven kwamba waende eneo hilo la Bar wakapige simu wakiona MTU anapokea simu ndipo watoe taarifa ili polisi wakamkamate, bahati mbaya namba ya mtu huyo haikupatikana tena mpaka dakika hii.
Hata hivyo siku NNE kabla ya tukio, mdogo wa bwana Steven , ajulikanae kama Martin, Alipigiwa simu na Balozi wa mtaa wao akamwambia amepewa maelekezo na Mbunge wa jimbo hilo aweze kumpata Steven Ng'owo na kumfikisha kwake kwa gharama yoyote ile, hivyo kwakuwa Balozi huyo anaheshimiana na Babu take Steven mzee Ng'owo, akatumia nafasi hiyo kutoa tahadhari kwamba Steven aachane na harakati za siasa jimboni hapo kwani zitamwangamiza kwakuwa anatafutwa kwa gharama yoyote.
Pamoja na hayo, mkewe na Steven siku tatu baadae aliitwa kwa simu jirani na eneo lake la kazi na MTU aliyejitambulisha kama askari mpelelezi wa kituo cha polisi cha Mafinga. Akamtaka ampatie simu yake, mke wa Steven alikataa na baadae askari huyo alimtajia namba aipige, kuangalia ni simu ya mumewe ndipo wakamwambia aseme yupo wapi, akawaambia yupo Dar es salaam maana alifahamu fika mumewe anawindwa kisiasa.
Leo tarehe 21/02/2019 ni siku ya tatu tangu Steven atoweke, mkewe na dadake walifika kuripoti tena kituoni hapo; wamemkuta askari huyo mpelelezi aliyesema, alijua lazma wataenda, akawaambia *Ndugu yao hajafa yupo salama atarudi, hivyo watapigiwa simu polisi.*
Jambo hilo linapelekea hofu kubwa katika familia na jamii ya wana Mafinga kwani inaonekana haya yote ni kutokana na maelekezo ya mbunge huyo.
Hata hivyo jeshi la polisi halijataka kuonyesha ushirikiano wa kusema wala kuonyesha alipo Steven.
Swala hili lina sura za kisiasa, ari ya familia inalitaka jeshi la polisi kumrejesha ndugu yao akiwa salama salmini sambamba na kuliomba kufanya kazi kwa weledi bila kufuata maagizo ya kisiasa hasa mbunge wa Mufindi, ya kumkamata mtu ambaye hana tuhuma zozote za jinai.