Historia iko wazi na haijawahi kukanushwa,Ccm waliukataa mfumo wa vyama Vingi na waliukubali kwa shinikizo la baba wa taifa...Mwalimu nyerere....ila nafsini mwao hawakuwa tayari!
Na hii imeendelea kujidhihiri kila rais anayekaa madarakani.
Kimsingi, hata nyerere aliwahi kulalamika kwamba kila kitu alichokipangilia na kukitolea hoja nchi hii,baada ya nyerere kutoka madarakani,Ccm walikitupa,sembuse vyama vingi!!
Kwa kuwa vyama hivi vimekuwa kero kwao japo sheria ya kuvianzisha ilitungwa na bunge lililokuwa na wabunge 100% Ccm,basi namshauri mwakyembe waziri wa sheria kwamba,apeleke muswada(kama ana ubavu)akavifute kwa kuwa bunge hili asilimia mia wanaokaa ni Ccm baada ya ukawa kuwaachia ukumbi