INAFURAHISHA, INASIKITISHA!!
Ni mwaka wa pili unaisha sasa tangu serikali ya awamu ya tano iingie madarakani
Bado mh anatafuta watu wa kufanya nao kazi. kila anayemteua baadaye kidogo anamuona mzigo
Hata wale wa karibu naye ni kama wamepigwa ganzi. wanaogopa kutenda wasije wakamkwaza mkuu. kila kitu anafanya yeye
Huwa najiuliza; Hivi kweli katika watanzania woote milioni 50 inachukua miaka 2 kupata japo watu 200 wa kufanya nao kazi??
kama ndio basi watanzania tu viumbe wa ajabu sana. pengine ile slogan ya elimu elimu elimu ya mtu flani ilikuwa sahihi?? Au possibly tatizo lipo kwa anayetuteua, ana akili nyingi sana za kung'amua udhaifu wa mteule wake!!?