Mwafrika ni nani?

hatuwezi kuwaita waarabu wa afrika kaskazini waafrika 100% (indigenous africans) wakati kwenye matabaka ya watu wa bara la afrika wanaitwa afro-asiatic kifupi ni waasia.
 
hatuwezi kuwaita waarabu wa afrika kaskazini waafrika 100% (indigenous africans) wakati kwenye matabaka ya watu wa bara la afrika wanaitwa afro-asiatic kifupi ni waasia.
mimi napata ukakasi zaid ninapomwazia Beyonce na Lil Wyne je wao najua sio wazungu pia hawajazalia Africa! wao je wajiiteje sasa! nisaidie hapo mkuu!
 
mimi napata ukakasi zaid ninapomwazia Beyonce na Lil Wyne je wao najua sio wazungu pia hawajazalia Africa! wao je wajiiteje sasa! nisaidie hapo mkuu!
wale ni waafrika kiasili biologically lakini legally wanatambulika kama wamarekani though beyonce ni half ni kama wewe ukienda kuomba uraia na ukazaa mtoto wako huko ufaransa utakuwa mfaransa kisheria pamoja na mwanao lakini nyie sio wazungu (indigenous)
 
na je? hivi wale waafrica wanaoishi marekani tena weusi kabsa ndo inakuaje, yan tuwaweke katika kundi lipi mana wanajiita black americans.
 
Hivi mwafrika ni nani? Ninachojua mtu yeyote aliyezaliwa Tanzania ni mtanzania. Vivyo hivyo mtu aliyezaliwa Afrika ni mwafrika, lakini dhana ya uafrika huwa inaambatanisha na rangi ya ngozi, yaani WEUSI/ COLORED?
...Hili swali linasumbua vichwa vya watu wengi, wasomi magwiji wakiwamo. Ila, wasomi kadhaa wanakataa/hawakubali kama suala la ngozi -je, ndio race, kwa maana ya hapa?- linahusika. It is more than that.

...Pengine mtu aliyezaliwa na anaishi Afrika, akarithi njia au namna fulani za maisha ya wanaoishi Afrika, ni mwafrika.

Je, ni halali kumwita mtu wa Libya, mwenye ngozi nyeupe kuwa ni mwafrika!?

...Tatizo lililopo kwenye kuchambua swali hili ni kuwa, mtu wa Libya ni mwarabu, ambayo ni race. Sasa, huyu anaishi kwenye bara linaitwa Afrika, yeye tunamtambuaje? Ndio maana, ukitaka kuitambua Afrika kama sehemu inayofahamika kwa race, inaleta shida. Jibu ni kuwa, mLibya ni mwafrika, kwa maana ya kwamba, kuwa mwafrika its more than race.

...Nimshukuru mtanganyika wa kweli, kwa kuboresha mjadala, baada ya kutoa reference ya magwiji waliojadili hili suala. Kama alivyoshauri, tafuta maandiko yao, uyasome.

...Hapa, kuna sypnosis ya kitabu cha Kwameh Appiah kinachoitwa "In My Father's House", ambayo inatoa mwanga kidogo kwenye swala hili.

NB: Nimesahihisha post niliyoinukuu ili mtiririko uwe sawia.
 
na je? hivi wale waafrica wanaoishi marekani tena weusi kabsa ndo inakuaje, yan tuwaweke katika kundi lipi mana wanajiita black americans.
...Kuna makundi makubwa mawili ya watu weusi wanaoishi Marekani. Kuna wale waliochukuliwa utumwa, au maarufu kama black americans, na african diaspora.

...As far as i know, black americans si waafrika bali waamerika, ila, asili yao ni Afrika. Kama ambavyo watu weupe kadhaa -white americans- pale ambao ni waamerika, asili yao ni Ulaya.
 
Kwa hiyo mkuu ukisema hivyo utaconclude vipi kwa hili swali la who is an African??
Je utaangalia rangi?? Maana rangi nyeusi ipo moja tu duniani haijalishi inapatikana wapi kwa sasa lakini asili yake ukitrace utagundua ni Afrika
Au utaangalia nationality?? Kwa maana ya mtu yeyote aliezaliwa Africa ni mwaafrica regardless his/her colour??
Dah hili swali linanipaga taabu sana nakumbuka wakati nasoma literature kulikua na swali kua what is African literature??
So hivi vitu viwili huwa vinanipa taabu sana kuvielezea hasa mpaka mtu akuelewe
 
Mm mwenyewe nachanganyikiwa kabisa kuna watu wako hawana tofauti na wazungu kabisa South Africa ila wamezaliwa hapo hivi na wale wa Africa
 
habari wakuu,

Naomba radhi kama mada hii nayouliza imeshawahi kujadiliwa au la, kikubwa hapa napata wakati mgumu sana ninapo jiuliza hili jambo

Hivi mwafrika ni nani?

Ninachojua mtu yeyote aliyezaliwa Tanzania ni mtanzania

vivyohivyo mtu aliyezaliwa Afrika ni mwafrika,
lakini dhana ya uafrika huwa naiambatanisha na rangi ya ngozi, yaani WEUSI/ COLORED
JE, ni harali kumwita mtu wa Ribya mwenye ngozi nyeupe kuwa ni mwafrika!?

naomba kuwasilisha!

Naungana na mtoa mada kwa kuongezea swali. Mtu akisema yeye ni muafrika basi watu wanachukulia kuwa ni mtu mweusi, sasa Afrika kama bara ina nchi 54 miongoni wake kuna nchi za kaskazini ambazo wakazi wake ni waarabu (Libya,Tunisia , Algeria, Sudan, Egypt, Morocco) sasa nashindwa kujua ikiwa Afrika ni ya watu weusi hawa wamefikaje na weusi walienda wapi? Je falme za kale za Misri, Morocco, Algeria, Sudan, Libya zilikuwa za watu weusi ama waarabu?

Zingatia: Kimaendeleo IMF, WB na nchi wahisani wanasema afrika ni masikini sana wakimaanisha nchi za kusini mwa jangwa la sahara (sub Saharan Africa) ambazo si za waarabu maana wao wapo kaskazini.

wanaJF hebu tujadili nini maana ya mwafrika, asili yake, maana ya neno "Afrika" na historia ya waarabu wa Africa kaskazini, Je asili yao ni urabuni (barani Asia) kama wenzao wahuko? Maana weusi wanatambulika duniani kote kuwa na asili ya Afrika.
 
Uafrica unatokana na wewe kuwa katika bara la africa,hata mlibya nae ni mwafrika as anapatikana na bara la AFRICA,uafrika hauhusiani na rangi,though wanadamu wengi wanaopatikana Africa ni weusi
 
Kwa hiyo mkuu ukisema hivyo utaconclude vipi kwa hili swali la who is an African??
...Conclusion ni ngumu. Ila, huyo diaspora ndio mwafrika, huyo mwengine sio! Sababu, zaidi ya rangi ya ngozi yake, hamna kitu kinamweka karibu na Afrika.

Je utaangalia rangi?? Maana rangi nyeusi ipo moja tu duniani haijalishi inapatikana wapi kwa sasa lakini asili yake ukitrace utagundua ni Afrika
Au utaangalia nationality?? Kwa maana ya mtu yeyote aliezaliwa Africa ni mwaafrica regardless his/her colour??
...Unajua, kama ni suala la rangi nyeusi, wapo wengine. Kuna wale kule Australia na New Guinea.

...Nationality inaweza kutupunguzia tatizo hili, ndio! Lakini, nayo kama haitoshi hivi. Vipi mswahili akiwa na uraia wa Finland, tutamwita mzungu?

...Hili suala ni gumu! Maana, mzungu hutambulika kwa rangi ya ngozi na bara Ulaya, lakini yule wa Zimbabwe au South Africa au Namibia ni mwafrika. Sasa, dah....sijui mimi nikilowea Ujerumani uzao wangu huko utaitwa wazungu? Ngumu yaani. Ila, najua wataitwa waJerumani.

...Nadhani, Afrika inajikuta katika sehemu kama inayojikuta Amerika. Kwamba, kuna watu wanaweza semwa ni wenye asili ya hapo. Ila, kuna wengine ambao asili yao si ya hapo. Lakini, wote waafrika.

Dah hili swali linanipaga taabu sana nakumbuka wakati nasoma literature kulikua na swali kua what is African literature?? So hivi vitu viwili huwa vinanipa taabu sana kuvielezea hasa mpaka mtu akuelewe
...Hiyo ilikuwa sio ngumu sana, kwa maana ukishawajui kina Chinua, Ngugi, et al. basi mbele kwa mbele.

...Ni vigumu, mie najaribu kuvielewa pia.
 
...Conclusion ni ngumu. Ila, huyo diaspora ndio mwafrika, huyo mwengine sio! Sababu, zaidi ya rangi ya ngozi yake, hamna kitu kinamweka karibu na Afrika.

...Unajua, kama ni suala la rangi nyeusi, wapo wengine. Kuna wale kule Australia na New Guinea.

...Nationality inaweza kutupunguzia tatizo hili, ndio! Lakini, nayo kama haitoshi hivi. Vipi mswahili akiwa na uraia wa Finland, tutamwita mzungu?

...Hili suala ni gumu! Maana, mzungu hutambulika kwa rangi ya ngozi na bara Ulaya, lakini yule wa Zimbabwe au South Africa au Namibia ni mwafrika. Sasa, dah....sijui mimi nikilowea Ujerumani uzao wangu huko utaitwa wazungu? Ngumu yaani. Ila, najua wataitwa waJerumani.

...Nadhani, Afrika inajikuta katika sehemu kama inayojikuta Amerika. Kwamba, kuna watu wanaweza semwa ni wenye asili ya hapo. Ila, kuna wengine ambao asili yao si ya hapo. Lakini, wote waafrika.

...Hiyo ilikuwa sio ngumu sana, kwa maana ukishawajui kina Chinua, Ngugi, et al. basi mbele kwa mbele.

...Ni vigumu, mie najaribu kuvielewa pia.
Kwa hiyo mkuu ugumu wa hii kitu unatokana na nn?? Yaani kwa nini iwe vigum kiasi hichi kumtambua mwafrika ni nani kuliko watu kutoka mabara mengine??
 
Kwa hiyo mkuu ugumu wa hii kitu unatokana na nn??
...Unatokana na kwamba hamna tafsiri rasmi ya nani ni mwafrika na nini ni uafrika.

...Hamna jibu lililo straight forward. Kwamba Afrika ni bara, je watu wote wanaoishi humo ni waafrika? Kipimo ni nini? Je, kuwa mweusi ndio uafrika? Je, weusi unapimwaje?

...Ndio maana ukitaka kuelezea kitu kama hicho, inabidi utoe ufafanuzi au tafsiri, halafu uendelee na maelezo.

Yaani kwa nini iwe vigumu kiasi hichi kumtambua mwafrika ni nani kuliko watu kutoka mabara mengine??
...Naomba nikujibu kwa kukuuliza. Je, unaweza kumfahamu mwamerika? kwa maana ya mMarekani, kama hamna utambulisho wowote?

...Je, ukipishana na mtu mwenye mwonekano wa kichina, utasema ni mChina? Utakuwa na uhakika? Vipi kama akikwambia yeye ni mAustralia? Uzuri wake, asia ni race.

...Tatizo la uAfrika ni kutokuwa race, bali mchanganyiko wa races. Kama Amerika ilivyo na races kadhaa.

...Negro ni jina ambalo lingeweza kufaa, ila lilichafuliwa na utumwa na ubaguzi. Ni offensive kumwita mtu nigger, Marekani.

...Tatizo majina ya races yametokea kwa wazungu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom