Siku moja nipo zangu Gheto, Mara waaah!! Simu
ikaita, kamvua kalikuwa kamenyesha kiubaridi cha
kutosha.
Kucheki ni Jirani yangu, binti fulani amejaaliwa
haswa.
"SIDE upo kwako?" Nikamwambia nipo.
"Nakuja sasa hivi kukupa ROMANSI"
Ebwana eeh nikashtuka.... Sikuamini nimeokota
dodo jangwani. Nikajikoki nikatandika kitanda fres
nikasema leo ndio leo. Na hiki kibaridi napewa
romansi
He!! Mara akaingia amevalia jinsi na mkoba wake
begani.
"Nasikia ROMANSI eti kodi imepanda kuanzia
mwezi ujao tunalipa elfu 30
He! Kamaliza huyooo kaondoka.
# Dah yaani kumbe anachapia badala ya RUMOURS
(tetesi) yeye anasema ROMANSI.....
# Nilikaa wiki nzima simsemeshi......