Muswada wa Huduma za Habari: Nape amshukia Zitto, Zitto naye amjibu

Habari ya Mujini

JF-Expert Member
Dec 22, 2013
2,517
1,044
ZITTO AACHE UNAFIKI

Na Nape Nnauye (MB)

NAZIONA juhudi kubwa za Mbunge wa Kigoma Mjini Ndg. Zitto Kabwe kujaribu kupotosha jamii kwa kutosema ukweli kuhusu masuala kadhaa yahusianayo na Muswada wa Huduma za Habari, 2016.

Kwa kawaida mimi huwa sio mtu wa kujibu hoja zinazotolewa kinafiki na kioga kama alivyofanya rafikiangu Zitto Zuberi Kabwe. Kwa hali ya kawaida ningeweza kumpuuza kabisa, lakini kwa hili uvumilivu wangu kwa kiwango hichi cha unafiki umefikia ukingoni. Hivyo nitalazimika kujibu baadhi ya hoja.

Nimesoma kwa masikitiko sana sana, makala ndefu kidogo aliyoisambaza ndugu yangu na mwanasiasa kijana mwenzangu Ndg. Zitto Zuberi Kabwe kuhusiana na alichodai ni hatari ya Mswaada wa Huduma za Vyombo vya Habari 2016.

Muswada huu uliochapishwa na kuwekwa hadharani tangu Septemba, 2016, pamoja na mambo mengine unakwenda kuhitimisha safari ya zaidi ya miaka 20 ya wadau wa habari nchini kuwa si tu na sheria nzuri itakayoratibu kazi na kulinda maslahi yao, bali sheria inayoitangaza rasmi kazi hii kuwa taaluma kamili.

Hata hivyo, akiyatumikia maslahi yasiyo wazi kwa sasa, akiongozwa na unafiki wa hali ya juu kabisa kupata kuushuhudia kwake, na baada ya kujaribu kuzuia muswada huu kwenye Kamati ya kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii na juhudi zake hizo kushindwa vibaya. Mbunge mwenzangu Zitto Kabwe ameanza kupayuka mitandaoni akieneza uzushi na kila aina ya uongo na upotoshaji kuhusu muswada huu.

Inahitaji ujasiri wa kinafiki kuandika aliyoyaandika mwanasiasa mwenzangu kijana Zitto Zuberi Kabwe. Licha ya kuwa nimekuwa nikimheshimu kwa muda mrefu, na bado namheshimu na kumpenda kama kijana mwenzangu, unafiki huu wa kutumikia masilahi binafsi umenistua sana.

Kama nilivyosema nitayajibu baadhi ya madai yake kama ifuatavyo:-

#1. Hoja ya Kushirikishwa wadau:
Zitto anajaribu kujenga picha kuwa muswada huu haukushirikisha wadau. Ndugu yangu huyu, huku akiwa anajua kuwa katika utungaji wa mswaada kuna hatua mbili za kutoa maoni.

Hatua ya kwanza ni pale ambapo serikali inapokuwa inatengeneza mswaada husika kabla ya kuupeleka kwenye vikao vya kiserikali kwa hatua za kuupitisha wadau HUSHIRIKISHWA ili kutoa maoni yao. Na kwa mswaada wa Huduma za Vyombo vya Habari ,2016 WADAU wameshirikishwa tena na ushahidi wa maandishi wa ushiriki wao na maoni yao UPO.

Hatua ya pili ya utoaji maoni huwa ni baada ya mswaada kusomwa mara ya KWANZA bungeni, Mswaada husika hukabidhiwa kwa Kamati husika ya Bunge, na ukishakabidhiwa huwa ni waraka huru kwa umma kuusoma na kutoa maoni yao( public document) kwa Kamati ya Bunge.

Hili pia limefanyika mpaka hatua ya wadau kuitwa na kuja Dodoma ambapo waliomba mbele ya Kamati wapewe muda wakamilishe kazi ya kusoma na kutoa maoni yao. Na Mwenyekiti wa Kamati Ndg. Peter Serukamba(mb) kwa uamuzi wa Kamati ya kudumu ya Bunge wakaamua kuwaongezea muda wadau kwa wiki moja kukamilisha kazi hiyo, shughuli inayoendelea sasa.

Ndg. Zitto kwa makusudi aliamua kujaribu kuzuia hatua hii ya pili isifanyike bila mafaniko.
Hoja yake hiyo ilianguka mbele ya Kamati tulipoonesha ushahidi wa wazi na wa nyaraka kuwa wadau wakuu wote si tu walishiriki katika hatua za ndani ya Serikali kutoa maoni na sasa watashiriki zaidi katika hatua hizi za Bunge bali sehemu kubwa ya maoni yao yaliingizwa katika muswada wa sasa. Zaidi ya asilimia 90+% ya maoni ya wadau yamezingatiwa katika Mswaada huu.

Alipoona kashindwa kabisa akaamua kuondoka Dodoma akasafiri na kusambaza waraka wa kizushi ili kufurahisha waliomtuma badala ya kuchangia kuboresha mswaada husika.

#2. Hoja ya kulazimisha vyombo vya Habari nchini kujiunga na TBC:-
Zitto pia anaeneza uongo kwamba muswada huu unadhamiria kuvifanya vyombo vya habari hususani TV kulazimishwa kujiunga na TBC kwenye vipindi vyake.

Kwanza nina wasiwasi kama ameusoma muswada huu na kama ameusoma naanza kuamini hana muswada sahihi. Au ndio kaamua kutoa maoni akiongozwa na unafiki.

Hata hivyo hili tumelifafanua katika Kamati, kwa bahati mbaya hakuhudhuria ili kupata uelewa mpana. Mosi hakuna kifungu kama hicho katika muswada huu; pili, hakuna dhamira hiyo kwenye muswada huu; na tatu, serikali haina hata wazo hilo.

#3. Mitandao ya kijamii:
Zitto katika kutimiza malengo na maslahi yake, anapotosha kuwa muswada huu unakusudia kuzibana blogs na kutaja mitandao ya kijamii kama JamiiForums kuwa nayo itatakiwa kusajiliwa.

Mtu huyu ni wa kumwonea huruma. Bahati mbaya muswada huo hauna mamlaka wala nia hiyo. Kifungu cha 3 cha Sheria kiko wazi kuwa usajili utahusu magazeti na majarida na machapisho yao ya mitandaoni(magazeti mtandao ya magazeti hayo rasmi na sio mitandao yote au mingine ya kijamii kama anavyopotosha).

Na kwakuwa nakala ya Mswaada huu ina tafsiri ya kiingereza na Kiswahili sitaki kuamini kuwa Zitto hakusoma hili, au waliomtuma hawakusoma vizuri hili.

Zitto anakwenda mbali kudai wachangiaji kama wa jamiiforums watatakiwa wafanyiwe ithibati! Bila shaka mwenzetu huyu anajadili muswada mwingine kabisa.

Muswada huu hauhusu wala hakujapata kuwa na fikra za kudhibiti au kuratibu mitandao ya kijamii na kuwataka watumiaji wa mitandao hiyo eti wasajiliwe. Huu ni upuuzi mwingine wa kupuuzwa.

#4. Ipo hoja ya Waziri kupewa mamlaka kuagiza chombo chochote kutangaza jambo lenye umuhimu kwa umma:
Katika hili pia tumsamehe kwa sababu hahudhurii vikao vya Kamati wakati wa mijadala hii. Hili limejadiliwa kwa kina na wahusika kuelewana. Hakuna kifungu kinachompa mamlaka hayo Waziri.

Bali kifungu kilichopo kinaipa fursa Serikali kuvishauri/kuvielekeza(Govt MAY) vyombo vya habari kuungana pamoja kulinda maslahi ya Taifa kunapokuwa na jambo la muhimu kama vile nchi kuwa VITANI au majanga makubwa. Zitto kama kijana wa Kitanzania kama haoni umuhimu wa hili basi hakuna namna nyingine ya kumsaidia.

#4. Kwamba muswada unampa Waziri wa Habari majukumu ya kutoa masharti kwa kazi za vyombo vya habari na kwamba anaweza kuamua gazeti lichapishwe habari aitakayo:
Hili ni eneo lingine linalothibitisha kuwa hapa tunajihusisha na mtu mwenye malengo ya hatari sana na anayejaribu kuweka matazamio yake katika jambo la muhimu kama hili.

Muswada huu hauna kifungu hicho zaidi ya Waziri kupewa uwezo wa kisheria, kama ilivyo katika sheria nyingine, kutunga kanuni za kutekeleza sheria hii. Hili nalo Zitto hataki!

#5. Zitto anasema muswada huu unampa mamlaka Waziri kuzuia chapisho au kitabu fulani kisisambazwe nchini:

Ni kweli muswada umetoa mamlaka hayo lakini Zitto ameamua kutosema ukweli wote.

Muswada unampa Waziri mamlaka hayo si kwa kila jarida au kitabu bali yale tu ambayo yamedhihirika kuchapisha habari huku yakivunja sheria za nchi. Kama Zitto anafikiri nchi yetu itaruhusu majarida yanayotaka kuhamamsisha vita na uvunjifu wa amani nchini, ajue hakuna nchi inayoruhusu mambo hayo.

#6. Zitto anazungumzia kuwepo kwa vifungu vya uchochezi akitoa tafsiri kuwa wabunge wa upinzani watabanwa:
Kwanza katika hili lazima ijulikane kuwa kwa mujibu wa mikataba ya kimataifa ukiwemo Mkataba wa Kimataifa Juu ya Haki za Kisiasa na Kiraia wa mwaka 1966, masuala yote yanayohusu kusababisha athari kwa usalama wa taifa ni ukomo unaokubalika wa uhuru wa habari (allowable restriction to press freedom).

Uandishi wa habari kama taaluma nyingine unabeba haki na wajibu. Moja ya masuala ambayo waandishi wanapaswa kubeba wajibu kwayo ni kutosababisha hatari kwa usalama wa Taifa kwa kusababisha vurugu, chuki katika jamii(uchochezi). Hivyo katika kuweka vifungu hivi muswada umezingatia ukweli huo wa sheria za kimataifa.

Hata hivyo ieleweke, tofauti na Zitto anavyopotosha, sheria hii imekwenda mbali zaidi kwa ruhusu wananchi na watu wengine kuikosoa Serikali na utekelezaji wa sera zake.

Sheria inasema haitakuwa uchochezi kama mtu atatoa maoni yake kwa minajili ya kukosoa makosa katika Serikali, makosa katika utekelezaji wa sera (kifungu cha 49[2]). Huu ni uhuru mkubwa sana kuwahi kutamkwa na sheria.

Mwisho, namshauri Ndugu Zitto Kabwe apunguze kuishi kinafiki. Akasome tena muswada huu na alete hoja zake kwenye Kamati ya Bungeni zijadiliwe, aache kupotosha umma mitandaoni na aache kujiweka karibu zaidi na vibaraka.

Muswada huu, narudia tena, unakwenda kuifanya sekta ya habari kuwa taaluma inayoheshimika. Ni muswada unaokwenda kuipa heshima taaluma hii na kila mmoja wetu awe tayari kwa mageuzi haya.

Katika kuifanya fani hii kuwa taaluma tunafahamu kuwa wapo waliozoea mambo ya kale na yale yale na kwamba watapinga; tunafahamu wapo watakaoona wanahabari waliowaajiri watadai maslahi zaidi na wapo watakaoona fani hii kuwa taaluma kamili watashindwa kuitumia kwa maslahi yao- wanahabari na wananchi tuungane kuwakataa wenye maslahi binafsi katika hili.

Tuungane kutoa maoni ili tuwe na muswada bora zaidi na utakaoifanya sekta ya habari kuwa na mchango mzuri zaidi kwa nchi yetu.

Kwasasa niishie hapa, lakini nitaendelea na awamu ya pili hata ya tatu ya ufafanuzi ikibidi. Uzalendo katika hili utashinda unafiki na utumwa wa kubeba mawazo ya watwana wachache walizoea vya kunyonga ambavyo kuchinja kwao msamiati!

----------------------------------
Majibu ya Zitto Kabwe kwa Nape Nnauye
----------------------------------

Majibu yangu Kwa HOJA za Nape Nnauye kuhusu muswada wa Huduma za habari, 2016

Ndugu yangu Nape Nnauye amejibu andiko langu nililolitoa Jana kuhusu muswada tajwa. Kama ilivyo ada ya Siasa za kijinga jinga Nape amejibu andiko langu Kwa kunishambulia binafsi na kuweka Hoja zake mbalimbali. Mimi sitamjibu Nape namna yake maana wenye busara wametufunza ' when they go low go high '.

Nitajibu Hoja za Nape Na sitamjibu Nape. Hata kwenye andiko langu sikutamka neno Nape Nnauye kwani Siasa zangu sio Siasa za mtu bali za masuala. Sitahangaika Na mtu bali Hoja ili kujenga.

1. Hoja ya Kushirikishwa wadau
Nape anasema:
Katika utungaji wa mswaada kuna hatua mbili za kutoa maoni.

Hatua ya kwanza ni pale ambapo serikali inapokuwa inatengeneza mswaada husika kabla ya kuupeleka kwenye vikao vya kiserikali kwa hatua za kuupitisha wadau HUSHIRIKISHWA ili kutoa maoni yao. Na kwa mswaada wa Huduma za Vyombo vya Habari ,2016 WADAU wameshirikishwa tena na ushahidi wa maandishi wa ushiriki wao na maoni yao UPO.

Hatua ya pili ya utoaji maoni huwa ni baada ya mswaada kusomwa mara ya KWANZA bungeni, Mswaada husika hukabidhiwa kwa Kamati husika ya Bunge, na ukishakabidhiwa huwa ni waraka huru kwa umma kuusoma na kutoa maoni yao( public document) kwa Kamati ya Bunge.

Hili pia limefanyika mpaka hatua ya wadau kuitwa na kuja Dodoma ambapo waliomba mbele ya Kamati wapewe muda wakamilishe kazi ya kusoma na kutoa maoni yao. Na Mwenyekiti wa Kamati Ndg. Peter Serukamba(mb) kwa uamuzi wa Kamati ya kudumu ya Bunge wakaamua kuwaongezea muda wadau kwa wiki moja kukamilisha kazi hiyo, shughuli inayoendelea sasa.

Majibu ya Hoja hii:

Kanuni za Bunge(kanuni ya 84 ) zinataka kwamba Muswada ukishasomwa Kwa mara ya kwanza Bunge lifanye MATANGAZO Kwa umma ili kuhakikisha kuwa umma unaelewa maudhui ya muswada na kuwezesha Wananchi kutoa maoni Yao. Muswada huu kwanza Bunge halikutoa matangazo yeyote (Kwa Taarifa tu Ni kwamba Hata Kamati ya Bunge ilishindwa kutoa photocopy nakala za uchambuzi wa muswada kutoka Kwa wanasheria wa Bunge Kwa sababu Bunge halina Fedha.

Bunge halina Fedha kutoa photocopy ya nyaraka za Wabunge kufanyia Kazi ). Wadau wote waliokuja mbele ya Kamati ya Bunge walitamka dhahiri kwamba wamepewa Taarifa ya kutokea mbele ya Kamati Siku 2 kabla ya vikao Na hivyo wameomba muda zaidi wa kutoa maoni Yao. Labda Ni kutokana Na uchanga wa shughuli za Bunge, Waziri anajenga Hoja kwamba Ushiriki ulianzia kabla.

Mtu yeyote anayejua namna Bunge linavyofanya Kazi atakwambia muswada Ni muswada pale ambapo umechapishwa kwenye gazeti la Serikali Na kusomwa mara ya kwanza Bungeni. Wadau wote waliiambia Kamati kwamba Kwa muswada huu Ndio walikuwa wanashirikishwa Kwa mara ya kwanza pale mbele ya Kamati.

Hivyo wadau hawakushirikishwa kwenye muswada huu tangu umesomwa Kwa Mara ya kwanza Bungeni. Kama Serikali ina ushahidi wowote ule kwamba kati ya Septemba Na sasa muswada huu umehusisha mdau yeyote waweke wazi uthibitisho huo. Nyaraka zinazoonyeshwa Na Serikali Ni za miaka ya nyuma kabla ya muswada kuwa muswada. Ushirikishaji unaanza rasmi pale muswada upo gazetted Na umesomwa Bungeni.

2. Hoja ya kulazimisha vyombo vya Habari nchini kujiunga na TBC
Nape anasema:

...hakuna kifungu kama hicho katika muswada huu; pili, hakuna dhamira hiyo kwenye muswada huu; na tatu, serikali haina hata wazo hilo.

Majibu ya Hoja:

Itakumbukwa kuwa muswada wa awali ulikuwa Na kifungu hiki Na wadau wakapiga kelele sana kukataa. Ukisoma muswada huu Kwa juu juu utaweza kuona kuwa kifungu hiki hakipo. Mtu mwenye dhamira ovu huficha huficha mambo yake. Kwenye muswada huu mambo mengi yaliyokataliwa Na wadau sasa yamewekwa kiujanja Kwa kuweka Mamlaka hayo Kwa Waziri mwenye dhamana ya Habari.

Serikali inaposea hakuna kifungu hicho haisemi kuna kifungu gani. Nitawaeleza kifungu kilichowekwa ambacho ndicho kitatumika na Waziri kufanya haya bila kuhojiwa Na mtu yeyote yule, kupitia kanuni.

Sehemu ya 7(1)(b)(iv) inatamka wazi kwamba Waziri anaweza kuagiza chombo chochote cha habari cha binafsi kutangaza habari Fulani au masuala Fulani yenye umuhimu kwa Taifa.

Serikali itatumia kifungu hiki kutekeleza jambo lile lile ambalo wadau walikataa kuwekwa sheria Siku za nyuma. Serikali italiweka Kwa mlango wa nyuma. Mbaya zaidi muswada unatamka wazi kwamba Waziri mwenye dhamana ataweka TERMS and CONDITIONS Kwa uendeshaji wa 'media houses'. Hivyo Hata wakifuta kifungu Hicho cha 7, bado Waziri kapewa Mamlaka makubwa sana ya kuamua Chombo cha habari kinaendeshwaji.

Ni dhahiri kwamba Waziri ama anajua haya au kawekewa vifungu ambavyo yeye binafsi hajui tafsiri zake lakini atashangazwa katika utekelezaji wa sheria. Kifungu cha 60(2)(a) ( Minister to make regulations for TERMS and CONDITIONS for OPERATIONS of licensed media house) inampa Mamlaka hayo Waziri kiasi ambacho ataweza kuendesha vyombo vya habari atakavyo yeye. Muswada huu unamfanya Waziri wa Habari kuwa Mhariri Mkuu wa Taifa.

3. Mitandao ya kijamii:

Mtu huyu ni wa kumwonea huruma. Bahati mbaya muswada huo hauna mamlaka wala nia hiyo. Kifungu cha 3 cha Sheria kiko wazi kuwa usajili utahusu magazeti na majarida na machapisho yao ya mitandaoni(magazeti mtandao ya magazeti hayo rasmi na sio mitandao yote au mingine ya kijamii kama anavyopotosha).

...Zitto anakwenda mbali kudai wachangiaji kama wa jamiiforums watatakiwa wafanyiwe ithibati! Bila shaka mwenzetu huyu anajadili muswada mwingine kabisa.

Muswada huu hauhusu wala hakujapata kuwa na fikra za kudhibiti au kuratibu mitandao ya kijamii na kuwataka watumiaji wa mitandao hiyo eti wasajiliwe. Huu ni upuuzi mwingine wa kupuuzwa.

Majibu ya Hoja:

Muswada uliopo mbele ya kamati ya Bunge unatoa tafsiri pana sana ya vyombo vya habari. Sehemu ya 3 ya Muswada inatamka chombo cha habari ni pamoja na gazeti, kituo cha radio na televisheni ikiwemo mitandao ya kijamii (online platforms).

Napenda umma wa Watanzania ufahamu kwamba muswada Ni wa Kiingereza. Muswada wa Kiswahili Ni Kwa ajili tu ya kuwezesha Wabunge wasiojua kiingereza kuweza kuelewa vifungu vya muswada. Muswada Ni wa Kiingereza, Ndio rasmi. Mahakamani hawatatumia muswada wa Kiswahili Bali muswada rasmi.

Tafsiri ya online platforms haikuwekwa kwenye muswada. Tafsiri ya media Ndio imeweka Hilo la online platforms. Naomba mtu yeyote aende Google Na kuandika online platform atapata tafsiri ni Nini. Nitsaidia kidogo hapa.

Social media is defined as “online interactions among people in which they create, share, and exchange information and ideas in virtual communities, networks and their associated platform”.

Serikali itatumia tafsiri hii ya kwenye muswada kubana mitandao ya kijamii. Hivi Watanzania mmesahau kesi ambazo Wananchi wanapewa kupitia sheria ya cyber crime? Hivi mnasahau kuwa Rais alisema anatamani mitandao ya kijamii Malaika washuke waizime? Malaika watashuka Kwa kupitia muswada huu. Muswada huu una nia ovu kabisa ya kukandamiza uhuru wa habari.

Pia...

"Ipo hoja ya Waziri kupewa mamlaka kuagiza chombo chochote kutangaza jambo lenye umuhimu kwa umma: Katika hili pia tumsamehe kwa sababu hahudhurii vikao vya Kamati wakati wa mijadala hii. Hili limejadiliwa kwa kina na wahusika kuelewana. Hakuna kifungu kinachompa mamlaka hayo Waziri.

Bali kifungu kilichopo kinaipa fursa Serikali kuvishauri/kuvielekeza(Govt MAY) vyombo vya habari kuungana pamoja kulinda maslahi ya Taifa kunapokuwa na jambo la muhimu kama vile nchi kuwa VITANI au majanga makubwa. Zitto kama kijana wa Kitanzania kama haoni umuhimu wa hili basi hakuna namna nyingine ya kumsaidia."

Majibu:

Msomaji utaona dhahiri kuwa hakuna Hoja ya kujibu hapo. Hivi CNN inaagizwa kisheria Na Serikali ya Marekani kuhusu kulinda Nchi Yao? Hivi hapa Tanzania kuna Chombo cha habari binafsi ambacho kinaweza kwenda kinyume Na Nchi wakati wa vita? Muswada umetaja vita? Maelezo ya Waziri yanaonyesha dhahiri kuwa Serikali haina Hoja bali inahangaika kuokoteza Hoja. Kwenye hili Sina la kujibu majibu yamo ndani ya maelezo Yao.

4. Kwamba muswada unampa Waziri wa Habari majukumu ya kutoa masharti kwa kazi za vyombo vya habari na kwamba anaweza kuamua gazeti lichapishwe habari aitakayo.
Muswada huu hauna kifungu hicho zaidi ya Waziri kupewa uwezo wa kisheria, kama ilivyo katika sheria nyingine, kutunga kanuni za kutekeleza sheria hii. Hili nalo Zitto hataki!

Majibu:

Nimeeleza huko juu kuhusu Mamlaka haya ya Waziri wa Habari. Kifungu cha 60 kipo wazi sana.

5. ...muswada huu unampa mamlaka Waziri kuzuia chapisho au kitabu fulani kisisambazwe nchini:
Ni kweli muswada umetoa mamlaka hayo lakini Zitto ameamua kutosema ukweli wote.

Muswada unampa Waziri mamlaka hayo si kwa kila jarida au kitabu bali yale tu ambayo yamedhihirika kuchapisha habari huku yakivunja sheria za nchi. Kama Zitto anafikiri nchi yetu itaruhusu majarida yanayotaka kuhamamsisha vita na uvunjifu wa amani nchini, ajue hakuna nchi inayoruhusu mambo hayo.

Majibu:

Nadhani wenye uelewa wanaelewa maana ya hili. Sina maelezo ya kujibu hili kwani linajitosheleza.

Nani anatafsiri maslahi ya umma?
Nani atafsiri kuwa sheria za Nchi zimevunjwa Kama sio mahakama?
Kwanini kabla ya Waziri kufungia vitabu au magazeti asipate amri ya mahakama?
Yeye Waziri Ni Nani Mpaka atoe tafsiri ya kitabu Fulani au gazeti Fulani limevunja sheria?

6. Kuhusu kuwepo kwa vifungu vya uchochezi akitoa tafsiri kuwa wabunge wa upinzani watabanwa:
Kwanza katika hili lazima ijulikane kuwa kwa mujibu wa mikataba ya kimataifa ukiwemo Mkataba wa Kimataifa Juu ya Haki za Kisiasa na Kiraia wa mwaka 1966, masuala yote yanayohusu kusababisha athari kwa usalama wa taifa ni ukomo unaokubalika wa uhuru wa habari (allowable restriction to press freedom).

Majibu:

Sina maelezo katika hili. Wenye uelewa wanaelewa namna Hoja za namna hii hutumika.

Kiufupi masuala yote ya uchochezi yaliyokuwa kwenye sheria kandamizi ya magazeti ya mwaka 1976 yamerudishwa kwenye sheria hii mpya.

Sheria hii inakwenda mbali Na kusema "Hata ukitamka jambo ambalo linaweza kujenga chuki ya Wananchi dhidi ya Serikali Ni uchochezi".

Mwisho:


Napenda kutoa ushauri wa bure Kwa ndg. Nape Nnauye, kwamba kujadiliana Kwa Hoja kuna Maslahi Kwa Nchi.

Wote waliosoma andiko langu wataweza kutofautisha vijembe, dharau, kulewa madaraka Na matusi kwenye majibu ya Nape Na Hoja kwenye andiko langu. Katika andiko langu sikumtaja Nape Kwa jina Kwa sababu najua anatimiza wajibu wake Kama Waziri.

Katika majibu yake kuanzia mwanzo Mpaka mwisho Ni vijembe tu. Hii inaonyesha uwezo wetu mdogo wa kuhimili mijadala. Hii Ndio inayofanya Watanzania tuonekane watu ambao hatukusoma au tulikwenda shule lakini hatukuelimika.

Haiwezekani kwamba mtu yeyote ambaye ana Hoja tofauti Na wewe atakuwa ametumwa. Kwamba hatuna uhuru wa mawazo binafsi Na hivyo lazima tutumwe. Hii Ni hulka mbaya sana ambao sikutegemea Kama wanasiasa vijana wanaweza kuiendeleza. Lakini Kama kuna mtu ambaye amezoea kutumwa Hoja Ni dhahiri kwamba anaona mwengine yeyote mwenye Hoja nyengine katumwa Pia.

Ninaamini muswada huu Ni mbaya Na unadidimiza uhuru wa habari. Ninaamini kuwa muswada huu Kama ulivyo haupaswi kujadiliwa Na Bunge Kwa sababu unapaswa kuandikwa upya.

Muswada huu ukipitishwa hakuna mchapishaji(printer) wa magazeti atakayekubali kuchapisha magazeti sababu Kwa mujibu wa muswada Mkurugenzi wa Maelezo anaweza kuingia kwenye mtambo wowote akiwa Na Polisi Na kuung'oa. Haya sio kwamba hayajaanza kufanyika, yamefanyika.

Wakati wa masuala ya UKUTA kuna wachapishaji walikataa kuchapisha gazeti lolote lililokuwa na neno UKUTA. Watu wa magazeti wanajua hili Na wanaweza kuthibitisha Kwa namna wanayoona inafaa.

Mimi nimeandika. Nimetahadharisha. Nimetimiza wajibu wangu.

Zitto Kabwe
Njiani kwenda Maputo
21/10/2016
 

Attachments

  • 1474021216-A BILL - THE MEDIA SERVICES ACT, 2016.pdf
    641.5 KB · Views: 176
Uwezo wa Zitto na wa Nape ni vitu viwili tofauti kabisa.
Najaribu sana kutokua na position katika majadiliano haya, kilichoniumiza ni kuona wanasiasa vijana, wakifikia hapa, where is our tomorrow, wakati matumaini yetu walau yalikua kwa vijana. Ni kweli majibishano haya yamekosa uungwana. Napenda tu kukumbusha kwamba hii siyo Tanzania tunayoitaka' wote Zitto na Nape waliwahi kuwa wadau wa kipindi kilichowahi kuheshimika hapa Tanzania, na hakijapanda mpinzani hadi leo, Kipindi cha Tanzania Tunayoitaka, mimi nikiwa moderator wenu. Mlipingana kwa hoja na kwa heshima na kwa kuweka maslahi ya vijana wenzenu mbele. Historia yenu katika taifa hili imeandikwa clearly. Kupitia kipindi kile Kila kijana wa Kitanzania, alikuwa anavutiwa na utashi wenu, na mkawa mashujaa wa taifa letu, na role models. wakati huo,

Where is that Legacy?
I must confess, you were both my pride and made this national, a pride. Mdogo wangu Nape, wakati wa vita yako wewe tulikutia moyo tukawa upande wako, dhidi ya nguvu kubwa iliyokuwa kinyume nawe, tusingeweza peke yetu, tulikua tunasimamia haki, mungu akaonekana akakutetetea, tukafurahi pamoja, leo una dhamana kubwa kwa nchi yetu. Mdogo wangu Zitto, wakati ukipitia magumu ndani ya chama chako, ukionekana uko peke yako, pamoja na kuwa ulikua unashindana na nguvu kubwa, usingeweza peke yako, tulisimama pia pale tulipoona, hapako sawa, mungu akakutetea ukarudi tena bungen, leo unadhana kubwa kwa nchi yetu. Sisi ni sauti zilizo nyikani, mimi ni mtumwa nisiye na faida, naongea kama dada, vijana wengi leo wamekua makini kwa sababu ya mchango wenu. Muswada wa Habari ni roho ya taifa letu, hata sisi ambao pengine hatuna nafasi kama zenu. Mungu awasaidie sana mufanye sawa na matarajio ya taifa hili, upole, kuheshimiana, moyo wa kunyenyekea ndio naomfurahisha mungu. Naweza kuonekana nina upande, ni kweli, upande wangu ni ule wenye 'nia njema' kwa taifa letu, lakini cha muhimu, acheni malumbano ya kwenye mitandao mnawakatisha tamaa vijana wenzenu na hata sisi wakubwa zenu ( kwa umri maana kwa vyeo hatuwawezi).

Yatosha, Tusonge Mbele!
Sisi hatuwezi kujua nani kati yenu anayetumiwa kama mnavyodai. Mungu ndio anayeijua mioyo yenu, kama kuna yeyote kati yenu anayetumiwa, iwe na watoa muswada huu ama wadau wake, mungu akutane nae. Nawaomba, kama dada tu wala sina mamlaka, msiendelee na mjadala huu hapa mtandaoni, mnatuumiza na mtazidi kuwagawa vijana wenzenu na taifa badala ya kutujenga. Hakuna mshindi katika maslahi ya taifa kwa kuwa wote tu abiria. Nawapenda wote na kuwaombea, you can do better than this and make Tanzania, the Country We Want! PEACE, naomba na sisi wengine tuachie hapa tusishabikie tuonyeshe maturity yetu kama taifa, marafiki wa viongozi hawa pia mko wapi mbona mko kimya? Tanzania Nchi Yetu!
 
Nape wewe huna nia njema na watanzania lakini unasahau kitu kimoja unapotunga sheria kali za kukandamiza uhuru wa watu kupata habari kisa wewe ni waziri ni makosa.

Angalia sasa bunge baada ya kutoa bunge live bunge limekosa changamoto kuibana serikali, wabunge mahudhurio ni hafifu bungeni.

Ulisema bunge linafanya wananchi hawafanyi kazi tazama sasa kwenu hapo serikalini wanafunzi wamekosa mkopo mmewapa wachache, mahospitali hakuna madawa kwasabbu hamna hela,uchumi wa nchi umeyumba hakuna biashara tena.

Wakati ukiwa mwenezi wa CCM haujawa mbunge ulikuwa na wivu sana ukiwaona wabunge Kama Mnyika, Zitto, Halima Mdee, Silinde wakiwa wanaisimamia serikali vizuri. Ulipopata uwaziri hasira yako ya kwanza ni kuzima bunge live eti watu hawafanyi kazi, sasa mbona nyie mmefilisika mpaka pesa za kuwapa mkopo wanafunzi mmeshindwa.

Wakati wa jk bunge live ilikuwepo, watu wako free wanafurahia nchi Yao kutoa maoni, wewe unakuja na hasira zako na sheria za ajabu ajabu utafikiri umeongea na Mungu utadumu milele na wewe awamu yako itapita tu, lakini msilazimushe fikra zenu eti ndo sahihi kwa kila kitu.

Mnakosea
 
I am really ashamed to read some statements.. Nchi hii haina maadili tena? Nchi hii haifundishi tena kwamba utumishi wa umma una miiko na misingi yake, ikiwa ni pamoja na kuwaheshimu unaowaongoza na kutumia lugha za staha? Kama Waziri angesema tu "Anashukuru kwa maoni aliyotoa Mh. Zitto, na serikali itayafayia kazi kulingana na uzito wake" angenyang'anywa uwaziri wake??? Nasema tu hivi kwa sababu Waziri kutoa majibu kwa staili hapo juu, ni kujiweka kwenye public spot na kuchochoe wasomaji wengi kuanza kukukosoa, kitu ambacho kisingetokea kama angejibu kwa staha. Why not save your public image?
 
.., nimeshawishika na majibu ya Zitto Zubeiry Kabwe kwa sasa.., wakati akimjibu Nape Nnauye bandiko lake..,

Baada ya kuusoma muswada wa sheria wa huduma za habari, wa mwaka 2016.., ulio katika lugha ya Kiswahili..

.., awali nilianza kushawishika kuwa Zitto labda kajitungia kwa sababu anazozijua mwenyewe au ana ajenda ya siri.., kumbe sivyo!

Lakini ufafanuzi wake katika bandiko lake nimeuelewa sasa na kubaini kwamba:

_1. Tunahitaji tuuone mswaada (bill) ule ulio katika lugha ya Kiingereza._

_2. Tunahitaji kujua kama taratibu za kibunge na kiserikali katika miswaada zilikiukwa katika ushirikiswaji wa Wadau._

_3. Mswaada huu ni tricky kama hufikirii outside the box._

_4. Muda wa kuupitia kwa umakini zaidi unahitajika kuliko huo uliotolewa na kamati ya Bunge._

_5. Ikiwezekana muswada huo wa huduma za habari wa mwaka 2016, uahirishwe hadi mwakani..., watu wajadili_

_6. Ushirikishwaji wa dhahiri na ulio wa wazi kwa wadau wote wa habari, ambao muswada huu unawahusu_

_7. Hakuna haraka ya kwenda mbele na kutaka vikao vya bunge wiki ijayo viupitishe.., tujipe muda, tusipitishe kwa mihemko_

_8. Wiki moja waliyopewa wadau kutoka kwenye kamati ya kudumu kujadili kwa kina na kuleta mapendekezo yao katika kamati ya bunge hautoshi_

_9. Inaonekana kuna mambo mengi ya ujanja ujanja ambayo yamefichwa na serikali na yamewekwa kwenye muswada huu kwa ujanja mwingi, ni very tricky bill_

_10. Tazama sehemu ya 7(1)(b)(iv) inatamka wazi kwamba waziri anaweza kuagiza chombo chochote cha habari cha binafsi kutangaza habari fulani au masuala fulani yenye umuhimu iwa taifa_

_*kitu kibaya zaidi katika eneo hilo muswada unatamka wazi sana kwamba waziri mwenye dhamana ataweka Vigezo (terms) na masharti (conditions) kwa uendeshaji wa 'media houses'*_

_Yaani maana yake ni kwamba, waziri anaweza kuamua ITV au Channel 10 (mfano) itangaze habari fulani na habari fulani isitangazwe kamwe.., au wajiunge na TBC kuonyesha habari za usiku kwa kujiunga na TBC mubashara!_

Watanzania.., acheni kulala.., hebu tafuteni muswada wa sheria wa huduma za habari 2016.., tupige kelele.., tuwasaidie wana habari na sisi pia... Bunge hili lina wabunge mizigo wengi ambao kimsingi hawawezi kusema hapana.., wataunga mkono, haswaa wabunge kutoka upande ule wa kijani na njano (wazee wa masauti)...


Martin Maranja Masese (MMM)
 
Wanasiasa vijana wanatutia aibu majuzi RC Gambo na Lema walidhihirisha vijana bado sana.Leo Nape na Zitto wanatupeleka kule kule kwamba vijana kukabidhiwa madaraka makubwa ni sawa na kumkabidhi fisi bucha.

Katika hili niko na Zitto naona kabisa Nape anataka kutunyamazisha kupitia sheria kandamizi kama hizi.Hataki watu wasema,hataki mawazo tofauti,hataki mawazo mbadala..Watanzania watatakiwa kuishi kama manyumbu hakuna kupinga jambo kila kitu cha serekali kitatakiwa kupigiwa makofi hata kama ni kibovu.

Ifike wakati Nape na wanasiasa wajue kwamba watanzania wanapenda uhuru wa kujadiliana,wanapenda kusikia mawazo mbadala toka pande zote.......ndio maana watu kama mimi sijawahi kuitazama TBC1 huu ni mwaka wa pili kwakuwa ni television iliyokosa ubunifu,isiyopenda kutupatia mawazo tofauti na serekali inachotaka.TBC1 ya kiwango cha juu ilikuwa enzi za Tido hii ya sasa inahitaji moyo kuitazama na kuisikiliza.TBC1 imeacha kuonyesha live bunge lakini inaonyesha live harusi,kitchen party !.
 
Mkuu hakuna mswada ambao ni siri.. Ule wa mafuta na gesi mbona uliletwa in time? Zitto aombwe alete huo muswada
Screenshot_2016-10-21-12-01-12.png
 
Mbona sasa sielewi hapa, mmetoa muswada ili 'wadau' watoe maoni sasa wanatoa hayo maoni mnaanza kuwaita wanafiki, wapotoshaji na waongo!!! Au mlitegemea wasihoji chochote kwenye hiyo draft?

Au turudi kwenye drawing board, kwani wadau ni akina nani!? Je, Mh. Zitto hana vigezo vya kuitwa 'mdau'!!!?
 
Mbona sasa sielewi hapa, mmetoa muswada ili 'wadau' watoe maoni sasa wanatoa hayo maoni mnaanza kuwaitwa wanafiki, wapotoshaji na waongo!!! Au mlitemea wasihoji chochote kwenye hiyo draft?

Au turudi kwenye drawing board, kwani wadau ni akina nani!? Je, Mh. Zitto hana vigezo vya kuitwa 'mdau'!!!?
Sasa ni zamu ya wadau kutoa maoni kwenye Kamati ya Bunge, Zitto badala ya kukaa na Kamati ya bunge kutoa maoni yuko kwenye mitandao anamwaga upupu kama vile kwenye kamati ni kwa moto. Aingie kwenye vikao aonyeshe umahiri wake wa kurekebisha mswaada.
 
Nape nnauye ameuvagaa mkenge kwa Zitto
Sasa ni dhahiri serikali kupitia waziri imeamua kumpa nape mamlaka ya kimahakama ya kuamua hiki kiandikwe na hiki kisiandikwe, mswada huu ni kiama cha Uhuru wa habari wale washabikiaji wajue huu ni msumeno utakata kote , serikali ya ccm imetufikisha hapa kwa uoga wa kukosolewa na hii ni dhahiri kuna jeraha la uchaguzi mkuu uliopita , jeraha hili linawauma sana ccm wanapambana kwa kila hali kuhakikisha hawatajeruliwa tena ... serikali ya ccm inaamini vyombo vya habari na mitandao ni chanzo cha jeraha walilolipata kwenye uchaguzi mkuu uliopita.
Nape bila aibu anatokwa povu kushadadia ofisi yake ipewe mamlaka ya kuidhinisha kipi cha kuandika na kipi sio cha kuandika,
Imagine Nape ni katibu mwenezi wa ccm alafu anatakiwa aidhinishe andiko la maoni ya kafulila kuhusu hali ya kisiasa nchini waziri amekua mtemi au chief au mfalme wa wapi mpaka apewe mamlaka yote hayo?
Dhambi hii na ibaki mikononi mwa wabunge wa CCM wenye majority votes bungeni pamoja na yeyote anayesupport mswada huu kusomwa bungeni
 
Sina uhakika kama wanaweza kutengeneza muswada wa kutoa uhuru kwa vyombo vya habari. Itakuwa maajabu ya dunia kama CCM watatengeneza mswada utakao tetea vyombo vya habari na siyo kuvikandamiza.

CCM itakuwa imezaliwa upya kama watapata nafasi ya kutengeneza sheria na watoe uhuru kwa wanahabari kuwakosoa. Nina imani anachochotetea zito kina ukweli, namtia moyo aendelee kupambana ili kuwe na uhuru katika kupata habari.

Kama waliweza kufungia magazeti, kufungia bunge live, cyber crime ambayo inatesa watu wengi tu, leo hii wapate nafasi ya kutengeneza mswada ndo watetea wana habari. Kukubali hili unaweza kuwa yule mmoja kati ya wanne katika ule utafiti wa uchizi:(o_O
 
Mbona sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 haiongelei kama Zitto alivyohoji?

Alafu muswaada huu kutaka kumpa Waziri mamlaka ya kuzuia uchapishwaji wa vitabu na majarida kwa uamuzi tu wa Waziri utakuwa na tofauti gani na hii sheria mbovu ya magazeti ya mwaka 76 ambayo tunaona jinsi inavyotumika vibaya hivi sasa?

Kwanini tuendelee kumpa Waziri wa Habari mamlaka ya Kimahakama ya kuamua hiki kichapishwe na hiki kisichapishwe?
 
Nape ni janga kwa taifa hili changa Zitto alieleza vizuri kabisa...


Huyu anauma na kupuliza.....

Huu mswada ni uhaini wa hali ya juu serikali itakaoufanya kwa wananchi wake....

Nape usiwafanye watanzania ni mafala Mimi binafsi nimeshauona .......

Wacha nije niumwage hapa.....

Nasisitiza zitto yupo sahihi.....
 
Final analysis;

Mnataka kuidhibiti sekta ya habari ifanye mpendavyo watawala wetu

Hampendi kuambiwa mnachofanya siyo sawa,mnataka kusifiwa tuu
Tatizo letu hatusomi ila tunapenda kuchangia. Tafuteni huo mswada muusome na muuelewe ndio mkomenti. Kama hujasoma huo muswada na unapinga ufafanuzi inabidi useme kifungu fulani kinasema hivi, hivyo kitasababisha moja mbili na pia utoe pendekezo maybe kingekuwa hivi ama kiondolewe. Mengine yote ni porojo na upuuzi usio na tija kwa maslahi ya taifa hili.
 
Tatizo letu hatusomi ila tunapenda kuchangia. Tafuteni huo mswada muusome na muuelewe ndio mkomenti. Kama hujasoma huo muswada na unapinga ufafanuzi inabidi useme kifungu fulani kinasema hivi, hivyo kitasababisha moja mbili na pia utoe pendekezo maybe kingekuwa hivi ama kiondolewe. Mengine yote ni porojo na upuuzi usio na tija kwa maslahi ya taifa hili.
Hatuna shid wala muda wa kufanya hivyo, maadamu tunaowapenda na kuwaamini wamesema hata kama wanatudanganya kwetu sawa tu. Ndivyo Wa Tanzania tulivyo Blah blah kwetu mtaji tuonekane tupo duniani
 
bunge live now bunge off, alie ripot njaa karagwe aliojiwa, juzi juzi tu hapa mwandsh wa Azamtv ndaniii zitto alioji juu ya bunge kuwa off akaojiwa na kamati ya maadili so tutegemee nn kipya, over my dead body hakuna jipya, nchi zenye kutaka maoni ya wadau na wananchi kwa ujumla huo mswada ungetolewa miez hata miwili nyuma ili watu wazomeee na kuelewa lakn hapa kwetu kila kitu ni mwendokasi mwendokasi tutasubiri sana watz
 
Dada Rosemarym Mwakitwange, sijakuelewa sis, sasa unawaambia waondoke huku kwenye mitandao ni sahihi kweli sis? Huoni kwamba kwa Zito kuileta hii issue hapa imewafanya watu wengi wamekuwa-aware nayo? Hata ile ya VAT watu wengi walikuwa aware na issue nzima ya kodi na VAT baada ya zito kuleta ile habari kwenye mitandao...
Sasa kama wanajadiliana kwa hoja hapa online kuna shida gani? Hapa si inatupa chance wadau wengine kujua linaloendelea na kushiriki? Si ni kama tu walivyokuwa wanalumbana kwenye ile TV programme yako? Sema tu hapa shida ni nape yeye hajikiti kwenye hoja anajikita kwenye kumkejeli mwenzake... yeye unamshauri nini basi? Sasa kama unashauri kwamba mjadala usiendelee hapa kwenye mtandao, basi uendelee wapi ili na sie wengine tujue kinachoendelea? Basi fanya mpango uwaandalie programme kwenye TV wakajadiliane huko ili na wadau wengine washiriki.

Je sis, pamoja na kuwaombea kwa Mungu wafanye sawa na matarajio ya taifa, wewe kama mdau wa habari unauongeleaje huo mswada na vifungu vyake?
 
Back
Top Bottom