Mungu hasikilizi Sala ya mtu muovu bila ya kufanya toba kwanza

Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
3,197
7,674
Leo Rais Samia akiwa Mwanza, akishirikiana na viongozi wa dini, wamefanya sala ya kuombea Taifa lipate mvua.

Ninachoshangaa, ni kwa nini hawa viongozi wa dini hawawi wakweli wa nafsi zao ambazo zinatakiwa kusikiliza zaidi maneno ya Mungu kuliko kumfurahisha mtawala wa kidunia.

Maandiko yapo wazi. Mungu hasikilizi sala ya mtu mwovu, mtu anayedhulumu nafsi na haki za watu. Nchi hii imejaa dhuluma. Tumerundika watu mahabusu kwa kuwaonea, tunawafungulia kesi za kubumba, tunatumia hovyo pesa za wananchi kwaajili ya kesi za kubambikia, halafu tunaenda kumwomba Mungu.

Neno la Mungu linasema, kabla hujamwendea Mungu, nenda ukayamalize nduguyo. Wapo mamia magerezani na mahabusu kwa uonevu, na kwa kesi za kubumba. Leo hii Tanzania ukitaka uende mahabusu haraka sana, basi uwe CHADEMA halafu umkosoe Rais na Serikali kwa ujumla.

1 Peter 3:12 says, "For the eyes of the Lord are on the righteous and his ears are attentive to their prayer, but the face of the Lord is against those who do evil."

Kama tunataka maombi yetu yasikilizwe na Mungu, ilitakiwa kutanguliwa na toba. Na kabla ya toba, tuondoe dhuluma. Tukawaondoe waliopo magerezani na mahabusu kwa kesi za kutengeneza. Tuka-denounce ushirikiano na watu waovu wanaowabambikia watu kesi. Baada ya hayo ndipo tumwendee Mungu kwa unyenyekevu, tukiwa na dhamira ya moyoni ya kuturudia tuliyoyatubia.

Kwenda mbele za Mungu kuomba mvua, huku tukiwa tumejaa dhuluma, tumewarundika watu mahabusu na magerezani, huku tukijua kabisa kuwa tunawaonea, tujue tunafanya kufuru. Na anayefanya kufuru, baada ya maisha ya hapa Duniani, kwake ni jehanamu;

'Proverbs 15:8 (DBY) The prayer of a sinner is an abomination unto God.

Kwa hiyo sala ya leo ya huko Mwanza ni kufuru mbele za Mungu.
 
Mungu ukimuomba akusamehe dhambi zako husamehe moja kwa moja lakini na wewe usizikumbuke tena (If you ask God to forgive your sins, God forgives your sins for all, but also do not remember your sins any more) swali fikirishi, je hao wanao omba wanaouwezo wa kutozikumbuka dhambi zao?
 
Maendeleo katika taifa yanaletwa na sayansi pamoja na mipango bora, sio maombi, sio vinginevyo.
Kwenye jicho la kiimani tunasema, 'Mungu hawezi kutenda badala ya yako. Kuna wajibu tunaotakiwa kuutimiza. Tunapoyafanya hayo, tunaomba Mungu aweke baraka juu yake"
 
Angefanya sala ya toba mwezi wa saba mvua ingenyesha tungesema kweli mungu kapokea maombi ya rais wetu lakini maombi miezi hii wakati ndo miezi ya mvua ni kutufanyia usanii
 
Watanzania mbona vigeu geu sana,nakumbuka kipindi Cha kuingiza nchini chanjo za corona watawala waliponda Sana kutegemea mungu pekee,wakaenda mbele zaidi kwa kudai Ni upumbavu ambao magufuliiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii ametukaririsha was kutegemea mungu asiyeoneka na badala ya sayansi,Cha ajabu Sana walewale walioponda falsafa ya magufuliiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii yakutegemea mungu,leo mnaomba mungu awape mvua,sayansi haina dili Tena,Bora mungu ashushe mapigo tu si kwa ukigeugeu huu!!!!!!
 
Back
Top Bottom