george aloyce
JF-Expert Member
- Aug 22, 2017
- 1,302
- 2,015
Mama Jennifer shikamoo. Mimi naitwa Lila (sio jina halisi) na kabla ya kuja Dar nilikuwa naishi kijijini kwetu mkoani Singida.
Mwaka jana nilibahatika kuchumbiwa na kijana anayeitwa Shiradi ambaye tumesoma naye shule ya msingi ingawa hatukuwa darasa moja yeye alikuwa mbele yangu ila hatukuwa na mazoea wala mahusiano yoyote. Yeye alipomaliza shule ya msingi alikwenda mjini kutafuta maisha. Mwaka jana alirudi akiwa amevaa sare za jeshi na kuja kuniposa kwa wazazi wangu. Mimi na wazazi tulikubali na akapangiwa kulipa mahari ambayo wazazi wake walilipa kwani haikuwa fedha bali ng'ombe.
Tulikuja mjini baada ya kufunga ndoa ya kimila na nilifurahi sana nikijua maisha yangu yanakwenda kubadilika kwa kuwa mwenzangu ana kazi na mshahara mzuri.
Tangu tufike Dar huku Mbagala sijawahi kumwona mume wangu akienda kazini huko jeshini! Maisha magumu, hela anaacha 3000 haitoshi na hajawahi kuleta mshahara. Ndipo nikapata mashaka na kumbana na sasa amenambia ukweli kuwa yeye si mwanajeshi ni mbeba mizigo sokoni Tandale na yale mavazi aliazima tu. Nimevunjika moyo sana kwa uongo huu na sina hamu tena na ndoa maana mimi nilimkubali sababu ni mwanajeshi nikajua nakuja kula kivulini sasa kama mtu mwenyewe mbeba mizigo sokoni naona ndoa itanishinda.
Unanishaurije...?