Mayonene
JF-Expert Member
- Mar 16, 2016
- 1,595
- 1,419
Ngoja tuone huo utaratibu mpya leo nimesikia kuwa hakuna tena matibabu ya bure lazima mgojwa achangie ( gazeti la mwananchi la leo) mchango ni 60%. Ninavyojua mimi chakula kwa mgonjwa ni sehemu ya tiba. Tanzania ina zalisha maskini wengi sana kadri tunavyokwenda mbele. Sehemu kubwa ya mafanikio ni stasticks tu. Tunaongeza idadi ya mashule huku tunapunguza ubora elimu tunayotoa ( kielelelezo ni matokeo, yakiwa mabaya tunabadilisha taratibu kwa kupanua gori) tunaongeza vituo vya afya huku tukipunguza ubora wa huduma etc etc. Tunakounda kugumu kuliko tunakotoka ingewezekana mimi ningerudi tunakotoka.Lazima ulipie elfu 30000 kwa ajili ya chakula kwa siku tatu kama mgonjwa wako atalazwa. Ni upfront payment, kama huna mgonjwa wako halazwi.
Maswali ya kujiuliza
1. Kama chakula wanachotoa sitaki nitafanyaje. Mfano mimi nataka supu asubuhi, mchana maini na jioni kuku je watanipa?
2. Je wenye bima na bina tunajua haihusiki na chakula cha mgonjwa bali matibabu na dawa itakuwaje.
Nadhani hii ni namna ya kusema watuwasiende mujimbili kutibiwa.