Mtwara: Mganga Mfawidhi asimamishwa kazi kwa kuwaambia Wagonjwa yeye ana Roho Mbaya kuliko wanavyofikiri

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,591
8,810

View: https://www.instagram.com/reel/C1rIUPsi23K/?igsh=ZWI2YzEzYmMxYg%3D%3D

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Abeid Abeid Kafunda, amemsimamisha kazi Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Mkwajuni Isabella Renatus kutokana na madai ya kutokuwa na kauli nzuri kwa Wagonjwa huku akijisifu kuwa ana roho mbaya na kwakuwa Wananchi walimshtaki kwa Wakubwa zake wa kazi sasa amedhamiria kuwaonesha kuwa ana roho mbaya zaidi ya wanavyodhani.

Mkurugenzi huyo amesema amemsimamisha ili kupisha uchunguzi wa tuhuma inayomkabili baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa Ismaili Shamte Mkazi wa Mkwajuni kuwa Mtumishi huyo wa Afya aligoma kumpa huduma alipoenda kuchoma sindano kituoni hapo huku Isabella akijisifu kuwa yeye ana roho mbaya na hatompa huduma anayoitaka.

Baada ya kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya Mkurugenzi na Mlalamikaji kwenye kikao cha pamoja, Isabella amesema aliongea hayo yote kwa utani lakini Mkurugenzi amesema hakuna utani wa aina hiyo maana baada ya majibizano ya hapa na pale, Mzee huyo hakutibiwa tena na akaondoka.

Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili, Mkurugenzi Kafunda ametoa maamuzi ya kumsimamisha kazi Isabella na kutaka uchunguzi ufanyike kutokana na tuhuma hizo.
 
Si afadhali alikataa kumhudumia huyo mzee, angeweza kumchoma sindano ya insulin au hewa kwenye mshipa w damu.

Apewe onyo kisha ahamiswe kituo, afanye kazi chini ya uangalizi kwa mwaka mmoja, ikionekana anafanya vizuri basi maisha yendelee. Hao wauguzi nao ni watu, wana stress za maisha kama watu wengine.
 
Si afadhali alikataa kumhudumia huyo mzee, angeweza kumchoma sindano ya insulin au hewa kwenye mshipa w damu.

Apewe onyo kisha ahamiswe kituo, afanye kazi chini ya uangalizi kwa mwaka mmoja, ikionekana anafanya vizuri basi maisha yendelee. Hao wauguzi nao ni watu, wana stress za maisha kama watu wengine.
Kabisa inaweza kuwa siku iyo kuna mtu alimchanganya.
 
Ndio hapo unapoambiwa mkubwa M/Mungu pekee na muda ndio unaoongea
 
Back
Top Bottom