Mtu wa kwanza kuwepo duniani alikuwa na urefu wa kilometa nne na upana wa kifua mita mia tatu

TAJIRI MKUU WA MATAJIRI

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
7,281
14,071
MAELEZO YA FUMBAKASA NA MWASI KWA NCHI YA ROBASASTA AU KONGO KWA LEO

FUMBAKASA alitambulika kua mtu wa kwanza hapa duniani akiwa na urefu wa km4 na upana wa kifua chake ni mita mia3, akiwa na rangi nyeusi. Mwenye asili ya nywele ngumu zisimamazo kwa umbile lake.
Pia MWASI ndio mwanamke wa kwanza kutoka kwa FUMBAKASA akiwa na rangi ya pink. Aliye na nywele laini zilalazo mwilini mwake. Ambayo rangi ya pink ndio uoto wa rangi nyeupe kwa sasa.
Mwanamke huyu alianza kua na urefu wa mita za kawaida mia tano na kuongezeka kufikia km3.5 kwa maana ya makuzi kutoka kwa mtu wa kwanza na upana wa kifua chake ni mita 240.

ROBASASTA inatambulika kama nchi ya kongo au zaire kwa leo. Nchi hiyo mtu wa kwanza alimzaa MWANZALULE NA MPANGOLO.
Na hao ndio walikua watoto wa kwanza katika nchi hiyo. Na hao watoto walifanikiwa kuzaa baada ya makuzi yao na kupata watoto mapacha 36, watoto mapacha 10 aliwazaa katika eneo la PUNGU ambalo ni pori la FIZI kwa sasa huko KONGO na watoto wengine mapacha 10 aliwazaa katika eneo la KISONGANI ndani ya kongo hiyo hiyo na watoto wengine mapacha 10 aliwazaa katika eneo la MATADI na mapacha wengine 6 aliwazaa sehemu iitwayo EKORO ambayo ndio EKWATERE kwa sasa.

Basi watoto hawa walizalika kwa mfumo wa mapacha mapacha na kila mmoja kupewa shamba lake baada ya makuzi. Majina ya watoto hao ni kama ifuatavyo kutoka pacha wa kwanza hadi pacha wa 36.
1-RUKUKA NA ZUMBA
2-KILOMO NA CHABANGA
3-ZUMELE NA KISHE
4-ABOGA NA NAKOROLO
5-KISEULE NA BOMBO
6-SHABANGA NA KAMBANGO
7-LUTO MA DUWIGERE
8-SABORO NA NIYONGOMO
9-MBOMA NA LUWITERE
10-SESE NA GAMBAYO
11-ZAOMO NA MTALO
12-LUBE NA CHIBENGA
13-GABA NA MUSOLELE
14-RINGAMAI NA MAISE
15-FOVO NA ZIKALANGO
16-MBANDA NA LUTABA
17-ZIMBERE NA KAFUMU
18-KWAYOKOO NA NDEREMI
19-SOLOGHI NA MWINHANA
20-SUPE NA BAMBALOLO
21-KABOO NA KABOLOSA
22-M'BONDOO NA ESHIMYA
23-FWAILE NA MISEROO
24-MUTIKIMBI NA ZABRAA
25-NGUMBALO NA ZEVE
26-KORONGO NA ZEZE
27-MILIYALA NA KABOTOLA
28-OBAMI NA ZIMBAMI
29-BIRAGO NA NYESHE
30-MSEMBO NA LWIZE
31-KISANGA NA PERE
32-KIBOMBOLO NA RUSEME
33-KABANGA NA MWETE
34-KIKONDE NA DAPARARA
35-KABOKALAMU NA SUMEMBE
36-HIROYE NA GABHY.

Hao ndio walikua wajukuu wa FUMBAKASA au mtu wa kwanza katika aridhi ya ROBASASTA au KONGO kwa leo. Watoto hawa wa MWANZALULE NA MPANGOLO Wapo 72 kwa vizazi 36.
Basi historia iliendelea kwa kufuata usia kwa maana ya kila watoto wakifia umri wa kujimudu hiyo kale ilikua wanapewa mashamba kwa vieneo vyao kwa kukuza uzawa. Basi kila mmoja walipofikia hatamu waligawiwa maeneo yao kama urithi kwa sasa. Na kila eneo lililogawiwa kwa wakati huo lilipata jina baada ya mrithi kuwepo.
Basi ndugu hao waliishi kwa kutembeleana na kufahamiana kwa machache lakini kila mtu akiwa na mke wake na kupewa majukumu zaidi.
 
Chai ya moto hii
 

Attachments

  • 20240707_094520.jpg
    20240707_094520.jpg
    93.7 KB · Views: 4
Kuna jamaa yetu alikuwa anatumia mihadarati akamkataa mamake, akasema yeye aliibiwa eti alikuwa na pacha wake na pacha wake ni Jay Zee
 
Back
Top Bottom