Mjanja M1
JF-Expert Member
- Oct 7, 2018
- 4,023
- 14,177
Kuna msemo unaosema ukistaajabu ya Musa basi utayaona ya Firauni, tukio la Baba mzazi mkazi wa mtaa wa Mafisa, Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kudaiwa kumuweka unyumba mtoto wake wa kike wa miaka mitatu limewachukiza wengi huku baadhi ya wananchi wakiiomba serikali kuchukua hatua kali zaidi kwa mtuhumiwa huyo ili iwe fundisho kwa wengine
Mtoto huyo wa miaka mitatu ambaye jina lake limehifadhiwa, inaelezwa ameanza kupitia maswaibu angali bado akiwa kinda (mdogo sana) ambapo majirani wanasema taratibu walianza kumuona Baba wa mtoto huyo akioga na mwanaye mara kwa mara na hatimaye kuanza kumfanyia ukatili, huku wakisema licha ya Mama kupenyezewa taarifa hizo lakini hakujali.
Mwenyekiti wa mtaa wa Mafisa, Salum Hamadi amesema tayari wameshamfikisha Baba huyo mikononi mwa Jeshi la Polisi, ambapo Jeshi hilo mkoani Morogoro limekiri kumshikilia Baba wa mtoto huyo kwa uchunguzi zaidi.
Source - JamboTv