Jerrymsigwa
JF-Expert Member
- Jun 23, 2012
- 14,083
- 8,374
Wakuu mtoto ananipa wakati mgumu sana, ana wiki 6 sasa na amekua analia sana usiku yani kilio cha yowe kabisa.
Nimejaribu kumpa dawa 'infacol' na bonnisan lakini tatizo bado liko pale pale shida itakua nn? Hizo dawa nimepewa baada ya kumuona pediatrician.
Alafu mida yake sasa ni kuanzia sa 7,8, 9 mpk sa10 tu kila siku. Mchana halii kabisa kabisa, daah ananipa wkt mgumu sana huyu mtoto.
Naomba uzoefu please
Mkuu mimi ni mkristomkuu sory wewe ni muislam au mkristo
Pole sana mkuu
Hiyo hali mara nyingi hutokea kwa baadhi ya watoto, jaribu kumtafutia kifaa hiki "baby pacifier" kinaweza kusaidia kupunguza tatizo lkn uwe makini asikizoee sana sbb navyo nadhani vinamadhara kama matumizi yatazidi
Lakn pia kama utaweza muache alie usimbembeleze anapoanza kulia baada ya muda ataacha mwenyewe japo siyo rahisi lkn pia inasaidia
Kama kushiba mtoto huyu anashiba mpk maziwa yanavuja kwa mama ake. Sasa sijui labda kujaribu kusuppliment hiyo maziwa ya kopo. Asante sana kwa ushauri mkuuLabda mtoto hashibi, niliwahi kumuona mama mmoja akihojiwa kuhusu mtoto wake aliyekuwa anasumbua sana usiku wa manane kwa kulia hata masaa mawili/matatu akahangaika huku na kule kwa madaktari bila ahueni yoyote mpaka alipokutana na daktari aliyemwambia huyu mtoto kote ulikopita hawakuona tatizo la kiafya mchana anashinda vizuri kabisa usiku wa manane ndiyo anaangusha kilio. daktari akasema labda mtoto hashibi jaribu kuhakikisha mtoto anashiba na labda maziwa yako hayamtoshi hivyo alimshauri anunue maziwa ya kopo. Yule mama akadai baada ya kuanza kumpa mtoto maziwa ya kopo pamoja na ya kwake kulia usiku wa manane kukafikia ukomo.
Mkuu huyu ni jinsia ya kike, ni mtoto wa2 na dada yake hakuwahi sumbua kiasi kama hikiTafadhali elezea jinsia ya Mtoto. Kwa mujibu wa maelezo yako nahisi ni mwanaume please confirm then nikushauri.
Duh jina gani sasa mkuu? hiyo sijawah sikia kbsniliwahi kusikia eti mtoto akilia usiku basi anakuwa analilia jina
MziziMkavu na mshana jr hivi hizo kulilia jina zipo kweli a...?
Ulichokiongea ndio uhalisia wenyewe wa mambo, hakuna uchawi hapo! Wampe mtoto maziwa ya kutosha halafu waache kumfunga pampas, wamwache awe huru, wakati mwingine mtoto analia kumbe ni pampas imelowa au imefungwa vibaya plus njaa, Kweli mtoto asilie?Labda mtoto hashibi, niliwahi kumuona mama mmoja akihojiwa kuhusu mtoto wake aliyekuwa anasumbua sana usiku wa manane kwa kulia hata masaa mawili/matatu akahangaika huku na kule kwa madaktari bila ahueni yoyote mpaka alipokutana na daktari aliyemwambia huyu mtoto kote ulikopita hawakuona tatizo la kiafya mchana anashinda vizuri kabisa usiku wa manane ndiyo anaangusha kilio. daktari akasema labda mtoto hashibi jaribu kuhakikisha mtoto anashiba na labda maziwa yako hayamtoshi hivyo alimshauri anunue maziwa ya kopo. Yule mama akadai baada ya kuanza kumpa mtoto maziwa ya kopo pamoja na ya kwake kulia usiku wa manane kukafikia ukomo.
Wakati mwingine huwa ni mepesi sana kutegemeana na msosi wa Mama, Aache kwanza kula chips yaiKama kushiba mtoto huyu anashiba mpk maziwa yanavuja kwa mama ake. Sasa sijui labda kujaribu kusuppliment hiyo maziwa ya kopo. Asante sana kwa ushauri mkuu
choo kawaida tu, ila gesi ni mojawapo ya sababu coz huwa anajamba jamba sana. Hata ivyo niliambiwa na Doc kua Bonissan ndio inamaliza gesi tumboni. Cha ajabu ni kuwa mchana anakua poa sana isipokua ikifika sa 6-10 ni balaa mtoto anapiga yowe ni vile tu naishi nyumba sehem ambapo sio rahisi kusumbua jiraniVipi kitumbo chake hakimumi gesi? Na vipi choo anapata kikawaida?
mkuu nashukuru sana kwa ushauri wako kwa kweli Mungu awabariki wote kwa ushauri huu. Nimeuchukua na nitaleta feedback kuanzia usiku wa leo.Ulichokiongea ndio uhalisia wenyewe wa mambo, hakuna uchawi hapo! Wampe mtoto maziwa ya kutosha halafu waache kumfunga pampas, wamwache awe huru, wakati mwingine mtoto analia kumbe ni pampas imelowa au imefungwa vibaya plus njaa, Kweli mtoto asilie?
Usimfunge hayo madude please, muache kabisa aiseeemkuu nashukuru sana kwa ushauri wako kwa kweli Mungu awabariki wote kwa ushauri huu. Nimeuchukua na nitaleta feedback kuanzia usiku wa leo.
Diapers ni rahisi zaidi kumsaidia mtoto kwani kuna wakati anakua na frequent pee so badala ya kubadili nepi inasaidia kumbaidili kwa mda kidogo.
nimeshauriwa asile vitu vyenye asidi mfano maziwa mgando, broccoli, cauliflower, malimao, machungwa, maharage, juice, lemonade nk viepukwe. Chips nooo haliWakati mwingine huwa ni mepesi sana kutegemeana na msosi wa Mama, Aache kwanza kula chips yai
Thanks, notedUsimfunge hayo madude please, muache kabisa aiseee