Mtoto auawa kwa kupigwa fimbo na baba wa kambo

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Mwanafunzi wa chekechea shule ya msingi Ilunga amefariki dunia baada ya kupigwa fimbo na baba yake wa kambo wilayani Magu mkoani Mwanza.



Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed Msangi

Taarifa ya jeshi la polisi imeeleza kuwa mnamo tarehe 27.06.2016 majira ya saa 12:00 jioni katika kitongoji cha Moha kijiji cha Ilungu kata ya Nyigogo tarafa ya Itumbili wilaya ya Magu mkoani Mwanza, mtoto aliyejulikana kwa jina la Julius Leonard miaka [7] mwanafunzi wa chekechea shule ya msingi ilunga aliuawa kwa kupigwa fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake na baba yake wa kambo aitwaye Leonard Joseph miaka [32] mkulima na mkazi wa kijiji cha Ilunga.

Inadaiwa kuwa marehemu alitumwa na baba yake huyo wa kambo kwenda kuchukua betrii ya simu iliyokuwa imepelekwa kuchajiwa ndipo alichelewa kurudi nyumbani hali iliyopelekea baba yake huyo kuwa na hasira na kuamua kumchapa hadi mtoto huyo akapoteza maisha.

Mwili wa marehemu tayari umefanyiwa uchunguzi wa awali na daktari na kuonekana ukiwa na alama za fimbo huku mguu wa kushoto ukionekana kuvuja damu kwa ndani kutokana na adhabu ya fimbo hizo.

Mtuhumiwa wa mauaji hayo ametoroka baada ya kuona amefanya mauaji.

Jeshi la polisi linaendelea na upelelezi pamoja na uchunguzi kuhusiana natukio hilo, huku msako wa kumsaka na kumtia nguvuni mtuhumiwa wa mauaji tajwa hapo juu ukiwa unaendelea.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed Msangi anatoa wito kwa wananchi akiwataka kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi, kwa kutoa taarifa za mtuhumiwa wa mauaji haya mahali alipo ili awezwe kukamatwa na kufikishwa

Chanzo: ITV
 
Jamani huu ni ukatili wa hali ya juu sana. Kuchelewa tu? Ndio ndio raha ya utoto ukitumwa lazima ucheze kidogo njiani
 
Hivi huu mkoa wa Mwanza unamabalaa gani, kila kukicha matukio ya kikatili hayaishi kutokea!! Nadhani tungemuachia tu Idi Amin aendelee nao kuliko doa liwekwalo na matukio ya mkoa huu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…